Yule mdada aliyekuwa anauza Uji kwa sasa Mambo yamebadilika soon atawaajiri

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,914
Kuna siku nilileta bandiko hapa la Mdada gradute kuuza uji watu kwa kifupi povu liliwatoka na wengi unakuta wako mtaani na wengine wanaishi kwa shemeji na wengine wamejiriwa wanakula Kilo 3 na nusu kwa mwezi.

Yule Dada mjasiria Uji, alifanikiwa kuandika proposal yake ambayo pia nilidaidiana naye na akampelekea Mtu fulani mwenye pesa zake zake. Baada ya kusoma Jamaa alivutiwa sana na idea na kukubali kuingiza pesa Milioni 50.

Kwa sasa Yule mdada anafungua kabisa hoteli na bado uji atauza ila kwa njia mpya na inayo vutia zaidi.Muda wowote akipata location nzuri kazi itaanza.

Na i hope atafika mbali sana na siku 1 atakuja kuajiri wale alio piga nao kitabu ambao still hadi leo wako mtaani wengine wanaishi kwa mashemeji na wengine kwao.

UJUMBE

Mara zote MUNGU husimama na watu jasiri palipo na uoga na aibu hapo Mungu hayupo bali palipo na ujasiri basi Mungu yupo.

Tuache kukalili maisha kwamba Gradute kuuza mihogo au mchicha unajidharirisha. Huji malengo yake, hujui target yake, hujui Ameplani vipi, Bujui end point yake ni ipo so ni vizuri kukaa kimya na kuangalia maisha yako wewe.

NB: Kuna watu wana pesa ila hawana mawazo na pesa ziko tu benki, Siku moja nitaelezea story moja inayo fanana kwa kiasi fulani na hii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahaaa! Naona unatafuta sehemu ya kujifariji.....
Sio uchawi ila kwa comment yako hapo juu naweza kuelezea unaishi life style gani Mkuu.
Nimeuliza swali hiyo uji ndio imemfanya afungue hotel? Huku kitaa kuna wamama wana migahawa ni miaka lakin hawajapata hata mtaji wa kufungua hotel, hivi hotel unaijua au unasikia tu hata hiyo 50M haitoshi kwa hotel

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeuliza swali hiyo uji ndio imemfanya afungue hotel? Huku kitaa kuna wamama wana migahawa ni miaka lakin hawajapata hata mtaji wa kufungua hotel, hivi hotel unaijua au unasikia tu hata hiyo 50M haitoshi kwa hotel

Sent using Jamii Forums mobile app
Unajua tatizo linalo wakabili? Most of Wanaume na wanawake wapika vitumbua na Mihogo na Uji na wakaanga karanga wanakosa Vision si kwamba hawapati pesa. Unaweza kuwa na pesa nyingi sana ila ukawa huna Vision

Usiwa rate kwa kuangalia Uvaaji wao. Hahaaa ile ni njia yao tu ya ku ji under rate ili wandane na jamii

Kuna jamaa ni M brash viatu ana kona nzuri anayo brashia viatu. Ukifika kwake utazimia mimi sikuamini alivyo nipelela kwake na tangia hapo hawa watu huwa si wa under rate kabisa.

Usiangalie wanavyo vaa au walivyo wengi wao wana miliki hadi Daladala kwa kuchoma mihogo ika hata siku moja hutasikia wanazunguzmia Daladala zao na wengi wana mageto na wanasomesha watoto vyuo vikuu kwa kukaanga mihogo.

Mihogo tu mtoto yuko chuo kikuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa Tanzania usijidanganye kuanza kutembeza "idea" yako kwa wafadhili au "funders" utaibiwa asubuhi tu na kufukuzwa kama mbwa.

- Na hata kama wakishindwa kuitekeleza, watakuwekea ugumu mzito utakapokuja kutekeleza wazo lako.

- Na kibaya zaidi serikali imeweka gharama kubwa sana za usajili wa mawazo na trademarks huko BRELA na COSOTA jambo ambalo siyo rafiki kwa START UPS !
 
Hahaaa basi kufa nayo. Una mkataba na Mungu? Uoga hujawahi kuwa suluhisho. Wewe waza hivyo wenzako wanapiga pesa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom