Yupi msanii wako bora wa hip hop Tanzania unayemkubali na kwanini huyo na si wengine??

Joh anaimba hip hop laini yaan utumii akili sana kuelewa...hao wengine mfano fid Q anaimba hip hop ngumu unatakiwa utumie akili.

Sio mtaalam wa hip hop so hayo ni maoni yangu tu mkuu.
Ok umeeleweka.
 
Chukua ulbum ya nakala za makalla yote isikilize
Kuna track kama arusha..ukiskia paa..sifagiliwi..siskii na nyinginezo.

Chunda ninamjua saana haina haja ya kunipa track zake.

Toka anaanza kuimba nawadabisha..swahili. usione hatari.nasema ninachojua ft fid namjua saana.

Unapopanga kikosi usiwaweke wachezaji wa aina moja sehemu moja. Ndicho nilichofanya mkuu. One mbishi stereo wanamziki unaoendana. Nimechukua wakali.
Hehe sawa mkuu lakini hujanijibu chunda na makalla nani mkali? Ntaku pm unipe track kali 3 za makalla
Kuhusu nikki, one na stereo wana maandishi ya style tofauti maybe hujawaskiliza vya kutosha kwahiyo si sawa kusema hao nu wachezaji wa aina1
 
Makalla ni nan au jcb kama ni huyo mtoe haraka ni mkongwe tu kwenye game nothing else, unataka kunambia makalla ni mkali kuliko prof j, songa, chunda, msodoki u must be kiddin bro

Huyo wa ukoo ni nani? Anyway ni mtazamo wako ila ningefurah kama ungenishawishi kwa punchlines
Nilivosoma hii komenti nimetamani Kulia,

Mungu akusamehe kwanza, pili tafuta ngoma za JCB afu kaa uzisikilize.. Zile za maisha ya kitaa, zile za bata, zile za mapenzi, na zile za unjanja ujanja wa kila siku.

JCB ni shule kubwa sana mdogo wangu.
 
ebwana kuna hii punch line hatari sana.....
naumiza ndonga naskonga nagonga dili nasonga unachonga
mi ndo kishindo usichohimili....

wajanja wanamjua uyo
 
Verse 1:
wachache ndo wanaishi wengi wetu ma escorts,
twiga wanapanda pipa hata bila ya passports,
mikoa mingi bado haina hata airports,
zaidi ya migodini madini kuya export,
bila ya wazawa kufaidika,
ndo mana wazanzibara wamechoka kutanga na nyika,
big up Mandela leo South sio Africa,
waliotangulia kupata uhuru bado wanapigika,
bidhaa zilizo expire kutubambika,
meli zinazidi zama wengi daily tunawazika,
wenye hali duni ndo tunao athirika,
wao ma vx yao ni special order uhakika,
tutalia machozi ya damu mpaka yata form bahari,
na tutaogelea wenyewe na watu hawajali,
leta mgomo baridi uijue serikali then muulize Ulimboka umuhimu wa Madaktari let's go
Chorus
(bado nalia tu na Tanzania yangu/kweli mali ni nyingi wale wachache wenzangu/me nalia na masikini wenzangu/eeh baba Mungu sikia kilo changu/issue is harder tuna suffer/sikia kilio changu/issue is harder tuna suffer/me nalia like..........)
Verse 2:
viongozi wa siasa kama viongozi wa dini,
mengi wanaongea coz silaha yao ni ulimi,
mh.spika Tanzania huru inazidi zeeka tayari ni miaka 50,
mengi mmetuahidi pia ahadi ni deni,
pia tunatambua umuhimu wa UN,
kupinga h.I.v,umaskini na rushwa and,
mabilioni yanayotumika kwa campgain,
kama za kupinga unyanyasaji wa watoto,
zisiishie kwenye promo na kuwalisha bado ndoto,
ishu sio kutupiana maneno bungeni,
bali watoto watoke mtaani warudi shuleni
,mkulima shambani anahitaji usafiri wa treni,
nyie piteni angani mazao yake muuzieni,
mpeni bei nzuri aweze mudu zaidi ya trector,
ni mawazo tu DIC usione nakuTATOR
(chorous)
Verse 3.
Tanu ilifanya kazi kubwa 61,
solution sio labda nchi wachukue upinzani,
bali mtanzania wa chini anaishi maisha gani,
watu wanakufa kwa njaa iweje tujivunie amani,
ni mengi tu mazuri yamefanyika mpaka sasa,
ila naamini bado tungekuwa mbali(hivi babu wa Loliondo nae inawezekana tu ilikuwa ni siasa)NO !(Lakini iko wapi hii kaburi ya Balali !?) Men ! Jibu unalo so usiulize swali,una dini ?
Mkristu sali na Muislam swali coz,
bado tunaishi ki mungu mungu,
Baada ya m weka z usikie kizungu zungu jinsi ukoloni unafanya mambo mpaka leo,
kuongoza jamii sio kumtawala mkeo,
najiuliza maisha yangekuwaje bila mziki,
hivi mtaani ingekuwa vp ? Ingekuwa mziki ...
(Chorous)
outro yeah chamber squad baby,one love,Tanzania,Muro jr I see ya ......
Till fade
 
Swali dogo tu, makalla na chunda nani mkali?
Nitajie ngoma tatu za makalla nikaskilize nami nitakupa 3 za stereo then tutafanya comparison kwa kuzingatia criteria hizi
1.iwe ya story
2.iwe kajiachia tu inayozungumzia vitu tofaut
3.collabo kali aliyowah kufanya

Nawasilisha
Ngoja tu niandike labda utapata chochote kipya.

Kwanza JCB ni moja ya ma-MC toka kundi la Hip Hop linaitwa WATENGWA, Maskani yao ni Kijenge Juu Arusha... Watengwa ya kina JCB, CHINDO MAN, CHABA, YUZZO, DONNIE, D-WIDA n.k ni kundi bora la Hip Hop kwangu Mimi, kwann...

1.Aina ya Muziki wanaofanya ktk Hip Hop unakubalika 95% (Ni ile Underground/Hardcore)

2.Kila Msanii ndani ya kundi Anastaili tofauti kuanzia Uandishi, Mitambao (Flow), na Midundo (Beats)

3.Kila Msanii kwenye kundi ana uwezo wa kusimama kama yeye na akatoboa mbele ya hadhira/mashabiki.

4.Muda.. Kundi hili lipo pa1 kwa muda mrefu sana, na wala hakuna vurumai wala chokochoko kama makundi mengine

5.Kundi Ambalo limeweza kuipeleka RAP ya kiswahili mbele, hasa nchini Ufaransa.

Tuje Kwa JCB... HAHAHAHAH, Mtengwa huyu anafahamika kwa jina la JACOB MAKALLA, nnyumbani kabisa ni Kijenge ya Juu nyuma ya Metropoo.

JCB ni brother flani kwenye hii gemu, ameanzia mbali sana... Toka enzi za Hardcore Unit akiwa pa1 na Spac Dawg na Lord Eyez.. (KAMA UMESIKILIZA ARUSHA CYPHER... Kuna sehemu JCB anachana hivi... SIONGELEI 96, AU 95 NAONGELEA 94.. Miaka ya 94 Jacob alikua ashaanza hizi harakati)

Kimuziki hapa Bongo huwezi taja Ma-MC 10 kisha usilitaje jina la JCB, (Kuwa makini, sizungumzii Marapa kama Harmorapa, au wana hip hop mguu nje mguu ndani kama ney wa mitego, madee, n.k)... Huyu Jacob ni MC, anatembea na misingi ya Hip Hop Kichwani.

Uandishi... Uandishi wa JCB ni wakipekee sanaaaaa, hafanani na wala hafananishwi.. Ukiangalia vzr uandishi wa JCB ni ule wa moja kwa moja Ila kwa kutumia Lugha ya Mtaani sana, JCB anaweza andika mstari ambao uko nusu na ili ueleweke ni lazima pia usubiri ukomo wa msitari wa pili (kina kinachofuata)

2.Mitambao... Nianze kwa kukuuliza swali, umewahi kumsikiliza JCB... je, Flow yake inafanana na nani hapa Bongo... HAKUNA, ila kwa mbele... Kwa mbali sana tena sana JCB anafanana na B.I.G NOTORIOUS.. Mimi napenda sana kusikiliza ngoma zake kwasababu ya ile Flow yake.

3.Ujumbe wa nyimbo... JCB sio MC wa siasa (Political Mc/Rapper) kama R.O.M.A au Kala Jeremiah, JCB sio rapper/Mc wa mapenzi kama Godzilla, Pia JCB sio Rapper/MC asiye na kitu kikuu cha kukiongelea/kudeliver kwa watu kwa manufaa ya jamii kama Dogo Janja, Ney, Madee, Weusi, n.k... JCB Anaandika kuhusu Maisha Ya mtaani... Ambako ndio chimbuko la Hip Hop,,, hebu soma mistari kadhaa ya JCB hapa chini toka ktk ngoma mbalimbali.

"Kitaa tunaishi na nyangumi, so dagaa inabidi niishi kihuni/Mara huyo ughaibuni/minya mpaka December/nilipopata dili haramu kwa mpemba.."

"Usipoangalia utaendelea kununua ma-jeans na kuyavaa coco beach/wakati wenzio tunawaza Paris"

Kesho nikiweza nitakuwekea mistari ambayo itakubadilisha kwa sehemu kubwa.

JCB ameshstoa Album Kali sana, ukiwa unasikiliza kama ni MTU wa hip hop huwezi kupeleka nyimbo mbele, zaidi ya kurudisha nyuma.. Fikiria Umetoka kusikiliza "SHIKILIA" au "Nimefurahishwa" au "Nakalla" au "KIJITI".

Tafuta ngoma hizo hapo Juu..
b5-click
 
Fid Q ndo msanii Bora wa hip hop kwangu...! Anaimbaa conscious sanaa na mistari yakee mpaka unajiuliza huyu jamaa aliwezaje kufikiria jambo kama hilii... Fid Q much respect...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom