Yule dada maarufu kama "Dada wa Taifa" inasemekana kaachana na siasa.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
1.Kweli ulitupa tabu,tena tabu kubwa sana
Tabu zilo na sababu,hasa ulipo tuchana
Uliwasema vibabu,wazee hata vijana
Mapoti na mabawabu,uliwaponda mchana
Dada kuacha siasa,wazee tutapumua.



2.Sasa tutakula bata,kwa siasa kuachana
Ingawa ulitusuta,na matusi kutukana
Ukatupeleka puta,kwa mwendo wa kukazana
Na pengine tulijuta,kwanini tulijuana
Dada kuacha siasa,wazee tutapumua.


3.Hakika ulitutesa,na vichwa tukagongana
Mambo yetu kuyanasa,pale tulipolumbana
Ukafunua mikasa,visa vilofichikana
Sasa tutakupa visa,uje hatuto kubana
Dada kuacha siasa,wazee tutapumua.


4.Siasa uwache kweli,isiwe twataniana
Uje kuzamisha meli,tena tuanze chimbana
Useme kusema ngeli,haijui yule bwana
Hapo kusema ukweli,kifwatacho kuuwana
Dada kuacha siasa,wazee tutapumua.

5.Ukitaka kutusema,kwanza tuje ambiana
Tushituwane mapema,ili mambo fichiana
Tusije shindwa kuhema,mengine kuzibiana
Mwisho tuka kata pema,maneno kurushiana
Dada kuacha siasa,wazee tutapumua.


6.Umesha ule wakati,wakti wa kukimbizana
Sasa mipya mikakati,mwaka le tutaonana
Tuzifaidi chapati,na keki tulogawana
Ukikipata kibuti,twanze kwanza konyezana
Dada kuacha siasa,wazee tutapumua.


7.Dada na kwaga kwa heri,kwa kheri ya kuonana
Nakuacha u buheri,hakuna tena banana
Zile zahama na shari,sasa tutasikizana
Tupige tari zimari,tutakutana kabana
Dada kuacha siasa,wazee tutapumua.


SHAIRI-DADA KAACHA SIASA
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
1.Kweli ulitupa tabu,tena tabu kubwa sana
Tabu zilo na sababu,hasa ulipo tuchana
Uliwasema vibabu,wazee hata vijana
Mapoti na mabawabu,uliwaponda mchana
Dada kuacha siasa,wazee tutapumua.



2.Sasa tutakula bata,kwa siasa kuachana
Ingawa ulitusuta,na matusi kutukana
Ukatupeleka puta,kwa mwendo wa kukazana
Na pengine tulijuta,kwanini tulijuana
Dada kuacha siasa,wazee tutapumua.


3.Hakika ulitutesa,na vichwa tukagongana
Mambo yetu kuyanasa,pale tulipolumbana
Ukafunua mikasa,visa vilofichikana
Sasa tutakupa visa,uje hatuto kubana
Dada kuacha siasa,wazee tutapumua.


4.Siasa uwache kweli,isiwe twataniana
Uje kuzamisha meli,tena tuanze chimbana
Useme kusema ngeli,haijui yule bwana
Hapo kusema ukweli,kifwatacho kuuwana
Dada kuacha siasa,wazee tutapumua.

5.Ukitaka kutusema,kwanza tuje ambiana
Tushituwane mapema,ili mambo fichiana
Tusije shindwa kuhema,mengine kuzibiana
Mwisho tuka kata pema,maneno kurushiana
Dada kuacha siasa,wazee tutapumua.


6.Umesha ule wakati,wakti wa kukimbizana
Sasa mipya mikakati,mwaka le tutaonana
Tuzifaidi chapati,na keki tulogawana
Ukikipata kibuti,twanze kwanza konyezana
Dada kuacha siasa,wazee tutapumua.


7.Dada na kwaga kwa heri,kwa kheri ya kuonana
Nakuacha u buheri,hakuna tena banana
Zile zahama na shari,sasa tutasikizana
Tupige tari zimari,tutakutana kabana
Dada kuacha siasa,wazee tutapumua.


SHAIRI-DADA KAACHA SIASA
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Dola imefanya yake. Zile hide my Id now ni expose my Id. Never trust a women, never my furendii
 
Nyepesi nyepesi zinadai kalamba milioni 660 za Kitanzania ili aache kumsema vibaya jiwe
 
This series is so fantastic
tapatalk_1540955185820.gif
 
Nyepesi nyepesi zinadai kalamba milioni 660 za Kitanzania ili aache kumsema vibaya jiwe
Kakosea sana..tena sana...Siri zote nzito nzito za nchi hii anapokea vijisenti hivyo..angewapiga kama bilioni 1 hivi au bilioni 1.5
 
Pumzi imekata..katumia silaha zote lakini kachemsha..watu washaanza kumuona wa kawaida..Hana jipya na hajapewa hata senti
 
Dada kuacha siasa, uamuzi wa busara
Kingine dada kukiacha, matusi na uhasama
Dada kumbuka wewe mama, wanao wanahitaji busara
Dada kuacha siasa, wazee tumejawa na furaha


Amani nchi imetawala, tangu enzi za Nyerere Baba
Dada ulitikisa wetu utawala, kwa habari zako zilizofubaa
Uongo nyumbu uliwajazaa, wengi wako ni watwanaa
Dada kuacha siasa, wazee tumebaki furahani

Dolari ngapi wahitaji, nikulipe upotee
Siri za Alhad sizitaki, zipotezee ndani uzisweke
Makonda ulimghasi, hakutamani ulimchafua kiongozi
Dada kuacha siasa, wazee tumebaki furahani

Kila adui umemtukana, wanaume wamekua mashoga
@Chahali umemkosea heshima, ubaya umemtwika
Dada ulikosa staha, bravo njia uliyoishika
Dada kuacha siasa, uamuzi uliojaa busara
 
Pesa za fisiem haijawahi kumwacha mtu salama.
Sasa anaunga juhudu za bwana jiwe tu na utawala wake
 
Back
Top Bottom