Kada wa CHADEMA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 289
- 615
Kuna watu wamekitumikia chama changu kwa jasho na damu. Walitumia muda mwingi kutafuta namna nzuri ya kukipaisha chama chetu kisiasa. Watu hao pia walifanya kila jitihada kuhakikisha kuwa wasaliti wote chamani wanashughulikiwa ikiwa ni pamoja na kuvuliwa vyeo na kufukuzwa uanachama. Miongoni mwa wahanga wa Kitengo cha Sera na Utafiti aka Majasusi wa chama ni pamoja na Zitto Kabwe, Mtela Mwampamba, Juliana Shonza, Habib Mchange na sasa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama, Wilfred Lwakatare.
Kitengo hiki kinafanya kazi kubwa ya kuwachonganisha wale ambao hawatakiwi chamani na wanachama wengine hasa kwa kutumia mbinu ya kuwafanya waonekane ni wasaliti na wanatumika na mahasimu wetu wa CCM. Kitengo hicho ambacho kwa kawaida husimamiwa na Mwenyekiti mwenyewe moja kwa moja, moja ya jukumu lake ni kuhakikisha kuwa Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe anaendelea kuwa maarufu na wengine wote watakaonyemelea nafasi hiyo wanazamishwa mapema kabla hawajaleta madhara kwa kiti.
Kwa jinsi mambo yanavyoenda sasa, inaonekana kabisa kitengo hiki kinayumba. Wafanyakazi wa kitengo hiki ama wamezidiwa nguvu ama hawawezeshwi ili wafanye kazi zao vizuri. Namuona Yeriko Nyerere jinsi anavyorukaruka as if hana pa kuelekea. Mkuu wa Kitengo hicho Ben Saanane ni zaidi ya miezi miwili sasa haonekani chamani na kwenye mitandao ya kijamii. Kulikoni?
Yapo madai kuwa kazi za akina Ben sasa zinafanywa na Vijana wa 4U MOVEMENT waliosalia baada ya kuchujwa. Lengo lao ni kuhakikisha kuwa Lowasa anakuwa juu zaidi ya Mbowe. Hili linaelekea kutimia kwani mpaka sasa, Mwenyekiti hana mamlaka makubwa chamani na nafasi hiyo inaenda kwa Lowasa? Je CHADEMA tunataka kutengeneza nafasi ya Ayatollah kama ilivyo kwa ACT?