Yupi msanii wako bora wa hip hop Tanzania unayemkubali na kwanini huyo na si wengine??

Sema kabadilika saana
Kwa kiasi flani kabadilika ila Yeye anajiita Baba lao la style Tofauti,hata Songa naye.

Mwanangu Nash Mc a.k.a Maalim,Nash dagama,Nash Zuzu,Nash Misimamo Kuna ngoma yake anasema Solo na pesa vinawatesa ndio maana wasanii wengi wanachekesha-Soko na Pesa.
 
hip pop ni kuongea ukweli...

nay wa mitego ndio best hip pop artist in tz
Mkuu,
Ney wa mitego anaimba vitu vilivyo Uch* sana.

Katika orodha ya kumi bora hip hop hawezi hata kufikiliwa na watu wa hip hop.
Anyway Watu hatufanani kama alama za vidole.
 
Nilivosoma hii komenti nimetamani Kulia,

Mungu akusamehe kwanza, pili tafuta ngoma za JCB afu kaa uzisikilize.. Zile za maisha ya kitaa, zile za bata, zile za mapenzi, na zile za unjanja ujanja wa kila siku.

JCB ni shule kubwa sana mdogo wangu.
Haha labda utamani kulia kwakua umekutana na ukweli na ukweli ni mchungu.
Jcb makalla nimemsikiliza kwenye ngoma kama tatu hivi na imetosha kuniambia uwezo wake maybe nahitaji kumsikiliza tena ila hata kwenye top20yangu siwezi mueka ila simaanishi kua si mwanaharakati maana tusije tukaelewana vibaya hapa,
Jamaa na nakubalia sana harakati zake na mchango wake kwenye game ya hiphop bongo
 
Kama Leo naforce budget ya usiku wa kesho before the night force kuifanya siku special usiku UK a pita kwa vita dhid ya usingiz na vita visivyo isha na tishw na jinamiz...nick mbish so wanchii
 
Ngoja tu niandike labda utapata chochote kipya.

Kwanza JCB ni moja ya ma-MC toka kundi la Hip Hop linaitwa WATENGWA, Maskani yao ni Kijenge Juu Arusha... Watengwa ya kina JCB, CHINDO MAN, CHABA, YUZZO, DONNIE, D-WIDA n.k ni kundi bora la Hip Hop kwangu Mimi, kwann...

1.Aina ya Muziki wanaofanya ktk Hip Hop unakubalika 95% (Ni ile Underground/Hardcore)

2.Kila Msanii ndani ya kundi Anastaili tofauti kuanzia Uandishi, Mitambao (Flow), na Midundo (Beats)

3.Kila Msanii kwenye kundi ana uwezo wa kusimama kama yeye na akatoboa mbele ya hadhira/mashabiki.

4.Muda.. Kundi hili lipo pa1 kwa muda mrefu sana, na wala hakuna vurumai wala chokochoko kama makundi mengine

5.Kundi Ambalo limeweza kuipeleka RAP ya kiswahili mbele, hasa nchini Ufaransa.

Tuje Kwa JCB... HAHAHAHAH, Mtengwa huyu anafahamika kwa jina la JACOB MAKALLA, nnyumbani kabisa ni Kijenge ya Juu nyuma ya Metropoo.

JCB ni brother flani kwenye hii gemu, ameanzia mbali sana... Toka enzi za Hardcore Unit akiwa pa1 na Spac Dawg na Lord Eyez.. (KAMA UMESIKILIZA ARUSHA CYPHER... Kuna sehemu JCB anachana hivi... SIONGELEI 96, AU 95 NAONGELEA 94.. Miaka ya 94 Jacob alikua ashaanza hizi harakati)

Kimuziki hapa Bongo huwezi taja Ma-MC 10 kisha usilitaje jina la JCB, (Kuwa makini, sizungumzii Marapa kama Harmorapa, au wana hip hop mguu nje mguu ndani kama ney wa mitego, madee, n.k)... Huyu Jacob ni MC, anatembea na misingi ya Hip Hop Kichwani.

Uandishi... Uandishi wa JCB ni wakipekee sanaaaaa, hafanani na wala hafananishwi.. Ukiangalia vzr uandishi wa JCB ni ule wa moja kwa moja Ila kwa kutumia Lugha ya Mtaani sana, JCB anaweza andika mstari ambao uko nusu na ili ueleweke ni lazima pia usubiri ukomo wa msitari wa pili (kina kinachofuata)

2.Mitambao... Nianze kwa kukuuliza swali, umewahi kumsikiliza JCB... je, Flow yake inafanana na nani hapa Bongo... HAKUNA, ila kwa mbele... Kwa mbali sana tena sana JCB anafanana na B.I.G NOTORIOUS.. Mimi napenda sana kusikiliza ngoma zake kwasababu ya ile Flow yake.

3.Ujumbe wa nyimbo... JCB sio MC wa siasa (Political Mc/Rapper) kama R.O.M.A au Kala Jeremiah, JCB sio rapper/Mc wa mapenzi kama Godzilla, Pia JCB sio Rapper/MC asiye na kitu kikuu cha kukiongelea/kudeliver kwa watu kwa manufaa ya jamii kama Dogo Janja, Ney, Madee, Weusi, n.k... JCB Anaandika kuhusu Maisha Ya mtaani... Ambako ndio chimbuko la Hip Hop,,, hebu soma mistari kadhaa ya JCB hapa chini toka ktk ngoma mbalimbali.

"Kitaa tunaishi na nyangumi, so dagaa inabidi niishi kihuni/Mara huyo ughaibuni/minya mpaka December/nilipopata dili haramu kwa mpemba.."

"Usipoangalia utaendelea kununua ma-jeans na kuyavaa coco beach/wakati wenzio tunawaza Paris"

Kesho nikiweza nitakuwekea mistari ambayo itakubadilisha kwa sehemu kubwa.

JCB ameshstoa Album Kali sana, ukiwa unasikiliza kama ni MTU wa hip hop huwezi kupeleka nyimbo mbele, zaidi ya kurudisha nyuma.. Fikiria Umetoka kusikiliza "SHIKILIA" au "Nimefurahishwa" au "Nakalla" au "KIJITI".

Tafuta ngoma hizo hapo Juu..
b5-click
Umeandika mengi sana kaka mkubwa ila kwa kifupi ni hivi jamaa ni mwanaharakati kweli na mkongwe kwenye hiphop ila uwezo wake wa uwasilishaji si mkubwa kwa kiasi unachozungumza wewe
Hem nitajie ngoma tatu kali za makalla ulizoziskiliza nami nikamtegee sikio labda ntaona hicho unachokiona wewe
 
"Leo nitam'Baka Mama yako ili ujifunze kutunza siri"

Huwa nikifika hapo wakati nasikiliza nacheka sana,
Aisee zohan, nzwangedaba,voice of the voiceless au Majina kibao yupo vyema mno anatisha.
Hahahaha Zohan hua na mistari ya kukufanya ucheke ila hapohapo unapata funzo, uwasilishaji wa hivi wanao wachache sana
 

Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom