Rufiji dam
JF-Expert Member
- Feb 20, 2020
- 3,803
- 8,786
Mkuu wa jiji la Dar es Salaam anatakiwa kupewa onyo anatakiwa akaripiwe. Huyu Makonda hana elimu ya afya. Makonda anatoa matamko hatarishi sana juu ya ugonjwa wa Korona.
Anakurupuka sana, analeta hofu. Anajenga hatari zaidi ya hatari yenyewe. Huyu afungwe speed gavana. Yupo wapi mganga mkuu wa jiji?
Nimemsikiliza Naibu Waziri wa Afya juu ya Barakoa ya kuwa leso haifai kabisa kuvaliwa kama Barakoa. Kitenge ama Khanga hazifai kuzibia pua zetu lakini Makonda kashauri zitumike Waziri Mkuu Majaliwa toa tamko.
Kuna kipindi alikusanya watu akitoa hotuba kwa vijana juu ya ugonjwa huu je hakujua kama mkusanyiko nao ni chanzo cha kukwaa gonjwa hili.
Barakoa inatakiwa kuvaliwa saa nne tu kisha unabadilisha sasa kwa bei ya Tshs. 3000 × 4= Tshs 12,000 kwa siku moja. Kwanini kusiwe na tamko la kulizima jiji la Dar es Salaam kwa wiki mbili!
Anakuja na hoja ya kufanya biashara kwa mfumo wa take away. Sijui anajua mfumo wa biashara upo vipi hasa kwa wachuuzi makasha ya kufungia bidhaa anajua yanauzwa kiasi gani? Huyu mtu anatakiwa kuonywa na kupewa elimu ya bure kuhusu madhara ya kukurupuka.
Msaada wa yule Mchina upo wapi, kwanini wanashindwa kusambaza masks bure kwa kila mkazi hasa wa jiji la Dar es Salaam kwa sababu uongozi wote wa serikali za kata na serikali za mitaa upo chini ya uongozi wa CCM.
MAKONDA AJARIBU KUWA NA UELEWA KATIKA MATAMKO YAKE HASA KIPINDI CHA UGONJWA HATARI. HII TAALUMA YA WATU SIO SIASA HIZI.