Yuko wapi kijana mtanashati January Makamba?

kinguo

JF-Expert Member
May 27, 2016
440
314
Wakuu poleni na majukukumu ya kulizungusha tairi la maendeleo.

Nakuja mbele yenu nikitaka kujua huyu kijana mwenzetu kwenye siasa za nchi hii.

Maana amekuwa kimya sana hata zile twit zake hatuzioni kwa kasi hii ya mzee wetu kipenzi hapa kasi tu. Ni kipi kimemsibu na kuwa kimya hivi.

Ukichukulia wizara anayoongoza bado inachangamoto sana. Si mwingine ni Januari Makamba. Hata kwenye mkutano wa juzi huko Dodoma hata picha magazetini au kwenye TV station akifanya mahojiano.

Maana tulizoea kumuona hasa wakati wa jk au wakati tukielekea kwenye uchaguzi alikua hakauki kwenye media nini kimempata kijana wetu.

Naomba kuwasilisha.
 
Kwani hata wale walioanza uwaziri kwa mbwembwe na kusimamisha watumishi kila uchao unawasikia tena, aah natania tu.Ila dhamira ya KWELI ya Hapa Kazi Tu anayo muasisi wa hii kauli mbiu tu na sisi akina Yohana lakini kule juu mhh mhh
 
Mbona anaonekana mkuu sema siyo sana hata siku kabla ya mkutano nilimuona taarifa ya habari ITV na wanaccm wenzake wakiongelea maswala yao ya chama
 
February marope akicheza vibaya na Ngosha anaisha kisiasa! Hana mizizi ya maana kwenye chama lakini na muona kama ana kiburi fulani hivi! Ngosha sio kwamba anahangaikia na wapinzani wake wa nje pia anamonitor nyendo za wapinzani wake ndani ya chama! Nadhani anajua ndio maana hata wizara aliyopewa sio ya kumfanya asikike sana! Akili kichwani
 
Labda uwaziri alipewa kwa memo.
 
Kashauriawa na Kina Mzee Warioba apunguze Public attention kwa kuwa ana Adui wengi
 
miezi michache hivi wameishiwa namna hii, je mwaka ukiisha itakuwaje. lakini vile vile msisahau kuisoma namba
Hivi walishapewea 'instrument' za kufanyia kazi? Kuna kanuni flani hivi wanatakiwa kupewa kudhibitisha kuwa ni 'mawaziri wenye meno'. Wanapewa kanuni hizo na mkuu wa kaya.
 
Wakuu poleni na majukukumu ya kulizungusha tairi la maendeleo.

Nakuja mbele yenu nikitaka kujua huyu kijana mwenzetu kwenye siasa za nchi hii.

Maana amekuwa kimya sana hata zile twit zake hatuzioni kwa kasi hii ya mzee wetu kipenzi hapa kasi tu. Ni kipi kimemsibu na kuwa kimya hivi.

Ukichukulia wizara anayoongoza bado inachangamoto sana. Si mwingine ni Januari Makamba. Hata kwenye mkutano wa juzi huko Dodoma hata picha magazetini au kwenye TV station akifanya mahojiano.

Maana tulizoea kumuona hasa wakati wa jk au wakati tukielekea kwenye uchaguzi alikua hakauki kwenye media nini kimempata kijana wetu.

Naomba kuwasilisha.

Unapaswa kujua Msemo Maarufu usemao "Kila Nabii na Enzi zake"
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Hali ipo hivi sasa hivi

1469459708966.jpg
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom