Elections 2010 Yuko wapi sheikh yahaya hussein na utabiri wake feki?

Kanjunju

Member
Oct 8, 2010
92
6
Kama kuna mambo watanzania wengi walikuwa wanatarajia kutokana na utabiri feki wa sheikh Yahya basi kuona uchaguzi mkuu unasimama kama ilivyotokea mwaka 2005.Uzushi wa mtabiri huyu ni kuwa mmoja wa wagombea wa urais angekufa kabla ya tarehe ya uchaguzi.Lakini uchaguzi umepita na hakuna lililotokea.Sijui yuko wapi sasa kujibu nini kimetokea.Sisi tusioamini uzushi ule tulijua hakuna kitu kama hicho.Watanzania wawe makini na mtu huyu.
 

Malunde-Malundi

JF-Expert Member
Jan 10, 2008
1,288
130
Jamani

Ukweli ni kuwa uchaguzi haujafanyika;hakueleweka na wote hatukumwelewa

Ili uchaguzi ufanyike

1. Vifaa vipelekwe mapema vituoni
2. Wananchi wawe huru kuchagua wanayemtaka bila vitisho vyovyote
3. Tume iwe huru
4. Wasimamizi wawe huru na wasio na uwoga
5. Vyama visiwe na fikra za kuiba vikiamini kuiba ni kuiba ni sawa na dhambi
6. Kura zipigwe kwa uwazi
7. Wanaohesabu kura wawe wazi na kura zitundikwe vituoni
8. Matokeo yatoke bila kubadilishwa
9. Kusiwepo na vituo hewa

Naona yote hayakuwepo kwa asilimia 100% ; hivyo naona uchaguzi haukufanyika kwa sababu zifuatazo

1. Vifaa vipelekwe mapema vituoni [sehemu ziingine hazikufika kabisa kama mpanda na sehemu za Zanzibar]
2. Wananchi wawe huru kuchagua wanayemtaka bila vitisho vyovyote[tulitishwa na JWTZ]
3. Tume iwe huru [Akina makame ni mapandikizi]
4. Wasimamizi wawe huru na wasio na uwoga [du watu wanalazimishwa kutoa matokeo tofauto, angalia kibaham,shy,mbeya vijijini,karagwe, kilombero, segerea nk]
5. Vyama visiwe na fikra za kuiba vikiamini kuiba ni kuiba ni sawa na dhambi [CCM ilijianda kuiba, sijui hata masanduku ya kura ambayo Makame alishasema hayapo huko Tunduma yalitoka wapi tuliona kura mitaani zikiwekwa alama ya JK, wabunge wa ccm na madiwani]
6. Kura zipigwe kwa uwazi [kidogo 50% kumbe kulikuwa na vituo hewa nchi nzima]
7. Wanaohesabu kura wawe wazi na kura zitundikwe vituoni [za urais zilipelekwa makao makuu tofauti na sheria iniayotaka matokeo kutundikwa kituoni na kutanganzwa ktk majimbo]
8. Matokeo yatoke bila kubadilishwa [tumejione uchakachuaji wa hali ya juu, segerea mfano wa kuigwa kwa hilo]

Nakubaliana na shehe yahaya aliposema uchaguzi hautakuwepo kweli haukuwepo ila kulikuwa na uporaji wa uchaguzi, sijui kwa nini tumeingia gharama wakati kumbe hadi maksi walikuwa wamempa na walijua watacheza na excel mwanzo mwisho; wangezema tu watu waproject namba zisifanane ila mshindi aweke yeye Yule yule

Funzo: Tanzania itapata uhuru wa pili pale tu watu wake watakapoamka na kuudai kwa nguvu ya umma na bila kujali mabomu yao; njaa huwa inafunza ipo siku tu maana ninavyoona hamna mtu mwenye utashi kusaidia kusukuma gurudumu mbele, zaidi ya kupeana ulaji kwa uswahiba na urafiki, kuuza mbuga na madini kwa bei chee, ni mambo ambayo yanakera ila ipo siku yatapatiwa

Mnaweza kuongeza mnavyoona inafaya; lakini kumbe shehe yahaya alimaanisha hivi (atachaguliwa mwingine ila hata hatakaribi kwenda ikulu maanake uchaguzi haukufanyika, nafikiria alichelea kusema kuna uporaji unakuja)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom