Yu wapi Prof. Paramagamba Kabudi?

We Know Next

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
814
380
Wana Jamvi, suala la muswada wa katiba, limefika patamu, kwa pumba kujulikana pumba na mchele kujulikana mchele. Nakumbuka kabla ya hoja hii kufikishwa Bungeni Prof. Paramagamba Kabudi, alipelekwa pale dodoma kuwapiga msasa wabunge kuhusu hili hasa akiwa na mlengo wa Ki CCM zaidi. sasa mambo yameback fire, nina hamu ya kumsikia atasema nini kwa hili sasa. Kabudi funguka tukusikie..... maana umeshikwa uchawi...
 
Maprof wengine bwana...wanapiga kelele kwa kupindisha ukweli na mate yakiwatoka utafikiri kweli kumbe njaa tu. Jamaa alipinga mgombea binafsi mahakamani baada ya kuhudhuria mkutano wa NEC ya magamba....akapata chake mfukoni sasa na hapa lipewa night allowance akabomoka upupu wake...****** kaona mbali zaidi ya magamba na maprof wao sasa wanaweweseka
 
Kabudi akikutana na Slaa na Baregu lazima akimbie. I wish na Prof. wa ukweli Shivji naye awe included kwenye hiyo tume
 
Nafikiri swala la Prof. mtani wangu Kabudi lilijadiliwa hapa na kutolewa ufasaha wa wazi kabisa.

Mahakama haiwezi kulilalizimisha BUNGE kubadili katiba. Sisi Mi-Tanzania yenye WIVU WA KIKE ndiyo tunaweza kuwachagua wabunge ambao wakienda Bungeni wataweza kubadili katiba.

Inabidi kuelewa mgawanyo wa hiyo mihimili mitatu. Mahakama inaweza tu kuionyesha Serikali/bunge kuwa hili Swala linavunja haki ya binadamu na katiba inabidi ibadilishwe. Bunge linasema ndiyo tutabadili (Wanaliweka kwenye ajenda za baadaye ambazo zinaweza kuchukua hata miaka 50).

Ndiyo maana wananchi walivyoanza kukomalia KATIBA MPYA, mchakato ukaanza. B

Badala ya kulia na Kabudi ambaye alisema ukweli kabisa (hata mie mwanzo nilimlaani) basi tuanze kulia na WABUNGE WA CCM.
 
Sikonge umesema saw a Kabisa, tatizo KUBWA la sisi wadanganyika tuna soma magazeti NDIYO tunachangia, badala ya kwenda kutafuta judgment NA kuona argument zilizotolewa, mwacheni Prof afundishe
 
Kati ya wasomi ninaowaona ni amnazo ni Dr. Bana na Prof Kabudi.

Kabud kwenye kesi ya Mch. Mtikila kuhusu mgombea binafsi mahakama ilimuita akapinga mgombea binafsi. Huyu huyu alitumiwa na bunge kuhalalisha muswada wa katiba.

Hapa JF waliwai kuweka matokeo yake ya chuo kikuu. Alionekana mwenye akili sana ila kwa hili ni bogus. Dr Bana na reet ni aibu tupu.

Hawa wakikutana pamoja na Dr. Slaa, Prof Baregu na Nshara Lugemeleza lazima wakimbie.
 
Kati ya wasomi ninaowaona ni amnazo ni dr bana na prof kabudi. Kabud kwenye kesi ya mtikira kuhusu mgombea binafsi mahakama ilimuita akapinga mgombea binafsi.huyu huyu alitumiwa na bunge kuaralisha mswada wa katiba.apa jf waliwai kuweka matokeo yake ya chuo kikuu. Alionekana mwenye akili sana ila kwa hili ni bogus.dr bana na reet ni aibu tupu. Hawa wakikutana pamoja na dr slaa,prof baregu na nshara lugemeleza lazma wakimbie.

Mdau Mbona lugha yako inaonekana haina weledi?
 
Anatafakari ajali ya kimchakato iliyomkuta...alidhani JK atampa zawadi ya u-VC baada ya Mukandala kumaliza muda na kuwapo kwa tetesi kwamba ataenda kuwa balozi Europe...jamaa kaongezwa muda, yeye kaachwa kando...
 
masikini we prof paramagamba kabudi....another typical example of wasomi walioamua kuweka usomi pembeni na kuwa mashahidi wa uwongo....

atashindana wapi na tambwe hiza aliyekulia mtaani?

kwenda shule kusoma na kutokuelimika nako ni GAMBA...hili huhitaji maombi na kufunga kulitoa!
 
Wana Jamvi, suala la muswada wa katiba, limefika patamu, kwa pumba kujulikana pumba na mchele kujulikana mchele. Nakumbuka kabla ya hoja hii kufikishwa Bungeni Prof. Paramagamba Kabudi, alipelekwa pale dodoma kuwapiga msasa wabunge kuhusu hili hasa akiwa na mlengo wa Ki CCM zaidi. sasa mambo yameback fire, nina hamu ya kumsikia atasema nini kwa hili sasa. Kabudi funguka tukusikie..... maana umeshikwa uchawi...

Jamaa alijua atapewa uenyekiti wa kuchukua kura za maoni juu ya uundwaji wa akatiba mpya, bahati mbaya ******* yememshuka utadhani ana mshipa wa kitanga. Hovyo sana yule, ndo maana wanasiasa huona wasomi ni wajinga tu coz ya kuwa na watu kama huyu walioshindwa kutumia elimu zao kwa manufaa ya nchi
 
Kuna usemi unaosema majina huumba, Prof Paramagamba, Huyu Prof anaonekana ni mwanachama mtiifu wa Magamba
 
Jamaa alijua atapewa uenyekiti wa kuchukua kura za maoni juu ya uundwaji wa akatiba mpya, bahati mbaya ******* yememshuka utadhani ana mshipa wa kitanga. Hovyo sana yule, ndo maana wanasiasa huona wasomi ni wajinga tu coz ya kuwa na watu kama huyu walioshindwa kutumia elimu zao kwa manufaa ya nchi
Ndyoko umenena hawa ndo wanasababisha madr kutukanwa na wanasiasa Paramagamba Aidan Kabudi hovyo kabisa.
 
Tatizo la maprofesa wa vyuo vya kata(sorry vyou vya serikali)wana mawazo ya kichama sana.mfano ni yule dokta bana very stupid dokta.wanakariri tu.
 
Alivyokuwa anaongea mpaka povu linamtoka kumbe kakodiwa atetee maslahi ya watu,aibu kweli,nakumbuka walikuwa wanamtupia vijembe prof.issa shivji kutokana na mtazamo wake chanya juu ya katiba mpya,lakini leo mieezi michache baadae kimenuka,aibu sana wanataaluma wetu kujidhalilisha kwa sababu ya njaaa,dr.bana ndio kinyaaa analeta,kwanza hata hajitambui anaongea nini?kwa nani?na wakati gani?
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom