Yupo wapi Ramadhani Mkangala? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yupo wapi Ramadhani Mkangala?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Selous, Oct 17, 2008.

 1. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #1
  Oct 17, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  WanaJF;

  Kama mtu huyu yupo hapa jamvini naomba amwambie Moderator afute hii thread, otherwise naomba kujua mtu huyu yupo wapi na anafanya nini. Nitaanza kumwelezea. Karibu

  Ramadhani Mkangala alikuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa UCLAS (Ardhi University) miaka ya 2001 - 2004. Sikumbuki exactly when but kwa wale waliokuwa mlimani na yule Rais wa DARUSO aliesaliti wanafunzi atakuwa anamjua. Alikuwa anasomea Bsc. Land Management and Valuation. Alisimamishwa kwenye ule mgomo na baadae nikamuona tena na nikamsisitiza but kwa bahati mbaya contacts zake sina.


  Huyu mtu nilipata nafasi nikaongea nae nikamuomba aingie kwenye siasa. Siasa inataka mtu ambae anajua kuongoza, kujenga hoja with reference za watu wanaoheshimika kama Mandela, Nyerere, Nkurumah, convising power, kujitolea n.k. Lakini ukiwa na WOGA uliojengwa na WAZEE WA CCM unaweza ukaogopa. Huyu bwana kwa muda mfupi nilimuona anafaaa. Nakumbuka baada ya yule rais (jina linakuja na kupotea) alipokimbia Rama alipewa muda wa kuongea pale Nkurumah hall alifanya wonder mpaka watu tukajiuliza kwa nini alienda kusomea mambo ya Ardhi Management kule UCLAS.

  Ushauri wangu kama kuna mtu ana contacts zake naomba anitumie kwenye PM yangu nitajitahidi kumtafuta but nashawishi kama hayupo kwenye siasa naomba CHADEMA (Chama ninachoshabikia, sina uanachama na wala si;pendi kwa sasa) mumtafute huyu bwana. You will enjoy kama akiwa moja ya vijana wakishirikiana na akina Zitto na John.

  Naomba kutoa hoja kama kuna mtu ana mawazo na mchango mwingine.

  Asanteni kwa muda wenu
   
 2. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #2
  Oct 17, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu Kichwangumu, hicho ulichosema hapo juu hakijakaa vizuri.

  Kama mliona alitakiwa akasomee mambo ya kuongea, inaonekana jamaa alikuwa mzuri kwa kitu hicho tayari, na hakuhitaji shahada ya kuongea.

  Kama mlitegemea akasomee Siasa, sidhani kama hata hao "watu wanaoheshimika kama Mandela, Nyerere, Nkurumah" unaomfananisha nao walisomea Siasa.

  Kama mlitegemea akasomee kwenye kozi za shuleni kwenu nyinyi hapo, ni nani shule yenu iliwafundisha wakatoka na umahiri kama wa huyu jamaa, na mliwasomesha kozi gani, na wako wapi sasa hivi, na walikuwa wapi siku hiyo alipokuja huyu msomea ardhi akawaacha nyote mmeduwaa ?
   
 3. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #3
  Oct 17, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Ndg; Kuhani

  Kwa mara ya mwisho alionekana Tabata Kisukuru akifanya kazi FINCA 2005. Haya mengine yako ni upungufu wangu na/au watu waliocomment nyakati zile. Hayana uhusiano na Ramadhani Mkangala.

  Najaribu kuibua au kutafuta watu ambao wanaweza wakaenda mbele na kuongea na watu. Sio mimi ambae hapa JF tu nimeficha jina. wewe sina hakika. Mimi siwezi kuwa mwanasiasa kwa kuwa sina karama hio.

  Sio kila aliesoma pale mliman, uclas, mzumbe, sua nk wanafanya kazi walizozisomea. hili ni tatizo la wote. kama ulibahatika wewe kusomea uinjinia na sasa upo huko, basi ni wachache wateule. Na hakuna mtu aliesomea uanasiasa labda sayansi ya siasa yenye kuajiri watu kama washauri wa hao wanasiasa. Hujui kama sura pia ni uanasiasa? Muuliza JK atakwambia

  Asante kwa maoni yako na nitafurahi sana kama unamfahamu huyu bwana mana yatamsaidia sana.
   
 4. H

  HAM Member

  #4
  Oct 17, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Huyu jamaa yuko FINCA hapohapo Dar.Ule mgomo ulikuwa mwaka 2000 na Rais aliyeingia mtini alikuwa ni Kusaga tukaongozwa na mwanadada Emily Kivugo, chini ya Uangalizi wa Gervas Mkili, Magabe Kibiki, Mukangala na Rugemalila ka Kabwe kalikuWEPO NA NDIPO KALIJENGA JINA HAPO.Chakushangaza aliporudi alikuwa Katibu wa DARUSO akayarudia yale aliyokuwa akiyakataa na kuyapinga kabla ya kuwa kiongozi. Ama kweli "wazuri hawajazaliwa"

  Nawasilisha.
   
 5. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #5
  Oct 17, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kichwangumu,

  Hata mimi nimekuwa natafuta sana kujua aliko Mkangala. Ninasikitika kuwa baada ya muda na misukosuko ya kuwakimbia polisi wa Mkapa 2001 na zile kesi kibao wengine tulizopata, nilipotezana na Mkangala lakini pia natumaini kuwa kuna mtu hapa atakuwa anafahamu aliko.
   
 6. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #6
  Oct 17, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mkuu HAM,

  Asante kwa info kuhusu Mkangala. Mbona unatumia lugha kali hivyo dhidi ya mbunge na mwanasiasa kijana ambaye ame-inspire vijana wengi tu nchini kwetu - Zitto Kabwe?
   
 7. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #7
  Oct 17, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mwenzangu Kabwe unayemsema hapa ni Zitto?
  Kama ndio sio vizuri kumtaja namna hiyo, naye anastahili heshma yake hata kama mnakinzana ki sera.
   
 8. Charles Dotter

  Charles Dotter JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2015
  Joined: Apr 16, 2015
  Messages: 741
  Likes Received: 353
  Trophy Points: 80
  UCHAGUZI KULA ZA MAONI CCM JIMBO LA TABORA MJINI

  Heshima kwako selous na wachangiaji mliotangulia,

  Natambua kuwa uzi huu ni wa muda mrefu sana 2008

  Hatimaye huyu kijana amejitokeza katika siasa

  kijana huyu amewakonga miyo vijana wengi sana hapa tabora mpaka nikaamua kuanza kumsearch huyu jamaa na kukutana na uzii huu. kwa kweli huyu jamaa anajua kujenga hoja na pia anajua kujibu hoja ka kujenga nyingine. kwa kifupi jamaa anafaa sana


  I mefikia hatua Aden Rage anazomewa na kijana huyu kushangiliwa kwa nguvu zote..

  kwenye siasa. tuna shukuru kwa uzi wako maaana tumejenga imani baada ya kusoma uzi huu


  [​IMG]
   
 9. Hossam

  Hossam JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2015
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 2,363
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Unapiga kampeni?
   
Loading...