Yuko wapi Josheph Shamba (Vengu)?

Mnisamehe tu sio wote tunaweza kuwasilisha mawazo yetu kwa kuandika
wasalaam
 
Mwaka 2013 nilikuwa taasisi fulani ya utafiti na tulikuwa na kaka yake ambaye alikuwa dereva wetu pale, ndiye aliyekuwa akiishi na Joseph Kigamboni na ndiye alikuwa akipambana na matibabu yake........kwa maelezo yake kwenye kundi lao la ze comedy ni Joti na Masanja pekee ndiyo waliokuwa wakienda kumuona.......na kipindi kile Mizengo Pinda ndiye alikuwa msaada mkubwa sana wakati ni PM,maana chakula alichokuwa anakula kwa siku ilikuwa kama elf 30 (special meal).

Ila jambo kubwa lililokuwa linaelezwa nikwamba ni issue ya ushirikina ndani ya kundi lao.........

Duu wamempiga kipapai mwenzao halafu wakaokoka!
 
Jamaa alikuwa class mate wangu huko mbozi mission kabla ajaanza kuugua nakumbuka nikitoka church maeneo ya mabibo aliinita akataka kuninulia hadi kilaji nilikuwa mda huo situmii hiyo kitu nilimshukuru tukaagana tukipeana ahadi ya kuonana tena, Mara siku si nyingi nikasikia taarifa zake za kuumwa nilijaribu kuwacheki hao wasanii wenzie kwenye mitandao yao ya kijamii nipate kujua yuko wapi nikamjulie Hali lakini sijawahi pata ushirikiano. Naimani uko aliko anaendelea vizuri namuombea kwa Mungu awe mzima kama zamani aje kuendeleza harakati zake alikuwa anafit Sana kumuigiza Mueshimiwa Mrema
 
Hivi kwanini hawasemi mahali aliko wala afya yake?
 
Salaam sana wanajamvi,

Nimeona taarifa kupitia TvE Tanzania leo asubui alikua anahojiwa mshiriki mwenza katika kipindi cha ucheshi kilichobamba kitambo kidogo ze comedy mpaka orijino komedi Mpoki akisema kwamba Bw. Joseph shamba maarufu kama Vengu ambaye tuliaminishwa amepoteza maisha kwa maradhi yalokua yakimsumbua

Je, Vengu anaishi kweli na kipi kinasababisha aishi maisha ya kivuli au kuna nafasi nyeti anaitumikia kwa sasa?

Karibuni wenye taarifa zaidi

Ana tatizo la kwenye ubongo ambalo hawezi kurudi Katika hali ya kawaida tena Katika maisha yake. Ila ni mambo ya kifamilia hayo.Hata Muhimbili waliligundua hilo na hata kwenda India ilikuwa haina maana kwasababu ni tatizo ambalo ukipata halina tiba zaidi ya palliative care tu.

Alipelekwa tu India na Serikali kwasababu wakati ule kundi lilikuwa maarufu na ilionekana kama viongozi wanapelekwa India why not Wasanii lakini kitaalam walikuwa wanaojua nothing new will be detected or diagnosed.

Yuko Kigamboni kwa Babu na baadhi ya ndugu zake wakimpa msaada pamoja kundi lao la OK likiongozwa na Masanja Mkandamizaji.

Ila inasikitisha sana.
 
Hili swali hata mimi linanipa wakati mgumu Sana sema kina salama jabir na wengine wanaondesha vipindi vya kuhoji Hawa wasanii siku wakimuhoji mmoja wa Hawa original comedy watusaidie kuuliza hili
Tafuta mahojiano ya salama jabiri na joti yapo mtandaoni na ni ya mwaka huu huu tu
 
Back
Top Bottom