Yule aliyesema zoezi la uokoaji/uopoaji linatarajia kukamilika ifikapo saa 12 jioni kwa nchi zilizoendelea angewajibishwa jana mapema

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,938
Huna taarifa sahihi ya waliokuwa ndani ya kivuko, unataarifa ya waliookolewa na kuopolewa tu. Umetumia hesabu gani kukokotoa na kupata jibu kuwa zoezi litaishia muda fulani?
Hata kama alifanya probability , probability nayo inahitaji ukokotoaji na jibu hata lisipokuwa kamili basi litatofautiana kidogo tu.
 
Bado kimebinuka tu siku ya Tatu watafute meli ivutwe itakaa sawa sababu haina mizigo mizito ni nyepesi
Mkuu sio rahisi kama maelezo yako yanavyosema inahitaji utaalam wa hali ya juu kumbuka hcho chombo kimebinuka kwao bila shaka kuna watu au vitu ndan yake.
 
Mkuu sio rahisi kama maelezo yako yanavyosema inahitaji utaalam wa hali ya juu kumbuka hcho chombo kimebinuka kwao bila shaka kuna watu au vitu ndan yake.
Vitu Magari na mizigo ukaa nje na huwa avifungwi vishazama ndani,kuopolewa kwa meli ya winchi,
 
Kwa namna ilivyo abiria waliokuwa ndani wamekaa naamini bado hawajatolewa, hivyo kusema zoezi linaisha mapema siyo rahisi sana
 
Mkuu sio rahisi kama maelezo yako yanavyosema inahitaji utaalam wa hali ya juu kumbuka hcho chombo kimebinuka kwao bila shaka kuna watu au vitu ndan yake.
Vitu gani ambavyo viko ndani yake vitakavyokuwa na thamani ya watu waliofariki?

Fikiri kabla hujaandika.
 
Hukunielewa mkuu nlichosema,sikumaanisha kma kwakuwa kuna vitu ndio haiwezi kubiruliwa hapana nilichokusudia unaweza ukatumia hivyo vifaa vya kubirua wakati uhisi unataka kuokoa watu kumbe ndo unazidi kuangamiza.
Watu wa rescue bila shaka waliyafkiria yote hayo ila lazima waangalie possibilty ya watu kuokoa watakapofanya hvyo na ukiangalia hio hali yenyew ilivyo.
 
Bado kimebinuka tu siku ya Tatu watafute meli ivutwe itakaa sawa sababu haina mizigo mizito ni nyepesi

Tatizo ni kifaa cha kukiinuwa na kukiweka. Sawa,kama waliweza kusitiza uokoaji ilipofika jioni,je wataeza kuwa na meli/fery yenye Crane ilio na uwezo wa tani 50?
 
Hukunielewa mkuu nlichosema,sikumaanisha kma kwakuwa kuna vitu ndio haiwezi kubiruliwa hapana nilichokusudia unaweza ukatumia hivyo vifaa vya kubirua wakati uhisi unataka kuokoa watu kumbe ndo unazidi kuangamiza.
Watu wa rescue bila shaka waliyafkiria yote hayo ila lazima waangalie possibilty ya watu kuokoa watakapofanya hvyo na ukiangalia hio hali yenyew ilivyo.
Hivi unafikiria kuokoa watu baada ya kusitisha zoezi la uokoaji kwa SAA 12?
 
Kinachonisikitisha ni pale Mkuu wa mkoa kusitisha zoezi sababu ya giza, yaani haiingii akilini kabisa. Mimi ninavyofahamu watu wanaoishi maeneo yenye bahari, maziwa, na mabwana wanauzoefu mkubwa wa kuzamia bila hata vifaa. Na uzoefu wao ni zaidi hata ya hao jeshi la uokoaji. kwa nini asingewaachia watu wanaojiweza kuendelea na uokoaji yeye ahakikishe vinapatikana vyanzo vya mwanga wa kutosha eneo hilo ? Hapa sipati jibu. Ninacho hisi huyo mkuu wa mkoa labda amezoea kulala mapema hivyo alizidiwa na Usingizi akashindwa kuondoka na kuwaacha watu wakiendelea na uokoaji akahisi watu wangemsema hivyo dawa waondoke wote, pili inawezekana jamaa ana wivu na mkewe hakutaka mkewe alale peke yake, ikapelekea asitishe zoezi. mbadala na hapo sielewi sababu nyingine....!! Mungu baba wapumzishe marehemu wote mahali pema, Amen.
 
Back
Top Bottom