Yule JPM wa Jana, Sio JPM wa leo.

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,864
3,851
JANA:-
"Nchi yangu itakuwa ya Viwanda na elimu bure" JPM.

"Katika Utawala wangu, ukimcheleweshea Mkopo mwanafunzi ujue kazi huna" JPM

LEO:-
-Dar-Ngongoti kufunga kiwanda baada ya Uchumi kuyumba.
-Wanafunzi wailalamikia Bodi ya Mikopo.
-Shule zapigwa mnada baada ya kushindwa kulipa Mikopo.

Yule JPM wa Jana, sio JPM wa LEO

1480513163036.jpg

Chanzo: Mtanzania, Nov 30, 2016.
 
Joni joseph kama José morinho alichukua timu kwa mbwembwe nyingi usajili wa kuvunja record wa pogba, na huyu wetu alivunja record ya kujaza mabrigedia na maprofesa ila tokea ligi imeanza tumekuwa watu wakutoa droo hadi uwanja wa nyumbani siku zinakwenda matumaini yanazazidi kupungua!
 
  • Thanks
Reactions: Gut
Acha tu....haya yana mwisho
Stahiki ninayostahili kulipwa inaitwa fedha ya dili!
 
Hivi mnaposema tufanye Nazi mnamaanisha nini,unaambiwa shule zimeuzwa(ajira zimepotea),dangote kafunga(ajira zimepotea),mikopo imekosekana mabenki tunapokopea mitaji,
Labda huyu kada aelezee kwanza maana ya neno "kazi". Maana mimi binafsi sielewei na pia ninakerwa na hii tabia ya hawa UVCCM kujificha katika kichaka cha "tuchape kazi" kila wanapokosa hoja juu ya mada husika.
 
Tufanye kazi jamani. Hizi ngonjera kwenye social media zinatupotezea muda mwingi mno
Logoff JF au delete kile kitufe cha JF na ufanye kazi uachane na social media. Please mind your own business. We are desperate Leave us alone!
 
Tufanye kazi jamani. Hizi ngonjera kwenye social media zinatupotezea muda mwingi mno
Unatafuta matusi... Watu tunatafuta kazi wewe unasema tufanye kazi!! Kazi zenyewe ziko wap... Mkuu nakuheshimu sanaa kama huna cha kuchangia uwe una nyamaza
 
Tanzania ili tusonge mbele ni lazima tuuondoe Mwenge, usikimbie wala kuzunguka nchini.
Mwenge ni adui wetu namba moja.
Adui wetu namba mbili ni twiga. Tutafute mnyama mwingine aggressive, tuachane na twiga, tuweke hata eagle au simba au chui.
Hatuna mipango hatuna dira hatuna uelekeo.
CCM oyeeee
 
Kazi zenyewe ndo zile anazofanya makonda eti alietukanwa ni mjumbe wa nyumba 10 ccm na shahidi ni mjumbe balaza la wazee ccm mh kwel tufanye kaz hii ngumu kumeza
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom