Yule afande shoga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yule afande shoga

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 4, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  [​IMG]

  Kova, aliliambia Ijumaa Wikienda juzi kwamba kitendo cha Mkenga kimemkwaza yeye kama kiongozi wa kanda ambayo koplo huyo anafanyia kazi, lakini pia ni aibu kwa jeshi la polisi.

  Kamanda huyo alisema kuwa tayari jeshi la polisi limekwishamfungulia mashtaka Mkenga na kwamba bado uchunguzi unaendelea.

  “Akikutwa na hatia, atahukumiwa kulingana na taratibu za jeshi la polisi,” alisema Kova na kuongeza: “Uchunguzi unaoendelea ndiyo utakaoamua hatma yake, ikibainika ni kweli amekuwa akihusika na vitendo hivyo, jeshi halimvumilia.”
  Mbali na kauli hiyo ya Kamanda Kova, habari za ndani zinasema kuwa Jumamosi iliyopita (juzi) ndiyo ilikuwa siku ya kwanza kusikiliza shauri la Mkenga katika Mahakama ya Kijeshi.

  Habari hizo zinaeleza kuwa awali mfanyabiashara wa Kenya alipewa wito wa kufika bila kukosa kwenye Kituo cha Polisi Usalama, Magomeni, Dar es Salaam ili aweze kutoa ushahidi wake.

  Ilielezwa kuwa katika maelezo aliyopewa mfanyabiashara huyo ni kwamba iliamuliwa na uongozi wa polisi, kulishughulikia suala la Mkenga kijeshi, hivyo hakutakiwa kukosa ili ukweli uwekwe hadharani.

  “Yule Mkenya alifika, kikaandaliwa chumba maalumu cha kuendeshea kesi,” alisema mtoa habari wetu bila kumtaja hakimu.

  Akiendelea zaidi, mtoa habari wetu alisema kwamba wakati wa kusikiliza kesi, awali alitakiwa Mkenya huyo kueleza kilichotokea mpaka wakafumaniwa chumbani na Mkenga katika jaribio la kufanya mapenzi ya kinyume nyume.
  Katika maelezo yake, mfanyabiashara huyo wa Kenya alisema kuwa alifahamiana na Mkenga alipopatwa na matatizo ya kutekwa na wahuni ambao walimpora kila kitu.

  “Yule Mkenya alisema kuwa alipofika kwenye Kituo cha Polisi Kimara ndiyo alikutana na Mkenga ambaye alianza kumtongoza na baada ya hapo alitoa taarifa kwenye gazeti hili la Ijumaa Wikienda ambalo liliendesha oparesheni ya fumanizi,” kilisema chanzo chetu.

  Mtoa habari wetu alisema kwamba baada ya Mkenya huyo kutoa maelezo yake, Mkenga alipewa nafasi ya kumuuliza maswali mfanyabiashara huyo kabla ya shauri hilo kuahirishwa mpaka leo (Jumatatu).

  Aidha, ilielezwa kuwa baada ya kumaliza kusikilizwa kesi hiyo, Mkenga aliwekewa dhamana na ndugu zake, ikiwa ni baada ya kukaa mahabusu kwa siku 11.

  Baada ya kupata maelezo hayo, juzi waandishi wetu walifanikiwa kumpata mfanyabiashara huyo wa Kenya ambaye alithibitisha kuitwa polisi na kutoa maelezo yake katika mahakama ya kijeshi.

  “Niliitwa na mtu ambaye nilielezwa kuwa yeye ni OCD, nikatoa maelezo yangu naye Mkenga akaambiwa aniulize maswali kisha tukaambiwa turudi polisi Jumatatu (leo) kwa ajili ya kuendelea na kesi,” alisema mfanyabiashara huyo wa Kenya.
  Nyeti zaidi kuhusiana na ishu hiyo, zinasema kuwa tangu Mkenga alipofumaniwa na habari yake kutoka gazetini, nyumbani kwake Keko, Dar es Salaam ni kama msibani kutokana na ukimya uliotanda pamoja na vilio katika vipindi kadhaa.

  Wakiongea kwa masharti ya kutotaka majina yao ‘yachorwe’ gazetini, baadhi ya majirani walisema kuwa tukio la Afande Mkenga limekuwa pigo kubwa kwa familia yake.

  “Mara nyingi nyumba ipo kimya, lakini kuna kipindi vilio vinasikika, halafu kuna mtoto wake wa kike anasoma sekondari yeye aligoma hata kwenda polisi kumuona baba yake wakati anashikiliwa mahabusu,” alisema mmoja wa majirani hao huku akiungwa mkono na wenzake.

  Mbali na hilo, habari za ndani ya Jeshi la Polisi zinasema kwamba Afande Mkenga amewasikitisha askari wengi kwa kuwa ni tegemeo yanapotokeo mapambano dhidi ya majambazi.

  “Imetusikitisha sana, jamaa ni tegemeo letu yanapotokea mapambano ya ana kwa ana na majambazi. Mara nyingi anakuwa kwenye ‘difenda’ mstari wa mbele, kwa kweli hili ni pigo kubwa,” alisema askari mmoja wa Kituo cha Usalama kwa sharti ya kutotajwa gazeti.

  Ijumaa Wikienda ndilo gazeti lililosimama kikamilifu katika kusuka fumanizi la afande huyo kabla ya kuandika habari iliyotoka ukurasa wa kwanza katika toleo lake namba 93 la Februari Pili, 2009, ikiwa na kichwa: “Afande Shoga Anaswa.”
  Global Publishers - Tanzania Newspapers
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  kweli hili ni pigo na matokeo ya kufungwa kwa ile blog iliyokuwa maarufu kwa mambo haya, tutaona mambo mengi sana na ya ajabu humu JF
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  MOds.... Tunaomba mtusaidie kuondoa influx ya zile posts za zeuchungu humu jamvini!! Tutaendelea vipi na mapicha uchiuchi hivi... tena hii ilikuwa kule pia

  zinahamishiwa humu jamani eehhh
   
 4. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  MTM kueleza ukweli ndio imekuwa Nongwa? huoni kuwa ni kashfa kwa Kwa afande kama huyu kuwa shoga? haya ndio maendeleo yetu hapo bongo?Tunaiga mambo ambayo hatuyawezi kuyafanya imekuwa kitu kizuri afande kama huyu kuwa shoga? itabidi Seriakali ikomeshe mambo kama haya yasitokee kwa mtu mwengine kama huyu afande shoga. Nimeweka hapo ili watu wajuwe kuwa hicho kitendo alichofanya afande shoga kisirudiwe tena na Maafande wanaotulindia nchi yetu hapa hatupo Ulaya wanako ruhusu mambo ya ushoga MTM nafikiri unielewe vizuri kwa nini nimeweka hiyo picha sina nia ya kumuadhiri Afande shoga la hasha napeleka huo ujumbe kwa Maafande wengine iwe ni fundisho kwao wasituaibishe upo hapo MTM? na nimeipata katika gazeti hili hapa hebu Bonyeza hapa Global Publishers - Tanzania Newspapers
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mkuu nakusoma vyema... ila tukianza kuelekea huko hapatakalika hapa jamvini, or at least ungeondoa hiyo picha ili iwe kama habari ya kawaida

  Tuko pamoja without zeuchungu mentality, au sio
   
 6. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,304
  Trophy Points: 280
  Moderator.... tafadhali pamoja na "uhuru wa kupost tulionao naomba hakikisha JF haiwi jalala la kuokoteza habari za kipumbavu... Hili sio gazeti la uwazi au ze-utamu... pse...
   
Loading...