Yussuf Manji aitapeli manispaa ya Kinondoni

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,462
21,334
Manji akumbwa na balaa
• Manispaa Kinondoni kumfikisha mahakamani


na Betty Kangonga




HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni, inatarajia kumfikisha mahakamani mfanyabiashara maarufu nchini na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Yusuph Manji, kwa kukabidhidhi matela ya kubebea takataka yaliyo chini ya kiwango.

Nia hiyo ya Manispaa ya Kinondoni, ilitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Uwekezaji ya Manispaa hiyo na Diwani wa Kata ya Magomeni, Julian Bujugo, ambaye alibainisha kuwa, halmashauri hiyo ilimpatia zabuni ya kuagiza matela mfanyabiashara huyo, lakini ameshindwa kulinda makubaliano ya mkataba.

Alisema wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kuona Manji hana nia ya kupeleka matela yenye viwango vinavyohitajika au kurejesha kiasi cha shilingi milioni 324 alichopewa kwa ajili ya kazi hiyo.

Bujugo alisema matela 27 yalikusudiwa kusambazwa katika kata zote za wilaya hiyo ili kuiweka manispaa hiyo katika hali ya usafi.

Alisema Manji alitakiwa kukabidhi matela hayo katika muda usiopungua miezi mitatu (Septemba – Desemba 2008), lakini alikiuka taratibu ambapo aliwakabidhi Novemba mwaka huu.

“Zabuni hiyo ilikuwa ni ya kipindi cha miezi mitatu, lakini Manji alikiuka utaratibu huo ambapo imepita zaidi ya mwaka ndiyo anatuletea matela hayo yasiyo na ubora,” alifafanua Bujugo.

Aidha, alisema halmashauri katika mkataba wake na Manji, ilitaka matela yenye matairi manane, lakini mfanyabiashara huyo aliwapelekea matela yenye matairi manne.

“Sisi tuna ushahidi wa kile tulichokiagiza katika makubaliano yetu. Tulihitaji kuletewa matela yenye matairi manane, amechukua muda mrefu anatuletea matela ya matairi manne, hatuyataki,” alieleza.

Alisisitiza kuwa, kamati yake na halmashauri haikuwa tayari kupokea matela hayo na kumshauri Manji kutimiza kile walichokubaliana katika mkataba husika.

Alisema hivi sasa kuna mbinu chafu na ushawishi unaofanywa na mfanyabiashara huyo kwa baadhi ya madiwani ili wakubali kuyapokea matela hayo.

Alibainisha kuwa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ilitoa siku saba kwa Manji kuyaondoa katika eneo yalipowekwa matela hayo na kuleta yale yanayokidhi viwango.

Alidai kwamba pamoja na agizo hilo, mfanyabiashara huyo alishindwa kutimiza masharti aliyopewa, jambo lilioifanya manispaa kufikiria kuchukua hatua za kisheria kuhakikisha jambo hilo linamalizika.

Tanzania Daima Jumatano lilijaribu kumtafuta Manji ili kuzungumzia sakata hilo, lakini simu yake ya mkononi ilipokelewa na mtu aliyejitambulisha kuwa ni msaidizi wake.

Msaidizi huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema Manji hakuwepo ofisini huku akilitaka gazeti limuachie maagizo ili akirudi ampe.

“Ninaomba uniachie ujumbe nitamfikishia na kama atakuwa tayari najua lazima atakupigia,” alieleza msaidizi huyo.

Hata hivyo, msaidizi huyo alishindwa kutimiza ahadi hiyo ambapo hadi Tanzania Daima Jumatano linakwenda mtamboni, hakuna simu yoyote iliyopigwa na Manji.
 
''Alisema Manji alitakiwa kukabidhi matela hayo katika muda usiopungua miezi mitatu (Septemba – Desemba 2008), lakini alikiuka taratibu ambapo aliwakabidhi Novemba mwaka huu.''
=======================================================
Sasa jamani hawa jamaa wanalamika saa hii, kwa nini hwakufuatilia toka kipindi hicho wakati mkataba ulikuwa wa miezi mitatu?This is November 2009
 
''alisema manji alitakiwa kukabidhi matela hayo katika muda usiopungua miezi mitatu (septemba – desemba 2008), lakini alikiuka taratibu ambapo aliwakabidhi novemba mwaka huu.''
=======================================================
sasa jamani hawa jamaa wanalamika saa hii, kwa nini hwakufuatilia toka kipindi hicho wakati mkataba ulikuwa wa miezi mitatu?this is november 2009


hawa halmashauri nao matapeli watupu ndugu ukiona hili ujue watu wamenyimwa chao...
 
huyu Manji ni kariba ya watu kama Rostam Aziz, mimi nashangaa mpaka leo hajakamatwa, wizi wote mkubwa lazima watu hao wawili wahusike vilivyo. ...nchi hii bwana,
 
Wamekatana mshiko hao. Hawana lolote, sie tunawafahamu kwa undani jinsi walivyo, Manispaa hii ndo inaongoza kwa uozo. matela yaliyopita ilikuwa dili ya Mh. L....da, wakamsema weeeeeeeeeeee kisha wakaona dawa ni kuwa kama yeye, umasikini utawaua. Huyu Bujugo si ana kijikampuni chake kinaishia na neno executive. Simwamini hata kidogo.

siasa bwana, wanatafuta pesa za kununulia udiwani. hivi na wewe manji una matatizo gani, dili zingine zinakuchafua tu, au ndo unaonyesha jinsi usivyo mbunifu wa kutafuta pesa kwa njia ya halali. fanya dili za kimataifa ulete pesa Tz sio kuiba za wabongo. Watakuvumilia mwisho wataamua kama Mwamwindi, shauri yako
 
wanaomtetea huyu mukuje .......

Mnaposema ni chuki za fulani tu je mna uhakika?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom