Yupo aliepata kitambulisho cha taifa?

Makamee

JF-Expert Member
Nov 29, 2013
2,029
1,191
Habari zenu wadau?
Hivi kuna Mtanzania ambaye ameshapata kitambulisho cha Utaifa tangu mchakato uanze?
Kama ndio nijulisheni yafuatayo.
1.kina muda wa kuisha?
2.Umri wa kupewa huanzia miaka mingapi?
3.pindi ukipoteza wapi unapata kingine kipya?
 
1.miaka 10 ndio validity yake
2.kuanzia miaka 18
3.nenda nida karipoti
 
Habari zenu wadau?
Hivi kuna Mtanzania ambaye ameshapata kitambulisho cha Utaifa tangu mchakato uanze?
Kama ndio nijulisheni yafuatayo.
1.kina muda wa kuisha?
2.Umri wa kupewa huanzia miaka mingapi?
3.pindi ukipoteza wapi unapata kingine kipya?

DSC_1065.JPG

MAMLAKA ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ilianza kutoa Vitambulisho vya Taifa kwa wafuatao:

1. Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.

2. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt.Emmanuel Nchimbi.

3. Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi.

4. Rais Mstaafu awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa

5. Rais Mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume

6. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad

7. Kada wa CCM Mzee Kingunge Ngombale Mwiru

8. Askofu Malasusa wa KKKT

9. Shekhe Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhaj Elihad

10. Mwenyekiti wa CUF Professa Ibrahim Lipumba

11. Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dkt.Ramadhani Dau

12. Mkurugenzi Mkuu wa PPF Bwana William Eriyo

13. nk...

cardwoman.png

Mwonekano wa Mbele
muonekano.png
 
Ahsanteni sana kwa taarifa sahihi wadau!
KWAKWELI JF ni zaidi ya Google
 
Kwa vile vitambulisho nilivyowahi kuviona,vina upungufu wa tarehe ya kuzaliwa.mawazo yangu
 
Wapendwa wanajamvi, naomba mwongozo. Inakuwaje kwa mtu ambaye amemiss zoezi la upigaji picha kwa ajili ya kitambulisho cha taifa? Nimejikuta kwenye situation hiyo kwakuwa nililazimika kutoka nje ya Dar kwenda mkoani kwa shida ya kifamilia - nauguza. Nawezaje kufanikisha kupata kitambulisho? Mwanzo wa mchakato mzima nilikwenda nao sawa na ratiba zao i.e. kujaza fomu na kupeleka nakala za nyaraka za utambulisho.
 
Nafikiri labda mwishoni kutakua na zoezi la kufanya majumuisho kwa wale wote waliokosa.
 
Back
Top Bottom