Yusuf Makamba: Mbunge mzuri anaweza kutoka chama chochote! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yusuf Makamba: Mbunge mzuri anaweza kutoka chama chochote!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sir.JAPHET, Aug 5, 2012.

 1. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #1
  Aug 5, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]GAZETI LA MWANACHI LIMEANDIKA Makamba: Maisha bora hayawezi kuletwa na JK ,,
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Sunday, 05 August 2012 01:11 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Fidelis Butahe
  BAADA ya kimya cha muda mrefu, Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba ameibuka na kusema kuwa maisha bora kwa kila Mtanzania hayawezi kuletwa na Rais Jakaya Kikwete.

  Amesema kuwa mbunge mzuri anaweza kutoka chama chochote iwapo Watanzania watashirikiana naye katika kuleta maendeleo ya eneo husika.

  Makamba ametoa kauli hiyo ikiwa imepita muda mrefu tangu aibuke katika kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho (Nec) na kumtuhumu Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kwamba amekigeuza chama kuwa mali yake binafsi.

Katika kikao hicho Makamba alisema hatua ya Nape kugeuza chama hicho kama taasisi yake binafsi ndiyo ambayo imesababisha kikose mwelekeo.


  Lakini jana wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya mwanaye, January ambaye ni Mbunge wa Bumbuli na Naibu Waziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia kufungua mkutano wa wakazi wa jimbo hilo, Makamba alisema maendeleo ya Watanzania yataletwa na wao wenyewe, kwa kufanya kazi.

  Huku akizungumza baadhi ya maneno kwa lugha ya kisambaa na kunukuu baadhi ya vifungu vya biblia takatifu, Makamba alisema Watanzania wamekuwa wavivu wa kufanya kazi na kwamba kila kitu wanategemea kitafanywa na Rais Kikwete.

  Makamba alisema kuwa kwa sasa kumezuka tabia ya baadhi ya Watanzania kuwatupia lawama viongozi kwa kushindwa kuwapa maisha bora.
  
Makamba, alisema kuwa maendeleo hayawezi kuletwa na mbunge peke yake bali kinachohitajika ni ushirikiano wa pamoja ili kuweza kutimiza lengo na ahadi mbalimbali alizotoa.
  
Alisema kuwa anashangazwa na baadhi ya Watanzania kuamua kumtupia lawama Rais Kikwete kuwa kashindwa kuleta maisha bora wakati hawana umoja wa kuunganisha nguvu katika kutatua changamoto zinazoikabili nchi.
  
"Hata kama CCM itaondoka madarakani na kuingia Chadema bado Watanzania wataendelea kulia umaskini kwa kuwa hatuna tabia ya kushirikiana na kufanya kazi," alisema Makamba.
  
Makamba alimwagia sifa mwanaye, January ambaye alikuwa akizindua Shirika la Maendeleo Bumbuli (SMB)ambalo alilianzisha baada ya kuwa mbunge mwaka 2010, kusema kuwa kijana huyo ni mfano wa kuigwa na Watanzania kwa kuwa katika kipindi kifupi cha uongozi wake jimboni humo ameweza kutekeleza ahadi mbalimbali.

  Alisema kuwa wananchi wa Bumbuli hawakufanya makosa kumchagua mbunge huyo na kuongeza kwamba wanatakiwa kumpa ushirikiano ili kulifanya jimbo hilo kupiga hatua kimaendeleo.

  Kwa upande wake, January wakati akiwakaribisha wakazi wa Bumbuli pamoja na waliotoka mikoa jirani, alisema kuwa wamekutana ili kuangalia namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo jimboni humo.
  
Alisema kuwa siku zote maendeleo huletwa na wakazi waliopo mbali na nyumbani hivyo aliwaomba kuhakikisha kuwa na umoja ili kuondoa matatizo yaliyopo jimboni humo ikiwa ni pamoja elimu, afya, miundombinu na maji.
  
Alisema kwa upande wake atahakikisha BDC, linawasaidia wakazi hao katika masuala ya ajira na elimu.

  Alisisitiza kuwa ili kuinua kiwango cha ufaulu katika jimbo hilo wamebuni njia ya kupandisha ufaulu wa wanafunzi kwani kuanzia sasa wameanzisha kambi ya wanafunzi zaidi ya 150 waliofanya vizuri katika mitihani yao ya mokono ili kuwanoa zaidi, lengo likiwa ni kuhakikisha wanafanya vizru katika mtihani wao wa mwisho.

  
Januari ambaye ni Naibu Waziri wa Sayansi na Mawasiliano, alisema kuwa wamegundua kuwa baadhi ya wazazi jimboni humo wamekuwa kikwazo cha wanafunzi kushindwa kufanya vema mitihani yao.
  
aliongeza kuwa BDC imepata fedha kiasi cha Sh 730 milioni kwa ajili ya kukusanya na kununua mazao ya mboga mboga yaliyopo jimboni humo, hatua ambayo itasaidia kununuliwa kipato cha wakulima.
  

  Alisema hatua hiyo itakwenda sambamba na kukifufua kiwanda cha matunda cha Maweni ambapo mkulima ataweza kuuza mazao yao huko na kuepukana na madalali na kwamba vijana zaidi ya 120 watapata ajira.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #2
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,908
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  Shetani akizeeka anakuwa Malaika..!
   
 3. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #3
  Aug 5, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mmmmmh atiii nin?
   
 4. R.B

  R.B JF-Expert Member

  #4
  Aug 5, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 6,163
  Likes Received: 1,098
  Trophy Points: 280
  BAADA ya kimya cha muda mrefu, Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba ameibuka na kusema kuwa maisha bora kwa kila Mtanzania hayawezi kuletwa na Rais Jakaya Kikwete.

  Amesema kuwa mbunge mzuri anaweza kutoka chama chochote iwapo Watanzania watashirikiana naye katika kuleta maendeleo ya eneo husika.

  Makamba ametoa kauli hiyo ikiwa imepita muda mrefu tangu aibuke katika kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho (Nec) na kumtuhumu Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kwamba amekigeuza chama kuwa mali yake binafsi.

Katika kikao hicho Makamba alisema hatua ya Nape kugeuza chama hicho kama taasisi yake binafsi ndiyo ambayo imesababisha kikose mwelekeo.


   
 5. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #5
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Anatafuta cheo، kachelewa asubiri rais wa a
  wamu ya Tano labda atamkumbuka.
   
 6. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #6
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,296
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  What a comment
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  nchi inachezewa na watoto, nasi twazwtizama tu.
   
 8. PROFESA KYANDO

  PROFESA KYANDO Member

  #8
  Aug 5, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  hujasomeka mkuu!!
   
 9. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #9
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,072
  Likes Received: 10,429
  Trophy Points: 280
  ha ha ha ha ha ha....
   
 10. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #10
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hivi huyu mzee bado watu wanamsikilizaga... Apumzike awaachie vijana ccm waiendeshe.. Angemchukua na mukama na yeye akapumzike vijana waendeshe chama
   
 11. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #11
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,769
  Trophy Points: 280
  maendeleo ya wanabumbuli yanajadiliwa dar kivipi???
   
 12. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #12
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Acha utani! He is expired na hafai hata kwa mbolea. Incineration is the only option
   
 13. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  kwa kutumia mkonga wa mawasiliano.

  Anatuma feedback kwa email, skype na wassap.

  Tuna safari ndefu.

   
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  mwandiko wangu mbaya??

   
 15. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #15
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,315
  Likes Received: 2,601
  Trophy Points: 280
  Wakiwa madarakani hawafanyi lolote la maana, waking'atuka hawaishi kutoa kasoro
   
 16. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 31,778
  Likes Received: 36,769
  Trophy Points: 280

  hichi ni kiini macho,
  mwanakijiji hana hata umeme sasa atajuijulia wapi skype?
  Huyu dogo aliomba kura kwa twitter??
  Tuna safari ndefu sana.
   
 17. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #17
  Aug 5, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,084
  Likes Received: 601
  Trophy Points: 280
  january ni mbinafsi ni waziri wa tanzania sio bumburi pekee, hata wasambaa amewagawa? mradi usingefaa lushoto yote?

  ok basi ajenge nyumb yake bumbuli sio mbezi beach
   
 18. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #18
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  watoto wa viongozi, kila kiongozi wa juu ccm wa sasa au aliyepita mtoto wake anakasehemu ka kuchezea sarikalini. Anaweza kupewa ubunge, ukuu wa wilaya n.k.
   
 19. a

  annalolo JF-Expert Member

  #19
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hivyi kumbe bado yupo. mbna hiki cheo cha katibu mkuu ni waropokaji sana. namkumbuka alivyokuwa katibu mkuu alivyokuwa mropokaji na mukama same story
   
 20. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #20
  Aug 6, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,067
  Likes Received: 1,803
  Trophy Points: 280
  ingawa ni mbunge wa viti maalum! Letcia nyerere ana ishi wapi..?? matatizo ya watanzania yajadiliwa kule anapoishi ...?
   
Loading...