Yuko wapi Wilfred Lwakatare? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yuko wapi Wilfred Lwakatare?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kidudu Mtu, Nov 13, 2009.

 1. Kidudu Mtu

  Kidudu Mtu Member

  #1
  Nov 13, 2009
  Joined: Nov 7, 2009
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aliwahi kushika nyadhifa kadhaa kwenye chama cha wananchi (cuf) na hata kuwahi kuwa mkuu wa kambi ya upinzani bungeni (kama kumbukumbu zangu ziko sawa). Kukatokea mtafaruku cuf, akavuliwa wadhifa wake. Akadai kuwa bado ataendelea kubakia cuf. Kisha siku chache baadaye zikaandikwa taarifa kuwa amelamba matapishi yake na amejiunga na chadema. Hajasikika siku za karibuni....ni mkakati wake, au ndo amefika kikomo cha uanasiasa?
   
 2. Nyumbu

  Nyumbu Senior Member

  #2
  Nov 13, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni mweyekiti wa CHADEMA mkoa wa Kagera. Amejichimiba huko Kagera, anajenga chama kwa kwenda mbele, subiri 2010 utaona matunda ya kazi yake.

  .
   
 3. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #3
  Nov 13, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Siwaamini sana mijitu inayohama hama vyama hata siku moja...? if there is problem you solve it siyo kuhama/kukimbia chama well labda anaweza kuwa useful kwa chadema time will tell!
  Lakini usisahau wafuatao waliokimbia vyama vyao..
  tambwe (hopeless man), kabouro (hopeless man), masumbuko (hopeless man) lyatonga (ametuchosha wanamageuzi) ..the list goes on...
  All the best lwakatare..however, you will never never get a trust from me...
   
 4. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #4
  Nov 13, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Yupo tu anauza chips kuku na matikiti maji
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Nov 13, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Yuko dar es salaam leo nimekutana nae ubalozi wa kenya mchana
   
 6. Nyumbu

  Nyumbu Senior Member

  #6
  Nov 13, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mtoa hoja ameuliza Lwakatare yuko wapi siku hizi na sio yuko wapi leo. Lwakatare amehamia CHADEMA kutoka CUF, haja hamahama kwenye vyama. Mimi nawaheshimu wauza chips kuku kuliko mafisadi. At least wanapata kipato chao halali kutokana na jasho lao.
   
 7. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ameshakwambia hiyo ndiyo itakuwa mwisho kuhama hama...safari moja huanzisha nyingine....CUF-CHADEMA-CCM-.....
   
 8. Nyumbu

  Nyumbu Senior Member

  #8
  Nov 13, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ameshakwambia hiyo ndiyo haitakuwa mwisho wake kuhama...usilolijua ni kama usiku wa giza

  .
   
 9. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #9
  Nov 13, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wewe wafahamu tuondoe gizani
   
 10. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  nafikiri sana anajuta sna. Walimdanganya sana CHADEMA. na kwa jinsi ninavyoijua Bukoba mjini sijui kama atashika nafasi ya nne katika UBUNGE.

  naomba hii muiNOTE kisha mniulize baada ya uchaguzi.

  Watu hawana inami naye ni ndumilakuwili tu.
   
 11. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Acha uzushi, dalili ya mvua ni Mawingu; chini ya Mwenyekiti Lwakatare CHADEMA imeshinda mitaa na vijiji kuliko chama chochote cha upinzani majimbo yote ya mkoa wa Kagera ikiwemo jimbo lake la Bukoba Mjini

  Asha
   
 12. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #12
  Nov 14, 2009
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  BRBR unakosea!Huyu jamaa aliahidiwa unaibu katibu mkuu CHADEMA kwani walitaka kumtosa bwana Zitto ili apewe yeye,lakini Zitto alipogundua hilo ndipo akaanza harakati za kuwania uenyekiti.Wazee wa CHADEMA walipoketi na Zitto kumshawishi aachane na kugombea uenyekiti yeye akawajibu mbona swala la kuenguliwa unaibu katibu mkuu na kubandikwa Lwakatare hamlizungumzii!?Hapo mzee Bob Makani akatoa amri kuwa Lwakatare awe mwamasishaji chama Kagera na Zitto aendelee na nafasi yake ya unaibu katibu mkuu.Yaliyotokea wote mmeyaona au kuyasikia sitaki kuyarudia tena,ila kwa taarifa ya jana tuu bwana Lwakatare amekutana na captain Chiligati ktk ukumbi wa Blue Pearl Hotel pale Ubungo plaza kwa mazungumzo yaliyochukua takribani masaa 2,sasa kilichozungumziwa huko ni siri yao ila tutege masikio yetu kwani hawa sisieeemu siwaaamini sana,maana Akwilombe,Tambwe,Atiki,Ngawaiya,Lamwai,Mtemvu,mswanzigwanko...n.k wote walikuwa katika upinzani!
   
 13. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #13
  Nov 14, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  sasa tuone kama Yeye Rwekatare atakuwa hata mshindi wa nne katika Uchaguzi wa ubunge wa Bukoba mjini.

  naweza kukuthibitishi kuwa baada ya CHADEMA kujulikana kama chama cha KIDINI na UKABILA sijui kama watashinda kule Bukoba na Kigoma.
   
 14. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #14
  Nov 14, 2009
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wakuu heshima mbele
  Vyovyote siasa za Tanzania zinavyofanyika ni lazima mpinzani aliyenuia ateseke sana kupata mahali pa kufanya siasa halali na zenye effects dhidi ya CCM. Kama tungekuwa na wagombea binafsi baadhi ya migogoro katika vyama vya siasa na pia mchezo wa kuhamahama usingekuwa dili.

  Lakini nimjuavyo Lwakatare CHADEMA ndo mahali pake kabisa. Hapo atafanya kazi ya siasa na atadeliver

  Tafadhali tumtakie mema!! Tusimtangulizie sababu za kuanguka. Hii ni dhambi kubwa yetu waafrika. Kabla ya kumtakia mwenzetu kufanikiwa tunamtangulizia maneno ya kumdhoofisha.
  Acheni hizo wapendwa.
   
 15. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #15
  Nov 14, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Lwakatare kafanya kosa kubwa sana kuhama CUF na kukimbilia CHADEMA bila kufanya tathmini ya kutosha.CUF walikuwa wakimtumia Lwakatare kuondoa dhana ya udini na Upemba ndani ya chama ndiyo maana tulikuwa tukimsika Lwakatare kila CUF walipokuwa wakifanya siasa zao huku bara.

  CHADEMA ni chama kilichojikita zaidi kanda ya kaskazini hasa mkoa wa kilimanjaro.CHADEMA nao wanamatatizo kibao lakini siyo tatizo la udini kama ilivyo kwa CUF hivyo hawawezi kumtumia Lwakatare kama walivyokuwa wakifanya CUF.Bado tutaendelea kumsahau tena asipokuwa makini anaweza hata udiwani asiupate.
   
 16. GP

  GP JF-Expert Member

  #16
  Nov 14, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  nadhani atakua amefanya jambo la busara sana, huyu ni msomi mzuri sana wa alama za nyakati, CHADEMA ndio chama pekee cha upinzani tanzania kilichaobaki na cha kweli, CUF si ndio hivyo tena ni tawi la ccm tuu, kwishney!!
   
 17. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #17
  Nov 14, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lwakatare amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Kagera. Pia aliwahi kutambulishwa na Dr Slaa kuwa ni afisa wa makao makuu ya CHADEMA akiwa na majukumu maalum ndani ya Ofisi ya Mwenyekiti wa Taifa

  CUF si walimuondoa unaibu katibu mkuu? Kwani alikuwa na nafasi gani CUF wakati anaamua kuhamia CHADEMA?

  serayamajimbo
   
 18. m

  mtemi Member

  #18
  Nov 14, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huyu nae anaelekea macweo kama ya lyatonga - mzee wa inci hii
   
 19. Nyumbu

  Nyumbu Senior Member

  #19
  Nov 15, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa vigezo vipi?

  .
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Nov 15, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Aaaaah kumbe ndio tumetoka huku eeeeh! sasa naipata pata picha nzima.
   
Loading...