Yuko wapi Dr Hilman Ngunangwa?

Mnyamahodzo

JF-Expert Member
May 23, 2008
1,932
985
Ni msomi wa masuala ya Uongozi,hata kuwa na Phd ya ukweli/jasho, Dr Hilman Ndembelwa Ngunangwa. Ambaye alikuwa Mhadhiri ktk Chuo cha MANTEP, Bagamoyo hadi 1990 alipogombea na kushinda nafasi ya ubunge Jimbo la Njombe-Kusini.

Kabla ya kushindwa kwa kuchakachuliwa na CCM+Anne Makinda 1995, itakumbukwa kuwa akiwa Bungeni, yeye alikuwa ni miongoni mwa wale Wabunge 55 walioitaka serikali ya Tanganyika irudishwe. Wabunge wengine walikuwa ni Njeru Kasaka na Pius Msekwa.

Hadi sasa huyu Dr Ngunangwa sifahamu yuko wapi na anafanya nini. Kwa mwenye taarifa atujuze.

NOTE: Lakini twaweza jadili nafasi ya wabunge wa G55 katika kurejeshwa kwa Serikali ya Tanganyika.
Dr Ngunangwa aliandika kitabu cha BINGWA wa MKAKATI ULI0KUFA KABLA ya KUANZA.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom