Augustoons
JF-Expert Member
- Oct 31, 2007
- 409
- 30
Wadau,
Kama mtakumbuka vizuri wakati wa kampeni na hata baaday ya uchaguzi kuna kitabu kilichapishwa nadhani na Prince Bagenda na nakala zake kuchapwa sana magazetini.Naam kitabu hiki kilitueleza matumaini mengi ambayo kwetu yalitafsiriwa kama mategemeo ya awamu ya nne.Kauli za kitabu hiki ziliendana kabisa na kauli mbie ya kasi mpya,nguvu mpya,ari mpya.Maisha bora kwa kila mtanzania.Na kwa upande mwingine zilipingana kabisa na kitabu cha mwisho cha mwalimu Nyerere ambacho alikiita "UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA"kitabu ambacho ni kidogo ila kama viongozi wetu wangekuwa wanakirejea sana basi hata mkuu wa kaya kwene uteuzi wake wa watendaji serikalini na baraza la mawaziri kingemsaidia.
Mimi kama mmoja wapo niliyeshawishika sana na tumaini lililorejea na matumaini tuliyoelezwa humo nilisubiri kwa hamu sana kuliona hilo tumaini. Hamu yangu ilizidi sana pale ambako maadhimisho ya siku 100 za mzee wa kaya ikulu yalipoadhimishwa na kutumia siku hii kueleza mipango mikakati mingi ya awamu ya nne,na ile itakayoanza kutekelezwa hivi punde(wakati huo).Kusema kweli chachu hiyo ilizidi kukolea pale ambapo mkuu wa kaya aliunda tume ya kuchunguza mauaji ya wafanyabiashara wa mahenge na mara tu baada ya tume kumaliza kazi yake mkuu wa kaya akatoa maamuzi. Kwa kweli nilisema kwa kasi hii basi tutafika mbali.Maamuzi haya na mengine ambayo nilikuja kugundua ni ya kasi tu pale ambapo yaligusa non-mtandao au antimtandao yalitupa matumaini watanzania wengi. Lakini taratibu kasi hiyo nikaona kwa tathmini yangu inaanza kulegea kama vile gari lililokuwa kwenye spidi kali halafu ghafla horse pipe ikakatika.
Toka hapo sijamwona Bagenda tena akitutolea tathmini wala magazeti ambayo nayo kwa wakati huo fasihi simulzi ilikuwa juu ya kasi mpya. Taratibu magazeti yakaanza kubadili mwelekeo toka kuwa kasi mpya hadi kuwa sumu kwa uongozi.Hii ilinikumbusha sana jinsi kampeni za kibaki zilivyokuwa miaka ile na ambavyo NGos,magazeti na wanharakati wengine walivyokuwa wanamkampenia na kuwa na matumaini makuwa sana na kibaki lakini baadaye hayo hayo yakaja kuandika kitabu kiitwacho "NEVER AGAIN".Je,watanzania mnataka kunisadikisha kuwa na sisi au ninyi mmeanza kuandika page za mwisho za kitabu hicho cha never again.
Binafsi japo mtatofautiana sana na mimi na hilo nalitegemea kwa kuwa najua jf ni uwanja wa hoja,and lawyers say "we must agree to disagree" naamini kuwa serikali ya mkapa japo tulikuja kugundua baadaye kulikuwa na mafisadi na ufisadi mkubwa bado ilileta matumaini makubwa kwa watanzania kuliko ya sasa. Kwani pamoja na kula walikokula bado waiweza kutekeleza ule msemo wa wazungu kwamba "you are eating and we are eating tu" ambapo mwanamuziki mmoja hapa nchini aliwahi kupiga wimbo unaofanana na kauli hiyo usemao "Na sisi huku tupate ae aeeeeee".
Ni kipindi cha Ben ambacho tulishuhudia kukua kwa sekta ya mawasiliano, barabara nyingi kujengwa pamoja mikakati kama MMEM,ulipaji madeni nk.mishahara mingi ilokuwa duni wakati huo ilipanda wakati wa ben licha ya serikali yake kukumbwa na balaa nyingi anapoanza uongozi ikiwamo EL Nino, mv bukoba,kivuko cha kilombero nk. Lakini serikali ya mkuu wa kaya imekubwa na mambo mawili tu,Kukauka kwa mabwawa ya umeme na labda mfumuko wa bei. Hata hivyo nikiangalia mipango yote karibu 60% ya miradi inayotekelezwa au iliyotekelezwa bado ni programu zilizokuwa hazijaisha,zinatekelezwa au zinamaliziwa kutekelezwa na serikali ya awamu ya tatu. Mfano mzuri ni barabara bahati nzuri nilifanikiwa kufanya utafiti kuhusu miradi ya barabara na bomoa bomoa kule TANROADS NA Kwingineko nikaiona hiyo mipango kuwa barabara fulani itajengwa lini na kwa kiwango gani na pesa itatoka wapi.
Cha kushangaza sasa mimi sioni mabadiliko tuliyoyategemea zaidi ya ahadi. Ahadi bado ni nyingi na kasi ya utekelezaji wake ni kama 0.05% na hii inanifanya nimtafute Bagenda na kumuuliza kulikoni?miaka inazidi kukimbia wakati kasi inazidi kupungua. Katika matumaini yote tulokuwa nayo bado utekelezaji wake hata 20% haujafikia,sasa leo ni miaka mitatu wasiwasi wangu ni kuwa utekelezaji wake unaweza usifike hata nusu. Je, Mhe.Bagenda unatunga kitabu kingine?je,wadau wenzangu tumaini lililorejea bado lipo au niamini vingine.niendelee kuvuta subira?au litarejea awamu ya pili ya uongozi wa mkuu wa kaya?