Habari zenu wadau?
Hivi kuna Mtanzania ambaye ameshapata kitambulisho cha Utaifa tangu mchakato uanze?
Kama ndio nijulisheni yafuatayo.
1.kina muda wa kuisha?
2.Umri wa kupewa huanzia miaka mingapi?
3.pindi ukipoteza wapi unapata kingine kipya?
taja matumizi yako kwanza wewe....niambieni enyi wapenzi wa Mungu. Kingunge atakitumia wapi au kwa manufaa gani
Wapendwa wanajamvi, naomba mwongozo. Inakuwaje kwa mtu ambaye amemiss zoezi la upigaji picha kwa ajili ya kitambulisho cha taifa? Nimejikuta kwenye situation hiyo kwakuwa nililazimika kutoka nje ya Dar kwenda mkoani kwa shida ya kifamilia - nauguza. Nawezaje kufanikisha kupata kitambulisho? Mwanzo wa mchakato mzima nilikwenda nao sawa na ratiba zao i.e. kujaza fomu na kupeleka nakala za nyaraka za utambulisho.
Ahsanteni sana kwa taarifa sahihi wadau!
KWAKWELI JF ni zaidi ya Google
Acha dharau wewe!! Google na JF wapi na wapi