Yu wapi James Mapalala mwanzilishi wa CUF?

Huu mzozo aside,

Mapalala anasema Hamad Rashid Mohammed ni mtu muhimu sana katika CUF kwa sababu ndiye mtu pekee anayeweza kwenda kutafuta fedha nchi za nje kwa ajili ya chama (kuomba misaada) ?

Hawa ndio wanamapinduzi wetu jamani.

----
Ni kweli J. K. Mapalala alikuwa ni mmoja wapo katika waasisi wa CUF na inasemekana alifukuzwa uongozi Wa CUF baada ya kurubuniwa NA CCM ZNZ na ndio maana akaanzisha chama ndani ya chama.

Chama cha CUF kwa kawaida kadi zao za uanachama zinakuwa na viganja viwili vya mikono vinavyosalimiana na mizani wakati yeye alichapisha kadi ambazo zina tembo aliekanyaga mzani.

Sasa kama hizi habari zilikuwa za kweli mlitaka CUF wachukue hatua gani!!!? Waache chama kimoja kiwe NA kadi zenye nembo mbili tofauti na baadae chama kifutwe baada ya watu kutumia nafsi NA Mali zao kukianzisha!? Hilo haliwezekani.

Kuhusu Maalim kupenda hela hilo sio kweli maana sote ni mashahidi namna alivyokubali kupoteza uongozi NA uanachama ndani ya CCM wakati huo kwa lengo moja tu nalo ni kuitetea ZNZ NA watu wake.

Kuhusu Mapalala kuimarisha CUF wakati alipokuwa M/kiti hilo hakulifanya yeye peke yake!!!!??? Kama ni hivyo huu sasa ni zaidi ya mwaka wa7 mbona CHAUSTA hakijaimarika? Nadhani pamoja na propaganda mbali mbali inayofanywa JUU ya CUF, mfano fitina ya UDINI, UPEMBA NA UGAIDI WA MAHITA lakini bado CUF inajiuza yenyewe na ndio maana tokea kuasisiwa kwake pamoja na dharuba mbali mbali lakini bado imesimama wima!!!????

Viko wapi vyama vilivyokuwa na nguvu vya upinzani TZ!? Leo iko wapi NCCR mageuzi!???? Leo iko wapi TLP!??? Hata hiyo Chadema siku zake zinahisabika.

Jambo moja kubwa ambalo mimi hadi leo linanitoa MACHOZI ni kwa mzee Mapalala kukubali hadaa ya maira hadi kufikia kutoa RASILIMALI YAKE PEKEE tena kwa hela mbuzi!!!??? Sifikirii kama nyumba zake zilikuwa zinafikia thamani ya mil80! Lakini ile plot ni utajiri tosha ambao maskini huy umemtoka

NA sijui kwanini hakurudisha nyuma moyo wake na akamfuata Maalim amsaidie kwa chochote ili aokoe plot yake!? Ninavyomjua Maalim nilazima angalifanya bidii kubwa kuinusuru plot ya Mzee Mapalala maana Maalim ni MTU ambae haweki visasi na ni mwepesi wa kusamehe.

Kwa Maalim SIASA si uadui na ndio maana hutamkuta kwenye jukwaa akihubiri chuki wala kutukana watu!!!??? Matusi yote na madhila aliyofanyiwa na Salmin Amour baadae Amani Karume lakini alisamehe na kukubali kukaa nao chini na kupatana nao
 
Hawawezi kuzungumza nje ya box la misaada kwani ndiko haswaa wanakolenga! wanasiasa wengine bwana.
 
Mapalala hana uhakika wa maneno anayosema. Hawa wote wanataka kumuangusha Maalim Seif wakitumiwa na CCM lakini wamekuta Maalim amekita pazuri tu. Si rahisi kumuondoa Maalim Seif wakati huu ambapo yeye amejitahidi kuleta amani zanzibar na maendeleo yanaonekana. Ni mchezo mdogo huu. Na kwanini iwe ni ajabu wakati kila leo CCM, NCCR na CHADEMA wanawafukuza watu wao kila siku.
 
na bendera za cuf zinaanza kushushwa toka matawi yao dar. Genge la maalim lina kazi
 
CUF wamefanikiwa kumpoteza James Mapalala ila Mzimu wake utawasaka. Huyu ndo mwanzilish wa CUF mwaka 1992.na alishapata kamatwa kwa kuanzisha CUF serikali ikidai hakikuwa halal.baadaye alikuja kuunganisha na kamati ya mabadiliko ya kisiasa au KAMAHURU (the committee for political changes) kikiwa na S.Mloo na Seif Sharrif akaja kuwa makamu mwenyekiti. James Mapalala hakujua S.S Hamad alikuwa nyoka mwenye uchu wa madaraka kwa nguvu zote. Prof Lipumba na Seif Hamad wakamfanyia HILA na kumwondoa kumweka Prof Lipumba.Leo hatumsikii na CUF hawatak hata kumkumbuka kama mwanzilish wa chama. Julius Mtatiro yaliyomkuta kibeku na ungo pia yatamkuta. Seif Hamad si mtu wa kumwamin ana ajenda zake binafs.anawezana na Prof Lipumba ambaye kisiasa hana mwelekeo anaburuzwa tu. Hiki ndo chama cha wananchi CUF. Mzimu wa James Mapalala hautawaacha salama. Mtakumbuka maneno haya kwa uhuni mliomfanyia.
 
Historia inatushuhudia kuwa chama cha wanachi CUF kilianzishwa mwaka 1993 kutokana na muungano wa vyama viwili; Zanzibar United Front (ZUF) toka Zanzibar na Chama Cha Wananchi Tanzania (CCWT) toka Bara. Viongozi wa kwanza kabisa wa kitaifa wa CUF walikuwa ni James Mapalala (mwenyekiti taifa),makamu mwenyekiti alikuwa ni Maalim Seif Sharif Hamad na katibu mkuu alikuwa ni Shaaban Mloo. Lakini inaonekana baadaye James Mapalala alifukuzwa CUF. Kwanini mwenyekiti huyu wa kwanza wa CUF taifa alifukuzwa?
 
Kwani Mapalala Mpemba.

Mwanzilishi huku alikuwa James Mapalala, akadanganywa akajiunga na akina Mloo wa KAMAHURU. Kisha wakamfukuzilia mbali Mapalala kwa (misingi ya udini) na ndipo akapachikwa Lipumba.

CUF wanapindisha historia.

Unaweza kufafanua vizuri hapa tafadhali?....ili tuelewe vizuri
 
Ni kweli J. K. Mapalala alikuwa ni mmoja wapo katika waasisi wa CUF na inasemekana alifukuzwa uongozi Wa CUF baada ya kurubuniwa NA CCM ZNZ na ndio maana akaanzisha chama ndani ya chama.

Chama cha CUF kwa kawaida kadi zao za uanachama zinakuwa na viganja viwili vya mikono vinavyosalimiana na mizani wakati yeye alichapisha kadi ambazo zina tembo aliekanyaga mzani.

Sasa kama hizi habari zilikuwa za kweli mlitaka CUF wachukue hatua gani!!!???? Waache chama kimoja kiwe NA kadi zenye nembo mbili tofauti na baadae chama kifutwe baada ya watu kutumia nafsi NA Mali zao kukianzisha!? Hilo haliwezekani.

Kuhusu Maalim kupenda hela hilo sio kweli maana sote ni mashahidi namna alivyokubali kupoteza uongozi NA uanachama ndani ya CCM wakati huo kwa lengo moja tu nalo ni kuitetea ZNZ NA watu wake.

Kuhusu Mapalala kuimarisha CUF wakati alipokuwa M/kiti hilo hakulifanya yeye peke yake!!!!??? Kama ni hivyo huu sasa ni zaidi ya mwaka wa7 mbona CHAUSTA hakijaimarika? Nadhani pamoja na propaganda mbali mbali inayofanywa JUU ya CUF, mfano fitina ya UDINI, UPEMBA NA UGAIDI WA MAHITA lakini bado CUF inajiuza yenyewe na ndio maana tokea kuasisiwa kwake pamoja na dharuba mbali mbali lakini bado imesimama wima!!!????

Viko wapi vyama vilivyokuwa na nguvu vya upinzani TZ!? Leo iko wapi NCCR mageuzi!???? Leo iko wapi TLP!??? Hata hiyo Chadema siku zake zinahisabika.

Jambo moja kubwa ambalo mimi hadi leo linanitoa MACHOZI ni kwa mzee Mapalala kukubali hadaa ya maira hadi kufikia kutoa RASILIMALI YAKE PEKEE tena kwa hela mbuzi!!!??? Sifikirii kama nyumba zake zilikuwa zinafikia thamani ya mil80! Lakini ile plot ni utajiri tosha ambao maskini huy umemtoka

NA sijui kwanini hakurudisha nyuma moyo wake na akamfuata Maalim amsaidie kwa chochote ili aokoe plot yake!? Ninavyomjua Maalim nilazima angalifanya bidii kubwa kuinusuru plot ya Mzee Mapalala maana Maalim ni MTU ambae haweki visasi na ni mwepesi wa kusamehe.

Kwa Maalim SIASA si uadui na ndio maana hutamkuta kwenye jukwaa akihubiri chuki wala kutukana watu!!!??? Matusi yote na madhila aliyofanyiwa na Salmin Amour baadae Amani Karume lakini alisamehe na kukubali kukaa nao chini na kupatana nao
 
Mwanzilishi huku alikuwa James Mapalala, akadanganywa akajiunga na akina Mloo wa KAMAHURU. Kisha wakamfukuzilia mbali Mapalala kwa (misingi ya udini) na ndipo akapachikwa Lipumba.

CUF wanapindisha historia.

acha kupotosha ! Huyu alitimuliwa kwenye kikao TANGA , BAADA YA KUNUNULIWA NA KUWASALITI WENZIE , ni msaliti MKONGWE , JAPO SIKU HIZI KUNA WASALITI VIJANA !
 
Mzee Mapalala juzi nilikutana nae internet cafe Ips posta, mzee kachoka kimwili nadhani uzee na majuto ya usaliti vinamsumbua sana,
 
Mzee Mapalala ni ofisa wa usalama wa taifa, alikuwa na task ile ya mwanzo ya kuanzisha vyama hewa kuwarubuni jumuiya ya kimataifa na baadaye yeye mwenyewe alishiriki kuvivuruga.
 
Pumzika kwa katika Udongo mzuri James Kabelo Mapalala heri, amani na raha ya Milele iwe nawe!
 
Back
Top Bottom