Yuko Wapi Prince Bagenda Na Tumaini Lililorejea?

Augustoons

JF-Expert Member
Oct 31, 2007
409
30
Wadau,
Kama mtakumbuka vizuri wakati wa kampeni na hata baaday ya uchaguzi kuna kitabu kilichapishwa nadhani na Prince Bagenda na nakala zake kuchapwa sana magazetini.Naam kitabu hiki kilitueleza matumaini mengi ambayo kwetu yalitafsiriwa kama mategemeo ya awamu ya nne.Kauli za kitabu hiki ziliendana kabisa na kauli mbie ya kasi mpya,nguvu mpya,ari mpya.Maisha bora kwa kila mtanzania.Na kwa upande mwingine zilipingana kabisa na kitabu cha mwisho cha mwalimu Nyerere ambacho alikiita "UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA"kitabu ambacho ni kidogo ila kama viongozi wetu wangekuwa wanakirejea sana basi hata mkuu wa kaya kwene uteuzi wake wa watendaji serikalini na baraza la mawaziri kingemsaidia.

Mimi kama mmoja wapo niliyeshawishika sana na tumaini lililorejea na matumaini tuliyoelezwa humo nilisubiri kwa hamu sana kuliona hilo tumaini. Hamu yangu ilizidi sana pale ambako maadhimisho ya siku 100 za mzee wa kaya ikulu yalipoadhimishwa na kutumia siku hii kueleza mipango mikakati mingi ya awamu ya nne,na ile itakayoanza kutekelezwa hivi punde(wakati huo).Kusema kweli chachu hiyo ilizidi kukolea pale ambapo mkuu wa kaya aliunda tume ya kuchunguza mauaji ya wafanyabiashara wa mahenge na mara tu baada ya tume kumaliza kazi yake mkuu wa kaya akatoa maamuzi. Kwa kweli nilisema kwa kasi hii basi tutafika mbali.Maamuzi haya na mengine ambayo nilikuja kugundua ni ya kasi tu pale ambapo yaligusa non-mtandao au antimtandao yalitupa matumaini watanzania wengi. Lakini taratibu kasi hiyo nikaona kwa tathmini yangu inaanza kulegea kama vile gari lililokuwa kwenye spidi kali halafu ghafla horse pipe ikakatika.

Toka hapo sijamwona Bagenda tena akitutolea tathmini wala magazeti ambayo nayo kwa wakati huo fasihi simulzi ilikuwa juu ya kasi mpya. Taratibu magazeti yakaanza kubadili mwelekeo toka kuwa kasi mpya hadi kuwa sumu kwa uongozi.Hii ilinikumbusha sana jinsi kampeni za kibaki zilivyokuwa miaka ile na ambavyo NGos,magazeti na wanharakati wengine walivyokuwa wanamkampenia na kuwa na matumaini makuwa sana na kibaki lakini baadaye hayo hayo yakaja kuandika kitabu kiitwacho "NEVER AGAIN".Je,watanzania mnataka kunisadikisha kuwa na sisi au ninyi mmeanza kuandika page za mwisho za kitabu hicho cha never again.

Binafsi japo mtatofautiana sana na mimi na hilo nalitegemea kwa kuwa najua jf ni uwanja wa hoja,and lawyers say "we must agree to disagree" naamini kuwa serikali ya mkapa japo tulikuja kugundua baadaye kulikuwa na mafisadi na ufisadi mkubwa bado ilileta matumaini makubwa kwa watanzania kuliko ya sasa. Kwani pamoja na kula walikokula bado waiweza kutekeleza ule msemo wa wazungu kwamba "you are eating and we are eating tu" ambapo mwanamuziki mmoja hapa nchini aliwahi kupiga wimbo unaofanana na kauli hiyo usemao "Na sisi huku tupate ae aeeeeee".

Ni kipindi cha Ben ambacho tulishuhudia kukua kwa sekta ya mawasiliano, barabara nyingi kujengwa pamoja mikakati kama MMEM,ulipaji madeni nk.mishahara mingi ilokuwa duni wakati huo ilipanda wakati wa ben licha ya serikali yake kukumbwa na balaa nyingi anapoanza uongozi ikiwamo EL Nino, mv bukoba,kivuko cha kilombero nk. Lakini serikali ya mkuu wa kaya imekubwa na mambo mawili tu,Kukauka kwa mabwawa ya umeme na labda mfumuko wa bei. Hata hivyo nikiangalia mipango yote karibu 60% ya miradi inayotekelezwa au iliyotekelezwa bado ni programu zilizokuwa hazijaisha,zinatekelezwa au zinamaliziwa kutekelezwa na serikali ya awamu ya tatu. Mfano mzuri ni barabara bahati nzuri nilifanikiwa kufanya utafiti kuhusu miradi ya barabara na bomoa bomoa kule TANROADS NA Kwingineko nikaiona hiyo mipango kuwa barabara fulani itajengwa lini na kwa kiwango gani na pesa itatoka wapi.

Cha kushangaza sasa mimi sioni mabadiliko tuliyoyategemea zaidi ya ahadi. Ahadi bado ni nyingi na kasi ya utekelezaji wake ni kama 0.05% na hii inanifanya nimtafute Bagenda na kumuuliza kulikoni?miaka inazidi kukimbia wakati kasi inazidi kupungua. Katika matumaini yote tulokuwa nayo bado utekelezaji wake hata 20% haujafikia,sasa leo ni miaka mitatu wasiwasi wangu ni kuwa utekelezaji wake unaweza usifike hata nusu. Je, Mhe.Bagenda unatunga kitabu kingine?je,wadau wenzangu tumaini lililorejea bado lipo au niamini vingine.niendelee kuvuta subira?au litarejea awamu ya pili ya uongozi wa mkuu wa kaya?
 
Bagenda hasisiki tena sijui aliingia mlango wa nyuma wa nyumba ya mafisadi?
Kasi yake kisiasa imeporomoka sana. Hata huko kwao Muleba alikokuwa akigombea ubunge mara kwa mara kawaacha solemba. Hawajapata mbadala na hivyo wanarudisha mshirika wa mafisadi katika kila chaaguzi siku hizi.
Nadhani ajitokeze atuambie nini kimejili.
 
Watu wanaotushawishi sana kueleleka upande fulani wanatakiwa wasituache njiani waendelee kutuaminisha au kukanusha waliyosema
 
Na mimi nitatunga changu kitaitwa TUMAINI LILILOPOTEA
 
Wadau,
Kama mtakumbuka vizuri wakati wa kampeni na hata baada ya uchaguzi kuna kitabu kilichapishwa nadhani na Prince Bagenda na nakala zake kuchapwa sana magazetini.

Mkuu hapa mbele yangu nina nakala ya kitabu hicho. Kwenye sehemu ya 'Shukrani' mwandishi anatueleza kuwa kitabu hiki ni toleo la kwanza. Hivyo pengine hivi sasa mwandishi anaandika toleo la pili.

Miongoni mwa watu ambao mwandishi anadai anathamini sana ushauri wao na ambao hupata muda wa kurejea na kuchambua masuala ya kisiasa na kiuchumi mara kwa mara, kwa mujibu wa sehemu hii ya 'Shukrani', ni RA. Sijui mheshimiwa huyu anasaidiaje kulirejesha tumaini hili lililopotea.

Mwandishi pia anamnukuu mfadhili wa kitabu hiki, JS, anapotoa onyo kwa JK kwamba ndani ya timu yake kusiwepo na watu mfano wa akina OK, yaani ambao "wanakuwa na tamaa zao na siyo kuhudumia kama wanavyotamka". Sina hakika kama muungwana alisoma kipengele hiki.
 
Alaaa! kumbe mshauri wake ndiyo huyo ambaye watanzania wamepoteza imani naye?sikujua hilo mmh labda tusubiri second edition kwa kweli.
 
Alaaa! kumbe mshauri wake ndiyo huyo ambaye watanzania wamepoteza imani naye?sikujua hilo mmh labda tusubiri second edition kwa kweli.
Nasikia Bagenda ndiye mhariri mkuu/mkurugenzi wa gazeti la Karamagi. Ameshaamua kula sahani moja na mafisadi.
 
Nasikia Bagenda ndiye mhariri mkuu/mkurugenzi wa gazeti la Karamagi. Ameshaamua kula sahani moja na mafisadi.

Jasu una maana gani? Maana ya 'kula sahani moja' na mtu ninayoielewa mimi ni 'kumshughulikia' mtu huyo! In maana 'Mtoto Mfalme' ameingia jikoni kwenye hizo sahani ili awashughulikie mafisadi ndani kwa ndani? Hivi ni gazeti gani hilo? Na taarifa hizi umezitoa wapi? Hebu tafadhali weka hapa kipande cha nakala ya hilo gazeti kinachoonyesha bodi ya wahariri wake! Kazi kweli kweli!
 
wakutapatapa hao akina bagenda sio lolote kwenye siasa. wanatafuta kutuliza tumbo zao.
TUMSAIDIA AJITAMBUE KWAMBA TAIFA HALIPENDI KUYUMBISHWA KWA TAMAA ZA WACHACHE.
 
Bagenda alidanganywa na Salva Rweyemamu kuwa akijikomba kwa Kikwete na akafanikiwa kuchaguliwa kuwa rais angemteua balozi nchini kwao Uganda asijue jamaa yake naye ni tapeli mwenzake. Ilikuwa kama jamaa wa Magomeni waliouziana dhahabu feki kwa kulipana fedha feki. Bagenda mwandishi aliyekuwa akiheshimika na kuaminika alijivua nguo na kubakia kama changu akiogopa hata kujitokeza tena na kurejesha jina lake. Aliishia kama mtu aliyebakwa na kuondolewa bikra yake. Atairudishaje? Kwa sasa Bagenda ni mojawapo wa watu wanaomchukia Kikwete kuliko hata kale kagonjwa ka kwao. You know what? Alidhani ashomile kumbe bure kabisa. He is now screwed up waiting for Godot. When will he be appointed an ambassador? Tell it to the birds.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom