Yumkini Kikwete ndiye mwenye kukihofia CCJ - Read This | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yumkini Kikwete ndiye mwenye kukihofia CCJ - Read This

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, May 27, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  May 27, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  JE, yawezekana Rais Jakaya Kikwete ndiye anakihofia Chama cha Jamii (CCJ) ambacho kina usajili wa muda tu, na kutokana na maagizo yake kitanyimwa usajili wa kudumu ili kisiweze kushiriki Uchaguzi Mkuu huu wa Oktoba, 2010?
  Kwa kweli jibu la swali hilo inategemea nani unamuuliza. Kuna dalili, hata hivyo, kuwa baadhi ya watu wanaamini kabisa kuwa kizuizi cha usajili wa kudumu wa CCJ kilichowekwa pasipo utata kinatokana na Rais Kikwete mwenyewe.
  Wengine wanadokeza uthibitisho wa hoja hii pale ambapo mtu pekee mwenyewe uwezo wa kutoa usajili alizungumza na waandishi wiki iliyopita akiwa amesindikizwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu (wenyewe wanasema ya “Rais”) Bw. Salva Rweyemamu.
  Katika mkutano ule, Bw. John Tendwa alisema kuwa hana bajeti (fedha) ya kufanya uhakiki; kwani anashughuli za kutoa semina. Mkurugenzi wa Ikulu hakusahihisha kauli hiyo au kuonyesha kuwa Ikulu ilikuwa na msimamo tofauti, na hivyo kutafsirika kuwa Ikulu inakubaliana au kuunga mkono maelezo hayo ya Msajili wa Vyama vya Siasa – ambaye tunaweza kumuita Mwendesha Semina Mkuu za Kisiasa; maana hana fedha za kufanya usajili!
  Kama hilo ni kweli (na hadi hivi sasa sina sababu ya kuamini kuwa siyo), basi, ni lazima tujiulize kuwa yawezekana kweli ni Kikwete ndiye mwenye kuihofia CCJ kiasi cha kusababisha kisipewe usajili wa kudumu hata kama kimetimiza masharti yote? Bado swali linanifanya nidadisi kuwa yawezekana wenye hoja hiyo wana ukweli.
  Vinginevyo tunaweza vipi kuelezea hatua zifuatazo kuhusu CCJ?
  Kwa nini CCM imetumia maneno makali ya kuikana CCJ na kuweka taarifa kwenye mtandao wake kitu ambacho haijafanya kwa vyama vingine vilivyowahi kutaka kuanzishwa?
  Kwa nini viongozi kadhaa wa CCM wamejitokeza kuikana CCJ mapema kabisa na kuibeza wakati kuna vyama vyenye usajili wa kudumu ambavyo inaonekana hawajali uwepo wao? Unakumbuka waliyosema Makamba na Mkuchika?
  Kwa nini Msajili wa Vyama vya Siasa alikana uwepo wa CCJ japo baadaye ndiye aliyewapa usajili wa muda?
  Maswali hayo na mengine yanatufanya tujiulize ni nani hasa katika CCM anayetishwa na ujio wa CCJ? Naomba nitoe pendekezo. Siamini kama Rais Kikwete anatishwa na CCJ, na hasa kama Rais wa Muungano.
  Kama utafiti wa REDET ni wa kuaminika, Rais Kikwete bado anatarajiwa kushinda nafasi yake (hasa kama CCJ haitasimamisha mgombea wa uhakika). Kama hili ni kweli, basi, Kikwete haogopi vyama vingine vyote vya upinzani; kwani vingine vilishatangaza kumkubali vikidai “anaangushwa na wasaidizi wake” ambao bila ya shaka atarudi nao ili waendelee kumuangusha!
  Tatizo, hata hivyo, naamini liko kwa Kikwete kama kiongozi wa CCM. Kama kuna kitu ambacho CCJ kinamtishia Kikwete ni kuhusu hatima ya CCM. Kwa miaka hii michache kuna kitu kimoja ambacho kinadokezwa na vyanzo vya kuaminika kuwa Kikwete hataki kuona CCM inameguka chini yake.
  Kama vile asivyotaka kuona Muungano wa Tanzania unavunjika yeye akiwa Rais vile vile hataki kuona CCM aliyorithishwa kuiongoza inameguka yeye akiwa Mwenyekiti wake.
  Hivi sasa siyo CHADEMA, CUF, TLP wala NCCR vinavyotishia umoja wa CCM. Vyama hivi vyote vimeshazoeleka na wananchi, na hata wana CCM hivyo havitishii moja kwa moja uwepo wa CCM. Na ni wazi wana CCM waliopo sasa hivi ndani ya CCM ni wachache ambao wanaweza kujiona kujiunga na vyama hivi hasa wale walio katika nafasi za juu za uongozi.
  Sasa, kukosekana kwa chama kingine cha kisiasa ambacho kina sera na misingi ambayo imejengwa kutoka katika historia yetu na matamanio yetu (kama CCM kabla haijakimbia misingi hiyo) kunawafanya waamue kubakia ndani ya CCM kwa kisingizio cha “zimwi likujualo”.
  Lakini kama CCJ itapata usajili wa kudumu na kuweza kujipanga kushiriki uchaguzi mkuu, kuna uwezekano mkubwa kwa kundi la wana CCM kutoka ndani ya chama hicho na kuanzisha chama ambacho kiko karibu na fikra na itikadi zao. Hili, Kikwete hayuko tayari kuliona linatokea.
  Kwa maneno mengine, uwepo wa CCJ ni ushawishi wa kuivunja CCM chini ya Kikwete.
  Lakini kuna sababu nyingine kwa nini Kikwete asingeweza kuona CCJ inapewa usajili wa kudumu sasa. Mtu mmoja amenidokeza kuwa aidha CCJ kitapewa usajili mwaka huu, lakini baada ya muda wa kuweza kushiriki uchaguzi kupita.
  Kwa mfano, kikipata usajili mapema mwezi Juni CCJ kitaweza kushiriki uchaguzi; kwani nina uhakika wa asilimia 100 kitaweza kujipanga kusimamisha wagombea hadi ngazi ya juu kabisa (urais). Lakini kwa sababu tunaishi katika zama za mazingaombwe na viinimacho usajili wa kudumu unaweza kuja baada ya muda kupita na hivyo kufanya usajili huo usiwe na maana kwa uchaguzi huu muhimu zaidi.
  Tatizo kubwa hapa ni kuwa endapo CCJ kitapata usajili mapema na kuweza kupanga safu yake ya uongozi, na hatimaye kuwa na mgombea wa kueleweka anayependwa na Watanzania, mwenye maono na rekodi inayokubalika, basi, Kikwete atakuwa na kazi ya kushindana naye.
  Na hii itakuwa na ukweli kama itatokea mtu apendekeze ufanyike mdahalo wa wagombea urais. Sote tunajua kuwa Rais Kikwete hana kipaji cha ujenzi mzuri wa hoja au ushawishi na atakuwa na kubabaika endapo atashindanishwa na mtu mwenye uwezo wa kuvuta hoja.
  Kwa mantiki hiyo, Kikwete yuko radhi kupambana na kina Lipumba, Mrema na Mtikila; lakini atakuwa na kazi sana kama itambidi amkwepe mtu ambaye ana heshima kwa hoja, uongozi, na maono ya taifa.
  Sasa hili ni muhimu kuelewa. Si kwamba Kikwete hatochaguliwa hata akipambanishwa na mtu huyo; bali tatizo ni kuwa atapoteza wabunge wengi. Hili nalo tunaweza kuliona kama tutaamini utafiti wa REDET.
  Kwa vile wananchi tayari wameonyesha kuchoshwa na baadhi ya wabunge wa CCM, ikitokea CCJ ikaja na namba mpya kabisa ya wabunge wenye misimamo mikali, siyo ya mrengo wa kati kama wa vyama vilivyopo vya upinzani, wananchi wa Tanzania wataamua kwenda na mrengo wa kulia na siyo mrengo wa kati.
  Matokeo yake CCJ inaweza kabisa kupata wabunge wengi zaidi kuliko chama kingine chochote na kujikuta kinakuwa chama hasa cha upinzani. Hili linaweza kufanya Kikwete ashindwe kutawala apendavyo; hasa kama wingi wa wabunge wa CCM (wanaozidi theluthi mbili) utaondolewa aidha na CCJ peke yake au na upinzani kwa ujumla wake.
  Sasa hilo ndilo tishio kwa Kikwete linalotokana na CCJ. Kwamba, ama CCM itavunjika mikononi mwake endapo CCJ itapewa usajili wa kudumu kabla ya muda wa kushiriki uchaguzi kupita au CCM itapoteza wabunge wengi kwenye uchaguzi mkuu endapo CCJ itasimamisha wagombea wake.
  Katika yote mawili, Kikwete atakuwa na kazi ngumu zaidi ya kutawala katika CCM na nchi iliyogawanyika kiitikadi kuliko ilivyo sasa ambapo anaongoza taifa lililogawanyika kimaslahi. Maslahi ni rahisi sana kuyatuliza lakini tofauti za kiitikadi ni ngumu mno kuzituliza.
  Sasa kwa vile tunakubaliana (kama hukubaliani na mimi itabidi uanze kusoma tena makala hii) kuwa CCJ ni tishio zaidi kwa Kikwete kuliko inavyofikiriwa, basi, hatuna budi kuamua tuchukue msimamo upi.
  Kama tunataka CCJ inyimwe usajili wa kudumu ili isiigawanye CCM na kufanya kazi ya Kikwete kutawala kuwa ngumu, basi, tunatakiwa tumshukuru Kikwete, Marmo na Tendwa kwa msimamo wao wa kuiokoa CCM.
  Kama, hata hivyo, tunaamini demokrasia inatuita kutetea chama hiki ambacho hakina watetezi; kwamba tunaamini waamuzi wa mwisho wa chama cha siasa siyo ofisi ya msajili au Ikulu; kama tunaamini Watanzania bado wana uwezo wa kuamua wenyewe nani awaongoze na siyo kuamuliwa, basi, hatuna budi kumtaka msajili wa vyama vya siasa kufanya kile alichoapishwa kufanya; yaani kuwa msajili wa vyama vya siasa.
  Tumtake msajili kukitendea chama hicho haki na kukipatia usajili wa kudumu ili Watanzania ambao wanataka kujaribu bahati yao na chama hicho wafanye hivyo pasipo kulazimishwa na watu wengine kujiunga au kuunga mkono vyama ambavyo hawakubaliani navyo au hawako tayari kukubaliana navyo kwa sasa.
  Kama unaamini katika hili: Unaweza kumtumia ujumbe wa sms Msajili wa Vyama vya Siasa Bw. John Tendwa kwa kumwambia “Tunakusihi ukipatie usajili wa kudumu CCJ ili kiweze kushiriki uchaguzi mkuu na wananchi waamue kukikubali au kukikataa.” Tuma kwenda namba 754 304772 au kwenda email:
  Labda baada ya kusikia sauti ya watu watawala wetu wanaweza kuona kuwa ni wananchi ndio wenye uamuzi wa mwisho.
  Vinginevyo, woga wao utathibitishwa na uamuzi wao na hivyo yawezekana wanajiepushia aibu kwa kukinyima usajili wa kudumu mapema. Je nimejibu swali au swali letu bado lipo: Je yumkini Kikwete ndiye anayehofia CCJ kupewa usajili wa kudumu ili kiweze kushiriki uchaguzi mkuu?
  [​IMG]

   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Huwa namshangaa sana tendwa anavyo ongea utafikiri kapewa na uwezo wa kuondoa uhai wa mtu. Kwa kifupi CCJ kunyimwa usajili wa kudumu kwa maneno ya kejeli ya tendwa nadhani Kikwete ana mkono wake pale, na sishangai sana kwa sababu CCM ni wale wale na tendwa ni CCM.
   
 3. M

  Magezi JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Lakini mzee mwanakijiji kitu ambacho mimi huwa najiuliza na sipati majibu ni je, kweli vyama vya upinzani Tanzania vimeshindwa kupigania tume huru ya uchaguzi inayoshirikisha vyama vyote?? Au wameridhika na hali??
   
 4. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #4
  May 27, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  .

  kwasababu ya mazingaobwe hayo, ndio maana siajabu Msajili wa vyama anakadi ya uanachama ya CCM, NA AHADI YA KUWA MWAMINIFU KWA CHAMA ALIAPA.
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Walianza kuzungusha swala la mgombea binafsi, likaja la CCJ nalo wanalipiga dana dana.
  Ipo siku watanzania wataamka na kusema 'enough is enough'.
  Soon and very soon demokrasia ya kweli itatawala nchini na wale wote wanaojifanya nchi hii ni ya kwao peke yao watalia kilio cha kusaga meno.
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Katika mfumo wowote wa uongozi, watawaliwa wakinyonwa sana wao wenyewe watanyanyuka na kutaka haki zao, hizo siku haziko mbali kwa bongo yetu!
   
 7. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,435
  Likes Received: 1,016
  Trophy Points: 280
  Naona mzee mwanakijiji unampa Kikwete sifa za bure, ambazo hazipo labda kama kuchangamsha baraza. CCJ ni chama kipya na bado kinacho kazi za kufanya sasa kabla ya kuelekea 2010 election. Kama vyama vingine wanatakiwa kutimiza wajibu wao katika kuandaa mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizombeleyao la usajili likiwa mojawapo. Kuanza kujenga hisia na kulalamika watakuwa hawana jipya ukilinganisha na vyama vilivyopo, chama lazima kipitie katika real life, high expectation za waanzilishi na makala zisizokwisha za waandishi hazipaswi kutuondoa katika mstari manake ndio utaratibu wenyewe.

  CCJ lazima watambue siasa za upinzani katika Afrika si lele mama, ni wajibu wao kujifunza kutoka Chadema, CUF, UDP, NCCR na ANC. Kutoka CCM hakutoshi kuwahakikishia ushindi au mafanikio ya haraka manake waandishi wa makala mmekuwa mkiandika toka NCCR wanaanza na kila raisi kwa wakati wake ameunganishwa na hoja hizi hafifu za MMK lakini walipata usajili hata DP kwa mbinde walipata usajili.

  CCJ kama kimeanzishwa kwa ajili ya uchaguzi 2010 basi ni msiba mwingine kwa watanzania manake the outcome can be predicted. Bora watanzania wakaelimishwa zaidi kuvipa nguvu Chadema, CUF na vilivyopo wakati CCJ ikianza kutambaa just for 2010. Binafsi naona kama recycling ya watu wale wale kutoka chama kilekile (CCJ) kibaya zaidi watu hao hawakuwa cream huko walikotoka walikuwa wa kawaida sana.
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  I CAN PUT MY FEW CENTS KWAMBA THREAT YA KIKWETE NI KATIBA MPYA NA SI CCJ... Ile kuplay dead na delaying tactics has made a good number of CCJ hopeful kuanza kutafuta mabanda kujikinga mvua

  all the best
   
Loading...