Yule Mama akaniambia; umekosea kuwahi kuoa. Je, yuko sahihi?

Kwema Wakuu!

Kama mada isemavyo!
Juzi nimeenda kununua Dawa Kama mnavyojua jijini DSM kuna vihoma mshenzi vinavyoendelea.
Nilipofika Duka la Dawa nikapokelewa na Mama mmoja mtu mzima, ni Daktari. Akanikaribisha Kwa bashasha zote. Huku akinambia ananionaga na Mdada mmoja, akaniuliza ni mke wangu, nikamdanganya ndio ni mke wangu.

Akastaajabu Sana. Akaniuliza umri wangu nikamjibu, miaka 27. Akazidi kushangaa Hali iliyovuta umakini wangu kuwa ni kipi kinachomfanya ashangae kijana Kama Mimi kuoa nikiwa na umri huo.
Akaniambia nimekosea kuwahi kuoa, yeye anaamini kuwa ndoa yetu hiyo niliyomdanganya haitafika popote.

Nikamuuliza, alitaka nioe nikiwa na umri upi. Akanijibu walau 33-35 nikamuuliza Kwa nini.
Akanijibu, Kwa hoja zifuatazo;

1. Umri huo akili itakuwa imetulia na nitakuwa tayari kuitwa Baba. Yaani sitakuwa na mambo ya kitoto.

2. Umri huo kiuchumi nitakuwa vizuri, ninaouwezo wa kumhudumia mke na familia.

3. Umri nilionao ni umri wa kuwasaidia wazazi kiuchumi Kwa kurudisha Fadhila huku nikiwekeza Kama kununua kiwanja ikiwezekana kujenga kabisa kwani nikioa majukumu yatakuwa mengi.

4. Bado sijala ujana vyakutosha, hivyo nitamsumbua mke wangu, au yeye atanisumbua Kwa vile bado naye hajala ujana.

5. Anadai mke(niliyemdanganya ninaye) hatujapendana, yaani kanihakikishia sijampenda naye hajanipenda sema tumetamaniana. N.k.


Mimi nilikuwa msikivu Sana Ila mwenye maswali ya ubishi ili kumchochea aniambie facts za Msingi.

Nikamjibu hoja zake Kama ifuatavyo;

1. Mimi ninaiona akili yangu imetulia na ninaweza kuishi na Mwanamke ndio maana nimefunga ndoa.
Nikamwambia akili haina umri, wapo Vijana wadogo waliooa wakiwa na umri mdogo kabisa zaidi yangu wakiwa na miaka 22-25 na wanaimudu ndoa. Lakini wapo waliochelewa na ndoa inawasumbua.

Umri wa miaka 27 nimemwambia ni kijana anayejitosheleza kabisa kiakili labda awe alipata hitilafu utotoni au anatumia madawa ya kulevya.

2. Uchumi hasa wa kiafrika hauna Guarantee kwamba ukifika umri Fulani utapata pesa.
Nikamwambia, wapo mamilioni ya vijana wenye Elimu na wasio na elimu wanaumri wa miaka 33+ na maisha hawayaelewi.

Nikamkataza kabisa asijewaambia watoto wake upuuzi huo maana alinambia ATI mtoto wake wa Kwanza ambaye yupo Chuo atamuambia aoe akiwa na miaka kuanzia 33.
Nikamwambia dunia walioishi wao mi tofauti na Dunia ya leo.

Nikamuambia mtu anaoa pale akutanapo na mtu anayehisi wanaelewana na sio ishu ya umri.

3. Kuhusu kusaidia wazazi. Nikamwambia kusaidia wazazi hakuna umri Ila ni matokeo ya vile wao wenyewe walivyokulea na kukujenga.
Mzazi unaweza usiwe na majukumu na usimsaidie na unaweza ukawa na majukumu ukamsaidia. Hivyo ni ishu ya malezi tuu.
Pia Kama mzazi alikuwa anasaidia wazazi wake(Bibi na Babu) wakati Mtoto yupo mdogo basi nao watasaidiwa kwani mtoto hujifunza kutoka Kwa wazazi wake.

Ishu ya kusaidia wazazi ni ishu ya malezi kuhusu tabia ya Mtoto.

Nikamwambia majukumu ya ndoa ni yandoa, kumsaidia mzazi hakumaanishi ukimbie yanayokuhusu Kama kujenga familia yako. Mzazi atapokea percentage tuu na sio kila kitu kutoka Kwa mtoto. Hivyo nikamwambia ni Bora ajiwekeze kuliko kutegemea watoto wachelewe kuoa ili warudishe Fadhila.

Nikamwambia ninyi ndio wazazi mnaozuia vijana wenu wasioe ili mupate Mia mbili kutoka kwao na ninyi ndio mnagombanisha ndoa za watoto wenu.

4. Sijala ujana wa kutosha.
Nikamwambia kila mtu ananamna yake ya Kula maisha na kuyafurahia. Wapo ambao kufanya zinaa na umalaya ndio kula maisha. Wapo ambao kunywa pombe na kwenda Club ndio Kula maisha.
Wapo ambao kusafiri na kuvaa vizuri ndio Kula maisha.
Hivyo Inategemea.

Nikamwambia Kama kwake Kula maisha ni kustarehe na wanaau wanaume basi asidhani hiyo ina-apply Kwa watu wote.

Pia nikamwambia wapo watu wazima wamama wanaovunja ndoa zao umri ukiwa umeenda miaka ya 40+ hao nao tusemeje kuwa wamewahi kuolewa? Au wababa wanaochepuka na umri mkubwa nao waliwahi kuoa?

Nikamwambia, ishu ya Kula maisha inatokana na malezi na makuzi ya mtoto vile wanavyoitafsiri.

5. Kuhusu hatujapendana Ila tumetamaniana.
Nikamwambia kuachana kuna sababu nyingi. Kuhusu kupendana au kutamaniana nikamwambia hiyo huwa Siri ya mtu. Hivyo asiusemee moyo wa mtu.


Akaniambia walau nijenge nyumba ndio ningepaswa kuoa.
Nikamuuliza wao wamejenga nyumba linii akanambia mwaka 2014, nikamkadiria kuwa mwaka huo yeye alikuwa na miaka 38 na mume wake 45. Nikamuuliza ulitaka mumeo akuoe ukiwa na miaka 39 ukiwa unakaribia menopause, alafu yeye akiwa na 45?
Nikamwambia ulitaka uzae ukiwa na umri 39?

Akanijibu hapana,
Nikamwambia tena wewe na Mumeo wote mumeajiriwa miaka ya 2000 lakini mmejenga nyumba miaka 14 iliyofuata.

Sasa ninyi mlikuwa mnaingia kwenye Ajira moja Kwa moja na mmejenga nyumba baada ya miaka 15 kasoro.
Hivi huyo mtoto wako atakapomaliza Chuo aanze kudunduliza pesa ya mtaji, kisha aanze biashara, imkubali, aanze kupiga pesa unafikiri atachukua miaka mingapi?
Na Kama itachukua miaka kumi mpaka 15 na sasa anamiaka 22 unafikiri hiyo miaka 33 ataweza kuoa na kuwa na maisha uliyonitajia hapa?

Mwishowe nilimshinda Kwa hoja. Nikamwambia Kama kijana atataka kuoa amuache aoe tuu tena faida ni nyingi kuliko hasara.

Nikamwambia miaka 33 ndio apate mtoto wa Kwanza ndoani, amtunze nikamwambia asije akathubutu kumshauri mtoto ujinga huo.

Amuache mtoto afanye vile maisha yatakavyomuamulia na atakavyoona.

Mwisho kabisa nikamwambia sijaoa, Ila natamani ningekuwa nimeoa ningali kijana Mdogo nikiwa naakili timamu.
Kuliko kuoa nikiwa nakaribia kilele cha nguvu zangu kabla hazijaanza kushuka ambao ni miaka 40.

Mjadala uendelee.

Taikon wa Fasihi
Kariakoo
Kuoa chini ya miaka 33-35 ni ufala,


Sio mara zote ukishinda argument basi you are right, kuna vitu huwez kuvi-prove wrong mpaka vikutokee...ndio maana ya experience, sasa oa saivi then subiri ufike 33- 35 ndio utajua huyo mama alikua sahihi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuoa chini ya miaka 33-35 ni ufala,


Sio mara zote ukishinda argument basi you are right, kuna vitu huwez kuvi-prove wrong mpaka vikutokee...ndio maana ya experience, sasa oa saivi then subiri ufike 33- 35 ndio utajua huyo mama alikua sahihi.

Sent using Jamii Forums mobile app


Huo ni mtazamo wako Boss.

Wengine kuoa Kwa umri huo ulioutaja pia ni ufala.

Na waliooa mapema wako poah zaidi kuliko waliochelewa.

Ukichelewa kuoa basi uwe umetoboa maisha walau maisha yasikubabaishe.
Lakini kama huna hili wala lile na ukachelewa kuoa jua umekwisha. Malezi lazima yakushinde.

Hata wanawake wenyewe hawawezi kukubali kuolewa na mtu mwenye umri 35 huko alafu Hana mbele wala nyuma. Anaishi chumba kimoja na vitu vya kijana anayeanza maisha akiwa na miaka 20.

Kama maisha yako yapo poah basi oa hata ukiwa na 40 lakini kama ndio Wale kipato hakifika hata 500k Kwa mwezi usithubutu
 
Mama yuko sahihi, maana ndoa zina mikiki mingi, na wengi walioa kwenye ndoa wanaumia kimya kimya na ulioko nje hauwezi kujua..na vijana wengi wanapoteza furaha muda mfupi baada ya kuoa
 
Back
Top Bottom