Yu wapi James Mapalala mwanzilishi wa CUF?

BASIASI

JF-Expert Member
Sep 20, 2010
9,733
5,006
Jamani kuna huyu mzee mwanzilishi wa CUF aliishia wapi jamani...? Mwenye kuwa nae karibu msalimieni sana sana.

Nadhani siasa ameachana nayo
 
Hao akina Mapalala wapo wengi sana, kama unamkumbuka Wakatwalwe, Tambwe Hiza, Shaibu Akwikombe, Leluu Jidawi na juzi Juma Usmani na Bi Mafunda, haijulikani hata wanaishia wapi.
 
Aaah nilimuona last 2 month pale Morocco anatembea tembea tu kama muuza mchicha
 
Thursday, 14 October 2010

A veteran politician, Mr James Mapalala, is living besides his cowshed after his two residential houses were auctioned and demolished, it has been learnt.

Reports say the houses situated at plot number 403 on Ursino North Street along Morocco Road in the city, were demolished early this week by a court broker.


Mr Mapalala, according to reports, guaranteed his friend, Mr Moses Maira, to borrow $12,000 from the city bank, Savings Finances, but the man could not pay back the loan before he met his death last year.


The veteran politician, who chairs Chama cha Haki na Usawa (Chausta), confirmed yesterday that the Sh80 million worth of residential houses and a plot valued at Sh1.5 billion were all sold at only Sh100 million.


The houses were demolished on Monday afternoon when he went to court to file his petition against a High Court order to demolish the houses.


"The High Court ruled out on Tuesday last week that my residential houses be demolished and the order was implemented on Monday," he said, explaining that he had since been living in a room of a house helper he hired for graze his cows.


He admitted that he was a guarantor of his friend, the late Maira, who secured a $12,000 loan from the Savings Finances bank in 2003.


"The contract indicated that Maira was required to pay back the loan in a two months period, but failed to meet the deadline," he said, adding:


"The bank filed case number 79/2004 at the Kisutu Resident Magistrate's Court the following year, but it was later resolved that the case be dealt with outside the court."


The court had in 2008 ordered Mr Mapalala's residential houses be auctioned to recoup the loan after being informed that Maira had defaulted.


Mr Mapalala said he filed a case at the Land Tribunal, praying that Maira should bear the burden of the debt himself.


He argued that his property did not serve as bond to the bank contract, as Mr Maira issued his own residential house and a vehicle all valued at Sh172 million to that effect.
 
Mwasisi wa Mageuzi avunjiwa nyumba mbili

Thursday, 14 October 2010

MWANASIASA Mkongwe na mwasisi wa mfumo wa vyama vingi nchini James Mapalala anaishi katika mazingira magumu, kando ya zizi la ng'ombe baada ya nyumba zake mbili kupigwa mnada na kubomolewa.

Habari zimeeleza kuwa nyumba hizo zilizoko kwenye kitalu namba 403 mtaa wa Usino North, barabara ya Moroco, zilibomolewa juzi na dalali wa mahakama kutokana na mtu aliyemdhamini kuchukua mkopo wa dola 12, 000 benki, kushindwa kulipa.


Mapalala ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama cha Haki na Ustawi (CHAUSTA ), alilieleza gazeti hili jana kuwa nyumba hizo, zina thamani ya Sh80 milioni na kwamba eneo husika lina thamani ya Sh 1.5 bilioni, lakini zimeuzwa kwa Sh100milioni.


Alisema nyumba hizo, zilivunjwa Oktoba 11, mwaka huu majira ya mchana wakati yeye akiwa mahakamani kukata rufaa kwa ajili ya kupinga hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama kuu.


"Mahakama Kuu iliamua nyumba hiyo iuzwe ili kulipa deni hilo,Oktoba 5, mwaka huu na ilivunwa Oktoba 11, mwaka huu.



"Tangu siku hiyo nimelazimika kuishi kwenye chumba cha mfanyakazi wangu wa ng'ombe ambacho kipo zizini," alisema Mapalala.


Alikisimulia mkasa huo, alisema mwaka 2003, alimdhamini rafiki yake ambaye sasa ni marehemu, Mozes Maira kukopa kwa ajili ya kukopa Dola 12,000 kutoka benki ya Savings Finances ya jijini Dar es Salaam.


"Mkataba huo, ulionyesha kuwa mkopaji (Maira) anatakiwa alipe ndani ya miezi miwili, lakini alishindwa kuzilipa.



"Ilipofika mwaka 2004, benki ilifungua kesi namba 79/2004 katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, lakini baadaye kesi hiyo ilikuwa ikizungumzwa nje ya mahakama kwa makubaliano ya benki na mkopaji, lakini mwaka 2008 mahakama hiyo, ilitoa hati ya kuvunjwa kwa nyumba hiyo baada ya mkopaji kushindwa kulipa deni hilo," alisema Mapalala.


Alisema kutokana na hali hiyo, alifungua kesi Mahakama ya Ardhi kuomba deni hilo adaiwe mkopaji mwenyewe kwa sababu udhamini wake kwa Maira, haukuhusisha mali.


"Kesi nilifungua, lakini haikuweza kusikilizwa mapema. Baadaye nikaamua kukata rufaa mahakama Kuu,lakini sikufanikiwa baada ya mahakama hiyo, kunieleza nimechelewa kukata rufaa.


"Nilipoiomba mahakama inisikilize na mimi upande wangu, ilisisitiza kuwa madai yangu yamepitwa na wakati na uamuzi ulikuwa tayari umetolewa," alisema Mapalala.


Mapalala alisema Maira alifariki dunia mwaka 2009, na deni alilokuwa akidaiwa rafiki yake, liliamishiwa kwake .
 
Very sad story.

Hawa jamaa sijui kwa nini hawaheshimiwi.

Wapinzani wana wanasheria wazuri sana, kwa nini wasingemsaidia kutetea haki yake? Mi najua kuwa kila mkopaji lazima akate credit life insurance, ambapo ikitokea amekufa, mkopo wake unalipwa na bima.
 
Mwanzilishi huku alikuwa James Mapalala, akadanganywa akajiunga na akina Mloo wa KAMAHURU. Kisha wakamfukuzilia mbali Mapalala kwa (misingi ya udini) na ndipo akapachikwa Lipumba.

CUF wanapindisha historia.
 
Mwanzilishi huku alikuwa James Mapalala, akadanganywa akajiunga na akina Mloo wa KAMAHURU. Kisha wakamfukuzilia mbali Mapalala kwa (misingi ya udini) na ndipo akapachikwa Lipumba.

CUF wanapindisha historia.

So Unawarejesha CUF kivipi?
 
So Unawarejesha CUF kivipi?
Ninawarejesha wanaJF katika historia ya CUF. Cuf haikuasisiwa ili iwe kimelea cha CCM. CUF iliwafukuza kinyemela waasisi wake na leo tunaona inaanza kujichanganya. Hiki ni chama chenye viongozi waliojaa hila za kila aina. Wanachama wa CUF hasa kwa Tanganyika wanapaswa kufikiri tena na kujiunga na vyama makini.
 
Ninawarejesha wanaJF katika historia ya CUF. Cuf haikuasisiwa ili iwe kimelea cha CCM. CUF iliwafukuza kinyemela waasisi wake na leo tunaona inaanza kujichanganya. Hiki ni chama chenye viongozi waliojaa hila za kila aina. Wanachama wa CUF hasa kwa Tanganyika wanapaswa kufikiri tena na kujiunga na vyama makini.

Du sasa mkuu hiyo historia ni mistari miwili tuu?
 
Mwanzilishi huku alikuwa James Mapalala, akadanganywa akajiunga na akina Mloo wa KAMAHURU. Kisha wakamfukuzilia mbali Mapalala kwa (misingi ya udini) na ndipo akapachikwa Lipumba.

CUF wanapindisha historia.

Heading nzuri maneno yaliyomo ni pumba tupu !
 
Jf,

Jina James Mapalala ni kubwa sana, ni mmoja ya waasisi wa upinzani hapa Tanzania. kinachonisikitisha mimi hivi huyu mzee aliwakosea nini CUF? sina uhakika kwa sasa yupo wapi ila hali yake kiuchumi na kiafya si nzuri, juzi juzi tu nyumba yake ya hapa morroco ikapigwa mnada.

Je CUF hamna utaratibu wa kuwaenzi waasisi wenu? je alikosa nini ndani ya chama hadi mmsahau kiasi hiki? Wengine wanasema James aliuza chama kwa hisa zote 100% kwa kina Seif.

Ufafanuzi tafadhali.
 


na Asha Bani

MUASISI na Mwenyekiti wa kwanza wa Chama cha Wananchi (CUF), James Mapalala, alisema yanayotokea ndani ya chama hicho hayamshangazi kwa kuwa Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad alitumia watu ‘walevi’ kumfukuza ndani ya chama hicho mwaka 1994.


Akizungumza kwa njia ya simu na Tanzania Daima jana, Mapalala alisema Maalim Seif ni kiongozi anayewatumia baadhi ya wanachama wake kupata mafanikio, na kisha hutumia nguvu kuwafukuzwa kwa vitimbi kama alivyofanyiwa yeye na sasa Hamad Rashid Mohamed.

Alidai kuwa Maalim Seif aliwahi kumtumia yeye kama daraja mwaka 1992 kwa kuzunguka nchi nzima bara na Zanzibar, akilala vijijini kwa lengo la kukitangaza chama ili waweze kuwakomboa wananchi wanyonge lakini matokeo yake alimfukuza kwa visingizio mbalimbali ambavyo si vya kweli.


Mapalala alienda mbali zaidi na kueleza kuwa Maalim Seif si mtu wa kawaida hasa unapogusia masuala ya madaraka kwa kuwa ni mtu ambaye anapenda fedha na madaraka, huku akiyatumia vibaya kwa kuwakandamiza wanyonge.

“Hakuna mtu ndani ya CUF asiyejua kwamba Hamad Rashid alikuwa ni mtu muhimu sana ndani ya chama hicho kwani ndiye kiongozi wa pekee mwenye uwezo wa kutafuta fedha nje ya nchi kwa ajili ya kuendesha chama, lakini Maalim amemtimua kama ilivyokuwa kwangu baada ya kufanikiwa kupata mafanikio mbalimbali hadi kuwa Makamu wa Rais,” alisema Mapalala.


Mapalala alidai kuwa Maalim Seif anapenda kila atakalosema yeye ndilo litendwe na watu wote ndani ya chama bila kuzingatia maoni ya watu wengine hata kama si jambo zuri kwa maslahi ya chama.


Akizungumzia kufukuzwa kwake ndani ya chama, alisema kuwa mwaka 1994 katika mkutano uliyofanyika mkoani Tanga alitimuliwa bila kupewa sababu za msingi na kwamba waliofanya maamuzi katika mkutano huo hawakuwa wanachama halali na nakala za barua na majina yao anayo hadi sasa.


Aidha aliwaonya viongozi mbalimbali wa CUF kuwa wanapozungumzia matatizo yao ndani ya chama hasa katika kipindi hiki ambacho wamemfukuza Hamad wasitolee mfano jina lake kwa kuwa ana vielelezo vyote vya Maalim Seif na wenzake kutumia ‘walevi’ wa pombe ambao walihongwa huku wakiwa si wajumbe ili waweze kunifukuza.


“Tena sitaki kabisa wasijipe umaarufu kusafisha dhambi zao kwa kunitaja mimi. Katika mkutano ule wa Tanga waliokuwa wameitisha kwa ajili ya kunifukuza mimi, nilipewa barua masaa machache na kwamba mkutano ulifanyika usiku, wajumbe walikuwa si halali na vielelezo hadi sasa ninavyo wasitake niwaumbue,” alisema Mapalala.


Mapalala alisema Maalim Seif bila kujiingiza katika migogoro alitakiwa kuangalia hali ya wananchi wa Zanzibar hasa Pemba ambao tangu kuingia kwa serikali ya mseto mambo ndiyo yamezidi kuwa magumu zaidi.

“Sharif Hamad ni kiongozi ndani ya CCM ndio maana anashindwa kuwatetea wananchi, ameua chama; watu wanahoji anakuja juu, watu wanahoji matumizi ya fedha anakuja juu, ni mtu ambaye anapenda sana madaraka na hili ndilo tatizo kubwa ambalo linaua demokrasia ndani ya vyama hasahasa chama hicho,” alisema Mapalala.

Aidha alimshauri mbunge huyo wa Wawi kama ana nia ya kuwakomboa wananchi hasa wakazi wa Pemba basi aendelee kwa kuanzisha chama chake asirudi CCM kwa kuwa chama hicho ndicho kimeungana na Maalim Seif.


Mapalala ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Chausta amemkaribisha Hamad Rashid kujiunga nacho kwa vile anaamini ni kiongozi makini na mchapa kazi hodari

 
Back
Top Bottom