Yuko wapi Pius Lugangila aliyeshiriki mapinduzi ya kujaribu kumpindua JK Nyerere?

mtu bati

Senior Member
Mar 29, 2021
117
128
Inaelezwa kwamba Pamoja na hayati luten mstaafu Zacharia Hans pope na wengine, kulikuwa na commando mmoja aliyeshiriki jaribio la mapinduzi lakin hakukamatwa alotoroka. Anaenda kwa jina la Pius Lugangila. Wenzake walikamatwa lakin yeye alitokomea. Yuko wapi huyu kamanda?
 
Ni Pius Lukagingira siyo Lugangila,Nakumbuka gazeti la RAI,kulikuwa na muendelezo wa masimulizi ya jalibio hilo,Kapteni MAGANGA nae alifungwa alikuwa anaelezea tukio zima mpaka kufungwa kwao,Lukagingira alitolokea Uingereza na kufia huko.
 
Nshomile huyo kutoka Kamachumu-Muleba-Kagera. Alifia UK akaacha vijana wake wawili wa kiume huko UK. Kinachofurahisha juu ya hao vijana ni kwamba wanaongea lugha mbili kwa ufasaha mkubwa kabisa Kihaya na Kiingereza. Marehemu Chrisostom Rweyemamu aliyewahi kuwa DC enzi za JK aliwafanyia mahojiano huko UK 2009 na anasema mahojiano hayo yaliendeshwa kwa lugha yao ya asili na alikiri walikuwa wananaimudu kuliko yeye mwenyewe. Usabihi wa jina ni Lugangila.
 
Alitoroka akiwa gereza la ukonga. Akatimua mbio mpaka uingereza bila kukamatwa. Kumbuka wakati huo Rais ni Nyerere makaburu wanatolewa nishai kila wakijaribu kuhujumu taifa. Chekechea tu ndiye anaweza kuamini hii hadithi ambayo ni identical twin na ile ya utekaji wa ndege ilioishia hukohuko uingereza.
 
Pius Mutakubwa Lugangira aka Father Tom au Uncle Tom ndio alikua mastermind and pay master wa ule mpango

Yeye ndio alitakiwa kua mstakiwa namba moja kama angefikishwa mahakamani na sio Hatibu Ghandhi au Hatty McGhee kama alivyokua anajulikana

Namimi hua najiuliza iliwezekana vipi kwa jamaa kutoroka kutoka gereza la Ukonga kwa kutumia chopper! Mimi hadi leo akili yangu inagoma kukubali kua tukio lile eti lilipangwa watu wa kawaida wasiokua na mafungano na vyombo nyeti vya dola
 
Back
Top Bottom