Yupi Rais bora kati ya marais watano wa Taifa letu Tanzania?

dunguni

Member
Jul 3, 2017
41
95
Nchi yetu imejaliwa kuwa na rasilimali nyingi yakiwemo madini, misitu, milima,mbuga za wanyama,mito mikubwa na midogo,bahari,maziwa,gas nk
Tumefanikiwa kuwa na viongozi wakuu wa nchi watano toka tulipopata Uhuru Mwaka 1961 na viongozi hao walifanya/wamefanya mambo mengi kwa kipindi cha utawala wao na hapa ntaeleza kwa kifupi baadhi ya mambo makubwa waliyofanya

1.Mwalimu Julius Nyerere: Jambo kubwa lililofanywa na baba wa Taifa katika utawala wake na ambalo limetujengea sifa kubwa Duniani ni lile LA kuunganisha familia,makabila,dini na itikadi zetu na kutufanya taifa moja la Tanzania, Kipindi cha mwalimu na hata sasa taifa letu lilijengwa katika usawa,Hutu,udugu na kwamba Tanzania ni moja. Jambo la pili ni kuzisimamia rasilimali zetu huku akiamini zipo ambazo kwa kipindi chake tungeweza kuzivuna na zipo tusizoweza kuzivuna kutokana na uchanga wetu,umaskini wetu,ukosefu wa raslimali watu,mtaji na kukosekana kwa technologia.Mwalimu pia alifanikiwa kuimarisha ulinzi na usalama wa mali zetu pamoja na watanzania kwa ujumla huku akisimamia kwa nguvu zote Sera ya ujamaa na kujitegemea, kusimamia Azimio LA Arusha,kusimamia katiba na kuheshimu utawala wa sheria.Wakati wote anayafanya haya na mengine hakuwa na wapinzani wa nje wakukosoa kile alichokiamini lakini kwa utashi wake alitambua na kuamini katika kuridhika na kidogo unachopata kwani vingi tutaondoka na kuviacha.Hii ililifanya taifa letu kuwa salama mikononi mwake na hata alipolikabidhi taifa MZEE Mwinyi bado hapakutokea MTU aliyekuja na uthibitisho kuwa mwalimu alikwapua Mali zetu na kujinufaisha mwenyewe.

2.Mh. Aly Hassan Mwinyi: Huyu ni mrithi wa baba wa Taifa(MZEE wa Ruksa) , moja ya jambo kubwa alilofanya mkuu huyu wa nchi ni kuzilinda rasilimali zetu kwa kutoruhusu ziingie mikononi mwa watu wasiowaaminifu, kusimamia usalama na ulinzi wa nchi,kuruhusu kuanzishwa mfumo wa vyama vingi nchini,kuruhusu Uhuru wa kujieleza na kuhifadhi katiba ya nchi. Katika kipindi chake paliibuka kundi la wahujumu uchumi ambao walijijengea misingi ya wao au familia zao kuneemeka na rasilimali za taifa letu kwa kujikita au kuwatengenea misingi wafuasi wao waendelee kuwepo na kuishi katika mifumo ya maamuzi ya serikali na baadhi yao walikuwa invisible. Kundi ili lilichangia kwa kiasi kikubwa kukwapua rasilimali za nchi na kupelekea kudorora kwa uchumi.Kama alivyokuwa mwalimu,MZEE Mwinyi akujijenga katika kujilimbikizia mali kwani hadi sasa hakuna uthibitisho wa wazi uliopo kuthibitisha hoja hiyo.

3.Mh. Benjamini Mkapa: Huyu akiwa ni mrithi wa Mhe.Mwinyi alipokea madaraka ya Taifa letu katika kipindi ambacho vuguvugu LA mabadiliko ya kisiasa,kiuchumi,kitamaduni na kitekinologia yalikuwa yapo juu.Alipokea nchi huku akiwa na kundi kubwa la wanaoifahamu nchi wakiwa nje ya chama tawala na nje ya serikali, lakini pia uchumi wa nchi ulikuwa umeyumba kutokana na kupungua kwa udhibiti katika biashara na nyanja nyingine za uchumi kipindi cha mtangulizi wake.Mhe.Mkapa aliamua kusimamia na kuishi kwa Sera ya utandawazi iliyomlazimu kufungua kwa kiasi kikubwa mianya ya uwekezaji kutoka nje na ndani kwenye rasilimali zetu.Wakati anafungua mianya hiyo ya uwekezaji mkubwa taifa lilikuwa halina wataalamu wa kutosha katika sekta zote jambo ambalo lilitupa changamoto kubwa katika taratibu za uwekezaji. Hapa ndipo ilipoingiwa mikataba mingi ambayo kwa namna moja ililenga kulinufaisha Taifa lakini kwa upande mwingine na kwa kuzingatia kukosekana kwa wataalamu mikataba iliyotokana na awamu ya Tatu imekuwa mwiba kwa taifa letu sasa na miaka mingi mbeleni.Lakini kwann mikataba hii inaliumiza taifa? ni kwa sababu ya mambo mawili au matatu, moja ni ubinafsi na ufisadi wa waliongia mikataba tajwa,mbili ni usiri mkubwa uliojengwa katika utoaji wa maamuzi na pia kusaini mikataba hiyo, Tatu ni msukumo wa kisiasa wakutaka kuwaonyesha wananchi nini umefanya ndani ya miaka mitano ili wakupe ridhaa ya kuendelea kubaki madarakani. Pamoja na mhe Mkapa kufungua uwekezaji kwa rasilimali zetu lakini pia ndiye kiongozi aliyeweza kusimamia na kuhakikisha anafanikiwa kujenga miundombinu hasa ya barabara ya kuliunganisha Taifa letu,alifanikiwa kusimamia kodi na mapato ya serikali ,alifanikiwa kulipa kwa kiasi kikubwa deni LA taifa ikiwa ni pamoja na kujenga hoja katika mataifa mengi yaliyokuwa yanatudai na kuifanya nchi yetu kupata msamaha kwa baadhi ya madeni.Kwa kiasi flani aliminya demokrasia lakini pia aliweza kuhakikisha nchi yetu ipo salama hadi anaondoka madarakani. Kuhusu kujimilikisha Mali,bado hakuna uthibitisho mkubwa unaoonyesha kuwa alishiriki kujimilikisha Mali za watanzania kinyume cha sheria

4.Mh. Jakaya Mrisho Kikwete: Huyu naweza mwita baba wa demokrasia,MTU mvumilivu na aliyeweza kuhimili mitikisiko mikubwa ya skendo za ubadhirifu wa Mali za uma ,ubovu wa mikataba,wizi wa rasilimali nk.Baadhi ya mambo yaliyofanywa na kiongoz huyu wa Taifa letu ni kuendeleza ujenzi wa miundombinu hasa barabara kuliunganisha taifa letu Sera hii akiwa ameirithi kwa mtangulizi wake.Katika kipindi chake alifanikiwa kuruhusu kuibuliwa na kuwekwa adharani baadhi ya makosa yaliyotendeka kipindi cha watangulizi wake na hata kipindi yeye akiwa madarakani,baadhi ya skendo kubwa kuibuliwa ni Richmond,EPA,Escrow,Meremeta nk.Pamoja na kuruhusu mambo hayo yawe wazi kwa jamii, ni katika kipindi chake ambapo mianya mingi ya uvujaji mali za umma ilifunguka na hivyo kulifanya taifa kupata hasara kubwa.Yawezekana aliwaamini sana waliochini yake au aliongozwa na misukumo mbali mbali ikiwemo ya uchumi mpana wa dunia kufika maamuzi ambayo baadaye hayakuzaa matunda mazuri, yawezekana pia kuna mambo aliyafanya kwa lengo LA kurescue situation iliyokuwepo kwani ni katika kipindi chake tuliposhuhudia tatizo kubwa LA ukame, tatizo LA umeme,ukosefu wa chakula nk mambo ambayo kwa kiasi kikubwa yalihitaji kuchukuliwa kwa hatua za dharura kuyakabili, ikumbukwe dharura uambatana ukosefu wa maamuzi yaliyo huru.Hoja ya kujimilikisha Mali bado inafanyiwa utafiti ndiyo maana wajuzi wa mambo hawajawahi kutoka adharani kuzitaja Mali alizopata kinyume cha sheria....ILA waliokuwa watendaji chini yake kwa namna moja au nyingine walimwangusha......aliwaamini ila shetani alipata mwanya wakuwaongoza kuliondoa taifa kwenye misingi yake.

5.Mhe. John Pombe Magufuli: Huyu ni mrithi wa Mhe Jakaya Mrisho Kikwete ambaye hadi sasa ana miaka miwili ofisini, tayari kwa kipindi cha miaka hii miwili amefanya mambo ya msingi ambayo tunaweza kujivunia kama:Kurudisha nidhamu ya serikali, kudhibiti rushwa, kuweka adharani ubovu wa mikataba iliyoingiwa na watangulizi wake akiwa na lengo LA kuangalia ni namna gani anaweza kurekebisha japo kwa kiasi kidogo dosari zilizopo kwenye mikataba husika,ameendelea kujenga miundombinu ,amebana matumizi, amesimamia kwa dhati usalama wa nchi na mali zake nk. Bado ni mapema kujua mapungufu ya utawala wake japo wajuzi wa mambo wa naona IPO haja ya yeye kusimamia michakato yote inayohusu rasilimali zza kwa uwazi na kuendeleza Uhuru wa kujieleza lengo likiwa ni kufungua mianya aweze kuwajua binadamu wanaomzunguka pamoja na mapungufu yao lakini kubwa zaidi kujifunza kutoka kwao

Pamoja na yote yaliyofanywa na viongozi tajwa hapo juu utabaini kila mmoja amefanikiwa katika jambo moja na kukwama katika jambo jingine,kufikia hapo naomba tujifunze mambo kadhaa

1.Rais wa awamu ya tatu na kuendlea wanayo changamoto ya kujibu hoja za wananchi za kila siku kwa kutumia rasimali zetu, utawala zao zinaongozwa na mipango ya miaka mitano,hakuna agenda au maono ya kitaifa ya muda Mrefu yanayobebwa katika tawala hizi,kila sekta inasimamiwa kwa sehemu ndogo jambo linalotufanya kila kitu tufanye nusunusu,hakuna agenda ya kitaifa ya kimaendeleo,misingi ya uwazi na uwajibikaji inategemea utashi wa mtawala,muhimili wa bunge kwa kiasi kikubwa umeshindwa kusimamia majukumu yake,serikali pia imejengwa si kwa misingi ya sheria Bali utashi wa kiongoz na ndiyo maana watumishi wale wale Leo wakipongezwa na utawala huu kesho watakosolewa na utawala mwingine,hakuna kujiamini,nk

2.Viongozi wote duniani siyo Mungu bali ni wanadamu ambao wameumbwa na mapungufu.binadamu kwa asili ni wabinafsi,wameumbwa na uchu na tamaa ya kulifikia lile wanaloliamini

2.Mfumo wa sheria katika tawala mbalimbali umewekwa kudhibiti utashi,tamaa,uchu na ubinafsi wa watu katika maisha ya kila siku. Hivyo hakuna binadamu anayepaswa kuishi kwa kufanya atakayo yeye bali tunaishi kwa kufanya yampendezayo Mungu na binadamu wenzetu.Hakutakuwa na maisha nje ya ustawi wa watu,hakuna amani nje ya ustawi wa watu, hakuna maendeleo pasipo haki hivyo hukumu zote zimejengwa katika misingi ya sheria na taratibu .

3.Ukifuatilia katika skendo zote za dunia utagundua kuwa kuna MTU alitanguliza tamaa, kuna MTU alikuwa mjinga ILA akajifanya mwerevu,kuna MTU alitambua madhaifu yaliyopo katika mfumo flani na kutumia upenyo huo kujinufaisha. Hivyo siku zote usijione wewe upo sahihi kuliko wengine, usimwamini yeyote,ruhusu mawazo mbadala,epuka kuwa mwamuzi wa mwisho katika kila jambo hasa yale ambayo yamekabidhiwa kwako ila huna utaalamu nayo,usipuuze chochote kinachokufikia kama kiongoz maana kila siku na kila jambo uja kwetu ili tujifunze.

4.Watawala wa kisiasa kuna wakati inatulazimu kuepuka kwa vyovyote vile kutoa maamuzi juu ya kile tulichoaminishwa ni sahihi kwa kutaka wananchi wakusifie ,bora usifanye kuliko kufanya usichokijua ukaliangamiza taifa na wewe kubaki kuumia hata baada ya kung'atuka.

5.Heshimu Hutu huku ukilinda kile kidogo ulichonacho.

6.Kumbuka Dunia tunapita hivyo kila kimoja tukionacho IPO siku utakiacha,bora kidogo cha haki kuliko kikubwa cha dhuluma.

CHANDA CHEMA UVIKWA PETE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
afadhali ya Mwinyi

bunge la tanzania ni "rubber stamp" ya serikali ya magufuli
 
Rais bora ni yule anaejua kuwa umma ndio mwajiri wake

Umma ukikosa Huduma urais wako ni vumbi tu

Boresha Huduma kwa wananchi boresha maslai ya wanaotimikia umma.

Miaka 60 ikishafika unatakiwa utoke waingie wengine sasa sound zisizo na tija sio uungwana
 
Back
Top Bottom