YUNO kitongoji kilichopotea na kutia watu hasara kutokana na uzembe wa viongozi

karv

JF-Expert Member
Dec 26, 2019
1,799
3,221
Habari wanajukwaa leo napenda kuwapa habari kuhusu kitongoji cha YUNO ambacho kimepotea hakipo tena kimepoteaje twende sambamba hapo.

Kitongoji cha YUNO kipo katika kijiji cha Sinyaulime kata ya Ngerengere tarafa ya Ngerengere wilaya ya Morogoro vijijini mkoa wa Morogoro.

Kitongoji hiki kimepakana na stesheni ya treni ya Ngerengere upande wa kusini , Mto Ngerengere upande wa mashariki na kusini na mto Wazi upande wa magharibi.

Mwaka 2017 ni mwaka ambao hautasahaulika kwa wakazi wa kitongoji hicho kilichokuwa chini ya Mwenyekiti mzee KIDULI ambapo shirika la reli Tanzania (TRC) lilivunja nyumba zote na sasa eneo hilo limekuwa pori huku baadhi ya wakazi waliosalimika wakisubiri amri ya kuwaondoa watu waishio mita 60 kutoka kwenye mto itekelezwe.

ILIKUWAJE KIJIJI KISAJILIWE NA TAMISEMI HALAFU KIVUNJWE?

Twende pamoja sasa kwa ambao mnaifahamu ile karakana ya reli iliyopo kichangani Morogoro basi ile karakana ilitakiwa kujengwa kilipokuwa hiko kijiji lakini kwa kuwa mto Ngerengere unaenda kuungana na mto Ruvu ambao ndio chanzo kikuu cha maji kwa wakazi wa Dar basi ikabidi waahirishe na kwenda kujengwa Morogoro. Hii ndio sababu iliyowaponza.

Kwa kuwa eneo lile lilikuwa pori basi baadhi ya wazee kwa wakati huo wakaomba kwenye mamlaka husika na kwenda kuanzisha kijiji katika eneo hilo. Asilimia kubwa ya wakazi wa wakazi wa huko walikuwa ni wakulima wa mbogamboga

Basi hatimae kijiji kikasajiliwa na mamlaka husika na wakawa na viongozi kabisa pamoja na hayo mke wa Rais mstaafu Mama Salma Kikwete alienda hadi kuzindua kikundi cha akina mama waliokuwa wanalima mbogamboga na mikopo juu wakapewa (enzi hizo mumewe akiwa madarakani).

Huduma za kijamii kama umeme maji na shule zikajengwa uone serikali walivyo wajanja shule ya msingi haikujengwa katika eneo hilo licha ya kuwa lilikuwa na wakazi wengi.
Baa zikajengwa mashine za kukoboa na kusaga na mambo mengine kedekede yakawepo.

WASTAAFU WAKAANZA KUWEKEZA HUKO

Wastaafu kama kawaida wakaanza kujenga mabaa maduka saloon za kike na za kiume nyumba za kulala wageni nyumba za kupangisha mashamba na viwanja si unajua tena mambo ya mafao.
Mstaafu mmoja wa shirika la reli akahamisha hadi kibao kilichokuwa baada ni mpaka wa shirika la reli Tanzania.

UJENZI WA SGR WAWAPONZA

Hapo awali reli ya SGR walipanga ipite katika hiko kijiji sasa ili kuepuka fidia ilibidi wakazi hao watolewe ili fidia isilipwe ndipo harakati za kuwaondoa zikaanza maana hilo eneo ni mali ya shirika la reli Tanzania.

WAPIMAJI WAKINZANA
Hapo awali walipima mita 50 kwa kila upande wa reli na wakazi wake wakapewa waraka wa kuwataka wahame.
Baada ya siku kadhaa WAPIMAJI wakaja na kuongeza mita 30 kutoka zile za awali zikawa mita 80 waraka wa kuhama ukatolewa.
Lakini cha kushangaza WAPIMAJI walienda mbali zaidi hadi kutoa waraka wa kubomolewa hadi kwa watu wasiohusika.
Mwisho wa siku TRC wakaazimia kuchukua eneo lao lote na kuwataka wakazi wa hapo wahame.

WANANCHI WATINGA MAHAKAMANI LAKINI WAPI
Pamoja na kwenda mahakama ya mwanzo Ngerengere lakini haikusaidia.

UBISHI WAWAPONZA
Pamoja na kupewa waraka wa kuhama mapema wapo waliokaidi ambao mwishowe hawakuambulia hata tofari siku ya kubomoa.

BAADHI YA WATU WAPONZWA NA RELI YA ZIADA
Kulikuwa na reli kwa ajili ya mabehewa mabovu ambayo pia ilisababisha baadhi ya nyumba kubomolewa baada ya kupima zile mita 80 lakini eneo hilo halikuwa kwenye mipaka ya eneo lililotengwa kwa ajili ya karakana.

Swali la kujiuliza Je? TAMISEMI hawakuwasiliana na Wizara ya Ardhi kujua mmiliki sahihi wa eneo hilo kabla ya kusajili kijiji.

Ndio maana sishangai kwa kinachotokea Ngorongoro maana wamezoea hao
 
Kama wakzi hao wangepeleka malalamiko yao UNO wangesikilizwa.
 
Narudia tena. Wananchi wanapokuwa kama makondoo serikali na viongozi wake wanajisikia kufanya chochote watakacho.
 
Back
Top Bottom