Yule jamaa aliyetokea mabwepande saa 12 asubuhi alikuwa anenda wapi?

Ninakubaliana na mtoa mada kabisa according CRIME INVESTIGATION first suspect ni aliyemuokota lakini kwa tanzania ni tofauti porojo nyingi ndioa sababu nilitoa mfano huu hapa sikuile,KANUMBA -the first suspect wa kifo cha kanumba alitakiwa kuwa Lulu and the second ni mdogo wake kanumba kwasababu all of them line under the police line of investigation alikuwepo wakati wa tukio hil inasemekana ilisikika sauti ya kiume kwa muda kama ugomvi ndani kwa kanumba na alikuwa anaishi na mdogo wake tu je ninani huyo? Inteligensia yetu inaishia mabwepande tu!!!!!!!,na yulewa kwanza kufika pia anahusika/mtoa taarifa .mfano mwingine Mtambuzi alitoa kisa cha yule mchungaji aliyewaua AJUZA wawili aliyetoa taarifa ni muuaji ilipochunguzwa aligundulika ni yeye aliyewaua so nakubaliana na mtoa mada huyo mtu angechunguzwa pia.
 
Last edited by a moderator:
Yesu akaanza kusema; "Mtu mmoja alishuka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko nayeakaangukia mikononi mwa wanyang'anyi"

"walimvua nguo zake, wakamwumiza na kuondoka, wakimwacha katika hali ya kaaribu ya kufa" wakamweka kando ya barabara.

Kabla ya muda mrefu msafiri mwingine alikuja katika barabara ile ile. Alikuwa kuhani alipomwona yule mtu maskini akilala pale mwenye kuhitaji msaada, alichagua kujali mambo yake na kuendelea na safari yake.

Baadaye, akaja mlawi sehemu ile, alipomwona yule msafiri aliyezimia akilala barabarani, naye
akapitiliza

Muda mfupi baadaye msamaria akaja katika barabara ile yenye ukiwa. Alipomwona yule msafiri mwenye mkosi moyo wake mara moja ukamhurumia, wazo lake la kwanza lilikuwa kumpatia msaada, akaenda alikokuwa na kukagua vidonda vyake. Kisha kwa uangalifu akavifunga "akavimiminia mafuta na divai" kadiri walivyokuwa wakifanya siku zile,kwa ajili ya kutuliza na kuponya. Baada ya kufanya vema alivyoweza, akamnyanyulia juu ya punda wake na kwendelea polepole na safari hadi walipofika penye nyumba ya wageni. Hapo alimweka katika hali ya kupumzika kadri alivyoweza, siku ya pili akampa mwenye nyumba ya wageni dinarii mbili (ikiwa sawa na nusu ya shekeli katika fedha za kiyahudi) na kusema "Mtunze huyu; na chochote utakachotumia cha ziada,nitakapopita tena, nitakulipa"
 
Jamaa alimkuta ulimboka akiwa hoi saa 12 asubuhi kwenye msitu mnene akaanza kumsaidia akiwa ametapakaa damu na alikuwa hamjui. Huyu ahojiwe vizuri anajua mpango mzima.

Kwa maana hiyo aliwageuka wenzie kama mpango mzima ulikuwa ni kutenganisha mwili na roho ya Dr. Ulimboka?!
 
Na wewe badala ya kumuhoji Abied Afisa wa Ikulu aliyekutana na Dr. Ulimboka, pamoja na ACP Ahmed Msangi, unakimbilia kupoteza ushahidi eti wamuhoji Juma Mgunda aliyemuokota na kumsadia Dr. Uli.

Hivi POLISI wameshamuhoji Dr. Deo au wanamuogopa wanajua MISSION itajulikana, maana Dr. Deo anamfahamu afisa wa IKULU Abeid.
 
kuhojiwa ni kawaida lakini futa kauli ya kusema alikua anajua mpango mzima,. unadhani kama yumo humu ndani cku akutana na mtu amepata tazizo atatoa msada tena? CHUNGA KAULI ZAKO UTAKWAZA WATU.
 
Jamaa alimkuta ulimboka akiwa hoi saa 12 asubuhi kwenye msitu mnene akaanza kumsaidia akiwa ametapakaa damu na alikuwa hamjui. Huyu ahojiwe vizuri anajua mpango mzima.

huyu ni msamaria mwema km yule wa vitabu vya dini. basi tuanze kuhoji yule wa kwenye vitabu vya dini alitokea wapi na tukipata jibu ndo tuje kumjadili mgaza. mkuu je unajua asili ya neno " msamaria mwema" imetoka wapi? kuna wasamaria wabaya pia ambao huwa wanawasachi maiti za abiria waliopata ajali na kuwaibia mizigo yao.
 
Naona wana JF tumeishiwa vitu vya kujadili...!!!

Kweli kabisa jamaa Ugrita sinka wake unashangaza,huyu aliyemsaidia ulimboka hatuna wasiwasi nae kabisa ni msamaria angekua mtu wa system lazima angemchoma hata sindano ya sumu au asingemsaidia angemuacha tu na wala asingeangaika kupiga simu ya kuomba msaada kwa rafiki wa ulimboka(namba alipewa na ulimboka mwenyewe)
 
By the way huyo mchungaji alikua anatania ama alikua serious aliposema madaktari warudi kazini na watakaogoma WAPIGWE?.
>hao waliompa kichapo huyo daktari kama ni professional basi kipigo hakikua na nia ya kuua but to send a message,na huyo mkenya nadhani wala hata hausiki.HE COULD BE A FALLGUY na wahusika si ajabu wakawa wanaongelea Timbuktu saa hii.
Na waliowatuma kushusha kipondo kwa dr hawawezi kuwa wajinga kiasi cha kushiriki wao wenyewe lazima walitumia MIDLEMAN ili kusiwe na connection yeyote ya kuwahusisha wao.THE WAY MAFIA DO THINGS
 
Kwa maana hiyo aliwageuka wenzie kama mpango mzima ulikuwa ni kutenganisha mwili na roho ya Dr. Ulimboka?!
Mwanamayu inawezekana kabisa sio kuwageuka ila kutoa taarifa maana ili watu /madocta wageuze attention nakutokana nakufanyiwa mwenzio hivo waingiwe na inferiority complex wasiendelee kugoma,na upande mwingine inawezekana ni msamaria mwema,na upande mwingineanatakiwa ahojiwe na wanainteligensia kama anadanganya watajua kama ni msema kweli watajua.NASISITIZA TUME HURU
 
Last edited by a moderator:
Huo msitu una barabara?hili ni swali muhimu kwa walw wanaosema alikutwa msituni vs wale wanaosema alikutwa barabarani.Kama huo msitu una barabara,basi alikutwa kwenye barabara ya msituni,cha muhimu sasa ni huyo mtu aseme alitokea wapi,inawezekana ni barabara inayotokea sehemu wanapoishi watu halafu ikawa inapita sehemu ya msitu,hii ni kama kuna makazi ya watu karibu na msitu huo.Haina haja ya kushambuliana,JF ni uwanja wa majadiliano na hoja kwa hoja.
 
Unanistaajabisha sana, Msamaria mwema ahojiwe kwa nini? Mungu ambariki sana yeye na uzao wake. Wangemfuata wale wabaya wake si wangemmalizia. Kama huna hoja stop writing.
 
Unanistaajabisha sana, Msamaria mwema ahojiwe kwa nini? Mungu ambariki sana yeye na uzao wake. Wangemfuata wale wabaya wake si wangemmalizia. Kama huna hoja stop writing.
Watanzania tusiwe na akili nyepesi kiasi hiki,kuhojiwa kwake si lazima awe ni mtuhumiwa.Lakini mimi siafiki kuhojiwa kwa yeyote na polisi.So licha ya kwamba sipingi yeye kuhojiwa na a credible investigators/investigating unit.Ila nina wasiwasi na nia ya mleta mada.
 
Jamaa alimkuta ulimboka akiwa hoi saa 12 asubuhi kwenye msitu mnene akaanza kumsaidia akiwa ametapakaa damu na alikuwa hamjui. Huyu ahojiwe vizuri anajua mpango mzima.
ule msitu umezungukwa na makazi ya watu na ndiyo maana tunaomba uondolewe haraka. huwezi kuwa na hifadhi ya taifa katikati ya maeneo ya makazi.
 
kama alikuwa anawai UBONGO, mabasi ya Kagera, songea burundi etc.....nini mbaya jamani!!
 
Ndio maana siku hizi watu hawana huruma kwa ajili ya mambo kama haya.Mtu anatoa msaada na yeye mnamgeukia...kha..Kweli wanadamu ni viumbe wazito...
 
Watu wa kwanza kuleta habari hapa ni wafuasi wa CDM,update zote zimeletwa na wafuasi wa CDM ,yaani tokea kuanzia kutekwa ,yaani hatua ya mwanzo leaders club,mazungumzo ya simu,kutupwa ,kuokotwa ,za wanaharakati ,za polisi ,za ndani ya chumba cha mgonjwa Uli zote wanashusha hapa ni wafuasi wa CDM huoni kama CDM inahusika kwa kiasi fulani na huu mkenge aliopandishwa Kova pale kanisani ,inawezekana kabisa ni mipango ya kupoteza muelekeo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom