Yussuf Manji: Kingunge ni mnafiki, alilikata jina lake uchaguzi 2005!

Kingunge ni muasisi wa Chama Cha Mapinduzi, wewe kadi yako ni namba ngapi hadi uwe na uwezo wa kumnyoonshea kidole?

Nyie ndiye mnayemtangaza kuwa Edo ni fisadi, maana ishu ya Richmond anayotuhumiwa nayo, ameshaiweka clear na mwenye Richmond hata wewe unamjua! Yule alietutangazia alivyoenda USA alionana na wenye Richmond, aje atueleze ni kinanani alioonana nao?

Waasisi wa chama Karume na Nyerere walishakufa

Kuhusu Edo Lissu ndiye aliyemuandika kwenye list of shame na Mbowe akiwa kiongozi wa kambi pinzani aliongoza jopo kumnadi Lowassa kuwa FISADI au uongo?
 
Katika kipindi cha Power Breakfast leo asubuhi, Yussuf Manji wa Yanga amemtuhumu mzee Kingunge kuwa si mkweli na anahisia za kinafiki.

Amesema mwaka 2005, yeye Yussuf Manji alipata kura za kutosha kabisa katika mapendekezo ya kuwania jimbo la Kigamboni.

Kingunge wakati huo akiwa Kingunge wa kweli, alitumika kulikata jina lake , ati kwa kisingizio cha umri.

Hiyo ni licha ya wana CCM kumkubali katika kura za mapendekezo.

Ameshangaa sasa iweje leo Kingunge huyo huyo anaialia kwa Jina la Lowassa kukatwa alimradi yeye alianzisha mtindo huo, na hatimaye kukimbilia UKAWA.

MY TAKE
What goes around comes around!

Hata waswahili walisema mtenda hutendwa, mkuki mtamu kwa nguruwe, kwa binadamu mchungu.

Asante Manji kwa kutukumbusha hili.
Kwa nini mtu akitoka kwenye chamacha sias ndiyo uonekana mbaya? Mbona Yusuf hakuyasema haya kabla!
 
Acha upuuzi... Kukaa karibu Na kanisa sio kusali au kufika mbinguni wewe.

Kingunge Leo ndo mpinzani!? Watu wananuona Shujaa.. Afu watu waliousimamisha upinzani mnawaona vikaragosi.

Chagua Magufuli 25/10

Kingunge na wenzie ndio waliiunda hiyo CCM, kama ni sala basi yeye ni miongoni mwa waliozitunga!

Ndiyo, Kingunge leo ni mpinzani.......na hakuna wa kumbishia, wewe kadi yako ni namba ngapi ili useme unaijua CCM kuliko yeye? Kaona kuna madudu CCM kaamua ajiondoe, na huo ndio ushujaa ambao utadumu katika historia ya nchi hii kwenye medani za siasa!

Magufuli ni mtendaji mzuri sana wa kazi, tatizo chama alichopo ndiyo shida! Chagua Lowasa
 
Waasisi wa chama Karume na Nyerere walishakufa

Kuhusu Edo Lissu ndiye aliyemuandika kwenye list of shame na Mbowe akiwa kiongozi wa kambi pinzani aliongoza jopo kumnadi Lowassa kuwa FISADI au uongo?

Inaweza ikawa kweli, lakini mwisho wake imekuja kudhihirika Edo sio Richnd jambo ambalo lilimfanya aitwe fisadi!

Katika hiyo List of Shame, walikuwa 11, mmoja (1) EL kaenda CDM waliobakia kumi (10) wote wamebakia CCM! Si bora ukichague chama chenye fisadi mmoja kuliko chenye mafisadi kumi!
 
Manji anatafuta kichaka cha kufichia wizi wake

.
Alipeleka mil 700 na ushee Dodoma kumpitisha Membe zikakamatwa na walioamua kujitundika kwa kuikataa mila ya chama cha majambazi ccm.
Halafu huyu ndie aliekabiziwa jukumu la ushauri wa kibiashara wa familiya ya mkuu wa kaya.
anataftiwa umeya?
.
 
kwani kuwa na kadi namba nane ndio haukosei au?ulafi wa hela unamsumbua huyu alishaonyesha mahaba mapema na lowassa kundi la friends of lowassa linaratibiwa je hakuona katiba inakiukwa je alishatoka hadharani kulisema zaidi alitoka mzee malechela,je kuwanunua wenyeviti wa chama wa mkoa ndo utaratibu wa chama unasema hvyo?je kingunge alitoka hadharani kulisemea hili?tutumie akili mzee alishaonyesha mahaba mapema kabisa na lowassa je kuhudhuria mkutano wa mgombea kutangaza nia nao ni utaratibu wa chama?kwann hakuhudhuria kwa wengine?kingunge mnafiki na mchumia tumbo!

Edo alishaona kuna mbinu zinafanyika tangu awali ili asigombee urais hivyo kitendo chake cha kununua hao unaosema ilikuwa ni njia ya kujihami na uonevu huo!

Hicho unachokiita wewe mahaba, kingunge alikiona mapema kama "kuonewa ama kuchezewa rafu" kwa Edo...!

-Mbona hapakuwa na mtu aliyenyanyua mdomo wake kusema Edo anachezewa rafu?

-Edo alikuwa anatukanwa na vijana wadogo wenye umri kama watoto wake tena hadharani, na hakuna aliyekemea alichokuwa anafanyiwa! Tena hao waliomtukana wengine walipewa na vyeo!

-Kwani ni kosa mtu kumpenda mtu Fulani awe rais? Kwani Membe hakupendwa na watu?
 
Kila zama na kitabu chake dogo!! everything happens for a reason and a good one at that! time is a deciding factor; wakati ukiwadia, ndio hapo pahala pa kuchukua hatua; the challenge to most of us mere mortals ni kutambua huo muda muafaka!!

Nikikutoa kwenye siasa nikakupeleka kwenye masumbwi kidogo; Lenox Lewis; boxing champion kutoka Uingereza aliujua wakati wake wa kustaafu masumbwi; so has Money man Mayweather! They have lefty the scene as legends; greats and kings of boxing and very rich as well, lakini Iron Mike Tyson hakuujua muda muafaka wa kustaafu ndondi, alilazimika kustaafu ndondi kwa aibu kubwa baada ya kupokea kipigo cha mbwa; na kafilisika mpaka hata kujaribu kucheza wrestling; patupu!!

Kingunge ameeleza wazi msimamo wake kwamba kati ya wagombea wote kupitia CCM, yeye anaamini ni Lowassa aliyekua na uwezo na nafasi nzuri zaidi ya kuleta mabadiliko, siwezi kusema yuko sahihi au la, bali huo ndio msimamo wake! lakini pia amesema wazi kuwa kilichomchukiza zaidi hadi kufikia maamuzi hayo; sio Edward kukatwa bali kusiginwa kwa katiba waliyojiwekea wana CCM kuhusu mchakato huo! that was the genie that broke the camels back! akasema enough is enough! akajiondoa na wakati sisi tupo hapa jamvini muda mfupi uliopita balozi anayeheshimika katika medani za diplomasia na katibu mkuu mstaafu wa jumuia ya afrika mashariki EAC; Juma Mwapachu keshabwaga manyanga; kajitoa CCM na kasema maneno almost kama yale yale ya kingunge; CCM kubinafsishwa na kupoteza mwelekeo!

Lakini kaka mwaka 1995 wakati mzee Kingunge akiwa latibu wa itikadi na uenezi. Mzee Malecela aliondolewa kwenye orodha ya wagombea urais kwa shinikizo la mwalimu nyerere ambaye kwa wakati huo hakuwa na wadhifa wowote,je hiyo haikuwa uvunjifu wa katiba?atuambie ni lini hasa ubinafsishwaji na ukiukwaji wa katiba ulianza ccm?
 
Inaweza ikawa kweli, lakini mwisho wake imekuja kudhihirika Edo sio Richnd jambo ambalo lilimfanya aitwe fisadi!

Katika hiyo List of Shame, walikuwa 11, mmoja (1) EL kaenda CDM waliobakia kumi (10) wote wamebakia CCM! Si bora ukichague chama chenye fisadi mmoja kuliko chenye mafisadi kumi!

Tatizo lililokuwepo si ndani ya mfumo wa chama, ila ni ndani ya mfumo wa serikali. Maana hao mafisadi hawakihujumu chama pekee, bali pia wanaihujumu nchi. Hivyo basi kutokuwepo na mfumo mzuri wa sheria na taratibu za kuwawajibisha mafisadi ndio uliotufikisha hapa

Kwa kulijua hilo Magufuli amekuwa akihubiri ufisadi, rushwa na wizi kwamba ataanzisha mfumo wa kushuhulika nao kwa kuanzishamahakama itakayodili n mafisadi tu, ninao anafaa kwa kuwa anahubiri hilo na utashi wake unaonekana pale anapokemea.

Ila ndugu EDO suala hili limekuwa zito kulizungumzia mara kwa mara, hivyo nina wasi wasi kwamba nikimpa kura huenda akazalisha mafisadi waliojificha zaidi, ni bora muadilifu mmoja atawanyoosha wengine kuliko mchafu mmoja awaambukize tabia chafu, kwa kuwa yeyey ndiye atakayekuwa baba wa nyumba
 
- Chama legelege huzaa serikali legelege! Mapungufu yaliopo serikalini yanatokana na mfumo wa CCM!

- Hivi unaujua ufisadi wa nyumba za serikali, hadi watu kuwauzia vimada na ndugu zao wasio stahili?

-Unajua ufisadi wa vivuko chakavu chini ya huyo unayemtaja?

-Unajua viwango duni vya barabara za lami zilizojengwa chini ya huyo?

-Unajua ufisadi wa karibu ya tshs Bil 250 zilizopotea chini ya wizara yake, kwa mujibu wa ripoti ya CAG?
 
Fisadi hizo zote japo ni kashfa lakini fisadi ya RICHMOND, iliyodumu kwa miaka na nane unaifumbia macho, na kama mfumo wa CCM hao wanaouona ni MBOVU nao walikuwa humo humo na wakashiriki kuunda sasa leo inakuwaje wajaribu kutuaminisha kwamba wao walikuwa wasafi na hawakushiriki, kama umewaamini hao waliokuwa na kashfa karibuni muongo mzima, basi mimi nawaamini ninaowaamini. Sinunuliwi, maana kuna sehemu chama kimenunuliwa sasa wanacham sijui mtafanywa nini kama si KUUZWA
 
1. RICHMOND mwenyewe ni = https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/932504-tundu-lissu-richmond-ni-ya-rais-kikwete-21.html

2. Hata kama walitenda dhambi wakiwa huko, sasa wametubu na wamekuwa watu wapya! Yaani wamezaliwa upya!

3. Nani anauza na kuuwa tembo wetu kwa ajili ya pembe? Nani wameuza madini yetu na kuacha mashimo wazi? Ukishawajua, basi hao ndio wakuogopa maana wameuza kila kitu!
 
Hata mimi najiuliza swali kama hilo kwa Lowassa.
Hadhi ya Udiwani na Urais vinalingana ? Huyo Lowasa unayemtaja katika siku zote za maisha yake amekuwa mwanasiasa tangu enzi za chipukizi mtiifu kwa chama, huyu mwingine mfanyabiashara tangu enzi za ujana wake, ghafla tu anataka Udiwani !!!
 
Lakini kaka mwaka 1995 wakati mzee Kingunge akiwa latibu wa itikadi na uenezi. Mzee Malecela aliondolewa kwenye orodha ya wagombea urais kwa shinikizo la mwalimu nyerere ambaye kwa wakati huo hakuwa na wadhifa wowote,je hiyo haikuwa uvunjifu wa katiba?atuambie ni lini hasa ubinafsishwaji na ukiukwaji wa katiba ulianza ccm?

Mwacheni mzee Kingunge kapewa mafao na lowasa astaafu vizuri kule ccm angekufa kwa njaa.
 
..nimefurahi tu kujua manji kawa mchambuzi wa siasa ndani ya clouds radio.!!
jamaa wamekaa kisanii sanii kwenye kila kitu, bora wabaki kwenye matamasha tu.
 
Nashindwa kumuelewa Kingunge. Anasema mchakato wa kumtafuta mgombea ndani ya CCM haukufuata demokrasia na taratibu za chama. Je utaratibu wa kumpata mgombea ndani ya CHADEMA ulifuata demokrasia na taratibu za CHAMA? Demokrasia gani anayoihubiri huyu mzee
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom