Yupo wapi Professor Silas Lwakabamba Mtanzania Mwanzilishi wa Kigali Institute-KIST

U'Kingunge' ktk academics ni hatari mno! Uishie huko huko kwenye siasa. Luhanga alienda kufundisha UK? Check your facts

Luhanga alikwenda kufundisha Chuo gani huko U.K. na lini.?? Toka aachie huo uVC yupo hapa Mbezi Beach anaswaga Konyagi tu!!!
 
Huyu bwana ni Mnyarwanda au? Yes, I get the picture now. Ndo maana Prof Mshana ameenda huyu bwana alikotoka maana hapa alikuwa kama jiwe lililokataliwa na waashi

Mkuu Ndahani
Hiyo ya kwanza umechorea mstari. Pili huyo Mshana baada ya kuukosa uVC UD aliendesha vita vya msituni kwa takriban mwaka mzima, bahati mbaya yeye na wafuasi wake walisambaratishwa vibaya. Pia wakati ameacha uCADO UD alichanganyikiwa sana akawa analewa sana Arusha maana ni kama alipokonywa uVC. Ila bora akae huko kwa majemedari wa msitu, labda atafanikiwa kujifunza mbinu mpya za kurudi na kukamata uVC
 
Naona Hata hata Wakuu wa kaya wakati wanachagua Ukuu wa UDSM huwa wanatazama nini, Maana Hata Luhanga anaweza kwenda UDOM na kufundisha ua kuendelea kufanya tafiti za hapa na pale katika Maendeleo ya Taifa
 
Huyu Prof. Bisanda kama sijakosea ndio Deputy Vice Chancellor (Academics) wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Nae nasikia alitokea Rwanda.
 
Huyu Prof. Bisanda kama sijakosea ndio Deputy Vice Chancellor (Academics) wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania. Nae nasikia alitokea Rwanda.
Mimi sijui kama anafundisha Open university of Tanzania, Lakini Juzi aliteuliwa na Bodi ya Chuo Kikuu cha Tanzania kuwa mmoja wa watu katika Chuo upande wa Planning
 
Kazi kweli kweli. We need these seniors guys for consultancy in many areas. The more we delay the more we suffer. Young guys, looking what happens to the old colleagues, when they go abroad, they never come back.
Solution...kukimbilia india
 
Mkuu Josh
Prof alirudi nyumbani kujenga taifa. Baada ya KIST kufanikiwa sana sasa yuko National University of Rwanda (NUR) ndio boss. Bado roho na tabia yake njema iko vile vile. I doubt kama atarudi tena Tanzania
kwa heshima anayopewa huyu profesa rwanda,kurudi Tanzania ni ndoto
 
Tuanze utaratibu wa kuwatumia hawa wataalamu sehemu ambazo wao ni strong. Kwa kipindi kirefu wamekuwa watazamaji wa shoo zinazoongozwa na wanasiasa. Kwa kweli wanasiasa wametufelisha, big time.
Wanapoona dreams zao hazitimii wakitoka nje tunawabatiza kuwa sio watanzania. Kuna baadhi yao tungeliwajua vizuri wanafikiri nini hata tusingethubutu kusema sema mambo ya wamefika saa kumi na moja wakapumzike. Hivi Prof kama Idrissa Mshoro, Prof Mshana na Prof Bisanda tumewahi kuonja hata tone la kazi zao? Sio wababaishaji hata kidogo. Ni watu wanaotamani waone knowledge inawafikia walengwa. Chonde chonde kuendelea kuwazarau itatugharimu sisi kwa manufaa ya wengine. Tusijisahau na kujiona kama tumemaliza yote au dawa ya mahitaji yetu watatupa Marekani ambao wanatusifia. Tutagawa rasilimali zetu zote bure kama tukiendelea kuwabeza watu wanaoishi wakiacha living legacy na kuwakumbatia matapeli wa siasa za TZ
 
Huyu Professor tuseme yote ila yupo mbali sana, tuseme tutakavyo lakini tumpe haki yake. Kumbuka kuwa alikuwa Dean wa Kwanza mswahili, kama kawaida vijembe, uhalisia wake na ukabila wa Nyerere vilimfanya akimbie. Kuna mtu ameongelea umri kwa mtu kuwa Professor kwa muda mrefu ni added gain. huyu bwana ni mtanzania ambaye kila miezi sita anaenda kwao likizo tofauti na wasomi wengine wanakimbilia mijini, huyu ni mfugaji katika ukoo wao. Kwa wale makao makuu ya wilaya mpya ya Misenyi, hapo utakuta nyumba nzuri ambayo aliijenga miaka ya 80s. kilometa 3 toka hapo utakuta makazi ya Professor Rwekaza Mukandala hapo Kyaka.

Kuhusu maendeleo ya Rwanda, wako mbali na ni watanzania wengi wamewabeba acha sisi tupige siasa tu.

Kwa anayetaka kuwasiliana naye, Business Card yake ya sasa hivi ni hii hapa, I will try later to send you a scanned card:

NATIONAL UNIVERSITY OF RWANDA

Prof. Silas Lwakabamba

B. Sc, PhD(Leeds), D.Tech(hon) (Glasgow CU), MIET, FWIF, FINIT

Rector

University Avenue
B.P 117 Butare, Rwanda
Tel: +250 530 053 or +250 551 033 07 or + 1 360 519 5629
Fax: +250 530 121

Mobile: +250 083 001 66 or +250 053 001 66 or +1 360 519 5581
Hpuse: +250 530 042

e-mail: rector@nur.ac.rw.
website: www.nur.ac.rw.

Wote mliotaka kujua yupo wapi, habari ndiyo hiyo.
Nawakaribisha Rwanda.
 
Asante sana kwa mchango wako na pia itakuwa busara sana kwa Watanzania kuomba watu kama hawa kurudi hapa Tanzania na kujenga Taifa letu
 
ili tuendelee tunahitaji ARDHI, SIASA SAFI, WATU NA UONGOZI BORA

hapakundikwa elimu bora kwahiyo tusahau elimu hii ndio Tanzania
Sijakuelewa kabisa ukisema kuwa hakuna sehemu iliyoandikwa Elimu?? Una maana gani wewe ulivyosema hapa juu au ndio unajifunza kuandika??
 
Hapana shaka kuwa Bara la Africa limekuwa katika brain illusion kubwa katika miaka yote hiyo na pia kulifanya bara hili kutowekewa wataalamu wengi sana
 
Tatizo letu kubwa tunapenda sana vitu rahisi rahisi, hivyo kuna ulazima wakuona mambo kama haya katika Taifa
 
Tatizo letu kubwa tunapenda sana vitu rahisi rahisi, hivyo kuna ulazima wakuona mambo kama haya katika Taifa

Mkuu Eid Mubarak
Kweli sisi ni watu wa cheap politics, cheap social life, cheap economic gains, cheap thinking, cheap cheap cheap!! Hatutaki kuumiza akili kufikiri, wenye lugha wanasema rahisi ni ya ghali
 
Ndio maana Taifa hili nimeingia gharama kubwa sana kwa sababu ya kupenda cheap stuffs mkuu wangu, Hivyo kuna haja sisi kama Taifa kuona kuwa tunakwenda na kuongeza uwezo wetu wa kufikiria zaidi na kuona Taifa letu linapiga hatua kubwa ya maendeleo
 
Usishangae kusikia hii, professor Lwakabamba baada ya kuanzisha KIST yaani kigali institute of science and technology na kufanikiwa kuunda kitengo cha kuwaandaa wahitimu kwenda kujitegemea uraiani akitumia centre of incubation maalumu iliyosheheni wataalamu,serikali ya Rwanda ilimhamishia chuo kikuu kingine cha serikali NUR kilichoko mjini Butare yaani National University of Rwanda ambacho awali kilianza kififia na sasa kinafanya vizuri sana chini yake akishirikiana na maprofessor wengine watanzania kama Proffessor Masanja mtaallamu wa Namba(mahesabu).
Nilipomtembelea mwaka jana nikiwa na msafara wa wanafunzi wa mwaka wa pili MBA SAUT chuoni kwake NUR proff alinisikitisha jamabo moja, anasema Rwanda imefanikiwa sana kuokoa mazingira kwa kuimarisha matumizi ya BIOgas, na anasema alipojalibu kumshawishi Mh JK kuona kama Tanzania inaweza kuanza hata kwa magereza kutumia nishati hiyo Jk alikubali na kumtuma waziri mmoja kuona jinsi ya kuanza lakini maajabu waziri huyo aliludisha majibu kwa Jk kuwa ni vigumu kutumia BIOgas Tanzania na kumuacha proff akiwa kinywa wazi kwa mshangao maana anachojua yeye Biogas inachohitaji ni Kinyesi ambacho binadamu wote tunafanana!
Huko pia wako watanzania wengine kibao akiwamo prof kaijage,masanja na mushi!
 
Back
Top Bottom