Yule shabiki wenu aliyemkumbatia Kaka - yataka moyo!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yule shabiki wenu aliyemkumbatia Kaka - yataka moyo!.

Discussion in 'Jamii Photos' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 8, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 8, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ukiondoa mambo yote ambayo yalitokea kwenye mechi ya Brazil Vs Tanzania kilichosisimua ni kisa cha shabiki mmoja kukatiza uwanjani na kwenda moja kwa moja kwa Kaka na kumkumbatia. Ni wazi jamaa alikuwa amedhamiria kufanya hivyo, alipiga mahesabu na kutekeleza kwa kiasi kikubwa.

  Ni wazi kulikuwa na kuvunjika kwa usalama kiasi ambacho kinatia aibu.. lakini wakati mwingine ndio burudani ya soka..

  Angalia mwenyewe..

  [​IMG]
  Vitu vingine kuvifanya inahitaji ujasiri wa kipekee. Kitendo alichokifanya shabiki huyu cha kuingia uwanjani kwa lengo la kwenda kumkumbatia mchezaji maarufu wa Brazili Kaka, kilikuwa ni cha kipekee, japo hakuwa na nia mbaya, lakini alihitaji ujasiri. Kamera yetu ilinasa tukio zima hatua kwa hatua...jamaa aliingia uwanjani huku akiita KAKA, KAKA, akiwa mikono juu kuashiria kuwa hana silaha yoyote, ...na hii ni hatua kwa hatua ya tukio zima....

  [​IMG]

  ..kafanikiwa kumfikia kaka na kumkumbatia

  [​IMG]

  ..bila hiyana kaka naye akampokea na kisha kum pet mgongoni...

  [​IMG]
  ...na kisha kuondoka naye hatua chache huku amemkumbatia kishkaji

  [​IMG]

  ...kisha anamuaga,,,jamaa anaondoka kwa furaha

  [​IMG]
  ...haya kwaheri mshikajii

  [​IMG]
  ....kaka kakaa kakaaa!!!!!!!​

  PICHA: Saleh Ally
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Jun 8, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Lol...yeah hii ilikuwa burudani kwa kweli.

  Ila hii chamtoto. Kuna wale ambao huvua nguo zao na kukatiza katikati ya uwanja uchi...halafu wanaanza kukimbizwa na watu wa usalama....

  Michezo hii hutoaga burudani kwa kweli. Hata kama ulikuwa una siku mbaya ghafla siku yako inaweza kubadilika hivi hivi kutokana na kicheko utakachoangua kwa kuona vituko kama hivi.
   
 3. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Jamaa hakika alikuwa kwenye ecstasy ya raha. Unaweza kuona.
   
 4. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Chakusikitisha ni kwanini hawa wanausalama wa Kibongo huwa wanajichukulia Sheria Mikononi? Ni sawa jamaa alivunja sheria lakini haikuwa kazi ya Polisi kumwadhibu (Kumpa hukumu kwenye kadamnasi) tena baada ya kumkamata.

  Kama jamaa walishindwa kumzuia asiingie uwanjani inaonekana walikuwa wajinga wakitizama mpira badala ya kulinda usalama. Baada ya Mshikaji kuibukia uwanjani wanamfamia na kupiga utadhani hatachukuliwa tena hatua za kisheria. This is very shame for security system. Inaonekana wanaingia bure uwanjani pasipo hata kutekeleza huo ulinzi. Kama wanazuia wananchi wasipige waharifu (Vibaka), kwa nini wao walimshuhulikia jamaa mbele ya wakuu wa nchi>

  Bongo yetu hii tabu tupu..
   
 5. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2010
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hakika ni aibu kubwa kumpiga mbele ya mkuu wa nchi! Na mbele ya vyombo vya habari vya kimataifa. Ni utovu wa nidhamu wa hali ya juu. Inaonesha ni kiasi gani nchi yetu haina utawala wa sheria. Ni maguvu tu.
   
 6. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ha ha haaaa

  Ilimkuta hata Gaucho hii

  Ronaldinho more tolerant of loving pitch invaders than security team - Dirty Tackle - World Soccer

  [​IMG]

  AC Milan played the Chicago Fire on Sunday as part of its unmotivated U.S. tour, and during the match, an unstable fan decided to run onto the pitch and express his unsettling degree of affection for Ronaldinho.

  To his credit - or perhaps complete disregard for his own personal safety - he let the fan kiss him on the cheek and even exchanged a few friendly gestures with the man.

  The security team at Chicago's Toyota Park, however, wasn't quite as kind to the invader as Ronaldinho. Although it first appeared that the initial security man on the scene was just getting his own taste of the passion on the pitch, he eventually dragged his detainee away from the footballer. When it finally seemed like he had the situation under control, a second security guard came bounding in to take down the easy target himself. The draw of pouncing on top of someone (or, at least, try to do something similar to that) was just too hard to resist, I suppose.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  polisi wanafundishwa ni wapi wanapaswa kutumia nguvu, lakini pia nguvu wanayotakiwa kuitumia lazima iendae na uzito wa tukio. Huwezi kumpiga mtu rungu au kopi wakati hata hana kijiti cha kuchokonoli meno mkononi labda angekudhuru au kudhuru wengine. Hata hao polisi wa kutuliza ghasi, huwa hawatakiwi kuruka na marungu juu ya miili ya watu hata kama wanaleta fujo mpaka pale hizo fujo zitakapo onekana zinaweza kusabaisha uvunjifu wa amani na utulivu ambao itakuwa ni ngumu kuthibiti.

  Mtu kama yule ambaye ameingia na kutoka uwanjani akishangilia hata kama katenda kosa ilipaswa kumkamata na kumpeleka kwenye mapumziko ya kipolisi (tena polisi mmoja tu) angetosha na sio kumrukia kwa nguvu utadhani ninyi wenyewe mlitimiza wajibu wenu vizuri. Kumbe wametulia wanachek game bila kiingiliao.

  Ikiwa jamaa watamfungulia mashtaka, ni wazi kabisa polisi waliohusika kulinda usalama pale taifa wanapaswa nao walambishwe machungu kidoo kadiri ya uzembe wao wa kuacha mpaka mshabiki anaruka uwanjani. Je, kama jamaa angekuwa na silaha, si angeweza kufanya lolote pale?.

  Ifikie wakati ambapo Polisi wetu wawe kama wa mataifa mengine kuwa wasiwe wanaangalia kiwanjani bali wageukle kutazama mashabiki ili twende sawa kuliko haya wanayofanyiwa ya kuingizwa bure kiwanjani ili walinde lakini wanakuwa bize wakitizama mechi wakati sie wananchi wengine tunalipa viingilio.
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Wakuu, its a shame kwenye security ya wachezaji... lakini every time i see the photos napata smile fulani maana jamaa anaonekana yuko very happy and no one can miss ile genuine bright face aisee!!! at least pamoja na shida na kutokua hata na viatu, jamaa forgot ufisadi, shida zetu na utapeli wa wanasiasa

  Nimependa sana Kaka alivyompokea, its really a good gesture wakuu

  Nilikua nasikiliza clouds leo jioni Kova anasema jamaa bado yuko ecstatic na hajutii kabisa kumshika kaka yaani hata huko selo yeye hakumaindi kabisaaaa... he says Kaka ni icon wake na alipagawa na jinsi alivyokua akicheza na pale alimpomshika ndio basi tena

  in short the guy is still happy pamoja na kunyanyaswa na wanausalama ingawa yuko selo
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Sikushangaa hiki kutokea kwa Kaka. Kaka, Lucio na wengine kadhaa, ni watu waamini dini wa NGUVU. Kuna wakati Kaka alikuwa akicheza na T-shirt ndani yenye maneno ya dini. Na World Cup Asia walikuwa wakishinda, basi wanasali na baada ya mechi kuisha, kwanza walitengeneza duara na wakasali na ndiyo wakaanza kushangilia.

  Kuhusu POLISI kuwapiga wananchi, nafikiri ni SABABU nyingine wanayotakiwa kuitumia CHADEMA/Upinzani kuwaambia wananchi kuwa POLISI wa CCM hao na wanapiga watu mbele ya RAIS. Hilo pia kweli siwezi shangaa maana Waziri wao yuko kwenye Good Time. Nafikiri kitendo cha jana KILIZIDI KUMTIBUA MAGUFULI.
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  sikonge!! Magufuli ameingia vipi tena hapa??
   
 11. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  eti dereva wagonga basi !! aaah sawa hiyo aaa ta hiyo si sawa dereva wacha vituko!!!!!!!
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, John Magufuli, ameiponda dhana ya polisi jamii inayotumiwa na Jeshi la Polisi katika kupambana na uhalifu kwa maelezo kwamba utaratibu huo hauwezi kusadia mapambano dhidi ya ujambazi.

  Magufuli amesema haiwezekani kuhubiri polisi jamii kwa jambazi huku wananchi wakiendelea kuumia, kupoteza maisha na mali zao kutokana na vitendo vya ujambazi.

  "Wenye kusikia wamesikia. Ningekuwa mimi huko (Mambo ya Ndani) polisi jamii ningeizungumzia kwa wananchi tu lakini kwa jambazi hakuna cha jamii, unamshughulikia kisawasawa. Nasema wasikie na msemakweli ni mpenzi wa Mungu," alisema.

  Aliongeza: "Endeleeni jamii huku watu wanaumia. Unamkuta mtu ana bomu bado una jamii, unamkuta mtu amemchoma mtu amekimbilia majini bado unang'ang'ania jamii. Unamkuta mtu ametega mawe barabarani ana mapanga amekaa bado unang'ang'ania jamii. Sitaki kuingilia wizara nyingine lakini hayo yananikera."

  Soma hapa: https://www.jamiiforums.com/habari-na-hoja-mchanganyiko/62072-magufuli-aponda-dhana-ya-polisi-jamii-dhidi-ya-majambazi.html

  POLISI wetu panapotakiwa kutumia nguvu, wanalala mbele na pasipotakiwa WANATUMIA NGUVU. Kwa maana hiyo, unadhani jana Magufuli kama aliona alifikiri nini?

   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  shauri yako, unamponza magufuli wa watu kwa JK
   
 14. M

  Malila JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kizuri zaidi,jamaa kamalizana na Kaka na wakaagana kwa amani,kisha jamaa karudi nje ya uwanja bila taabu yo yote,sasa bakora za nini? Nguvu ingetumika kama jamaa angekomalia uwanjani hataki kutoka. Bado sana,
   
 15. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Jamaa kanikosha ila hao "polish" ni wale wa enzi zilee.
  Inaonekana pamoja na MWEMA NA KOVA KUONGEA SANA NA MEDIA,BADO HAWAJA WAELIMISHA VIJANA WAO.
  Waache kuuza sura na badala yake waandae mafunzo ktk sehemu za kazi ktk kuboresha utendaji kazi wa JESHI LA POLISI
   
 16. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Bahati ya mtu huwa haipotei ila inacheleweshwa.

  La kuvunda halina ubani.

  Watabanaaaaaa mwisho wataachia.

   
 17. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #17
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  POLICE are holding Nageri Kombo (21), a student with Green Acres Secondary School who stormed into the soccer pitch and hugged Brazilian soccer maestro Ricardo Kaka, during a friendly game between Taifa Stars and Brazil at the National Stadium on Monday evening.

  The Temeke Regional Police Commander (RPC), Mr David Miseme, said today that the suspect, a resident of Sekenke in Kinondoni District, was detained at Chang'ombe Police Station in Temeke District.

  "He strayed into the football pitch after jumping over the fence and hugged a Brazil footballer named Kaka, much to the surprise of all players and spectators," said Mr Miseme.

  Information had it that Kombo had vowed to his friends and relatives that he would hug Kaka once he saw him - a promise that he fulfilled after invading the pitch unnoticed by security policemen.

  Further information had it that before dashing into the pitch, Kombo emptied his trouser pockets and handed valuables including a mobile phone and a wallet to a friend. He also handed over a pair of shoes as he was sure that he would be arrested for the foray.

  Mr Miseme said the suspect was arrested shortly after accomplishing his mission and that police were going on with investigations. During the incident, Kaka remained calm as other players looked astonished.

  Kaka's transfer fee of 60 million pound sterling from AC Milan to Real Madrid last year was the second highest after Christiano Ronaldo, who moved from Manchester United to Real Madrid at a cost of 80 million pounds. He was also the World Best Player for 2006/07.

  MTAZAMO:

  KIJANA HUYU AMEONYESHA UJASIRI WA HALI YA JUU NA KUTUDHIHIRISHIA WATANZANIA MBELE YA UONGOZI MZIMA WA NCHI KUWA TZ SUALA LA USALAMA SI KITU CHA KUKITUMAINI. AMEWEZA KUWEKA KUMBUKUMBU ZAKE SAWA ILI HALI AKIONYESHA WAZI KUWA WANA USALAMA WANAPASWA NAO WAANZE KULIPA VIINGILIO KWA KUWA HAWANA KAZI YEYOTE WAKIWA UWANJANI ZAIDI YA KUDEKU MECHI FULL TIME KAMA SIE WANANCHI. TAIFA LIMEPOTEZA MAPATO KUJAZA WANAUSALAMA WASIO NA KAZI PALE NDANI.

  KIJANA AKIFIKISHWA MAHAKAMANI, POLISI NAO HASA WALE WALIOPEWA DHAMANA YA ULINZI SIKU ILE NAO WAPEWE ANGALAU "ZAWADI"
  INAYOSTAILI KIPIMO CHA UZEMBE WAO.


  ZIDUMU FIKRA SAHIHI ZA JK KUTULETEA "WANASAMBA" KWA GHARAMA YEYOTE ILE HATA TUKILA MAJANI LAZIMA "KAKA" ATUE TZ KAMA ILIVYOKUWA KWA NDEGE YA RAIS NA RADA !!!


  http://www.youtube.com/watch?v=PD086_LTs-w&feature=fvw
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  ahaa! wamuachie tu huyo dogo, kwanza walimpiga kinyume cha Sheria. Wamuachie tu aandelee na shule zake.
   
 19. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Kova achia huyo kijana katafute majambazi na zuia uhalifu huo sio uhalifu no criminal element at all in that, au unataka publicity kuhojiwa na ESPN.
   
 20. F

  FYA PANDOMO Member

  #20
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 8, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 5
  hawa polisi hawana wanachokifahamu kuhusu ushabiki!huyu kijana hakumdhuru kaka ni ushabiki tu!mbona wanaowadandia akina fali ipupa na kofi olomide majukwaani hawawekwi ndani?
   
Loading...