Yu wapi Dkt. Masumbuko Lamwai?

Bob_Dash

Member
Nov 1, 2010
90
13
F58A6CC5-4F07-442E-8FCA-46233FEFF758.jpeg

Jamani hivi huyu mwasheria aliyewahi kuwa Mbunge siku za nyuma nadhani kupitia NCCR kama sikosei, yuko wapi siku hizi?

Mbona hasikiki tena, nilisikia habari kuwa alijiengua kutoka NCCR na kujiunga na CCM, je ni kweli?
 
Amefulia.................................................................................................................................................................................................................................................. lakini kisiasa
 
huyu bwana alivyoingia upinzani alikipata cha moto. hatakaa asahau. alirudi ccm akapewa ubunge wa kuteuliwa
 
Kuna Ndugu yake Joseph Selanini (Chadema) ambaye ameingia Bungeni kwa kumuangusha Mramba kule Rombo. Huyu pia awali alikuwa NCCR.
 
Katika wanasheria walioingia kwenye siasa mimi namkubali aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA jaji mstaafu BOB MAKANI, jamaa ni noma!

nakumbuka wakati wa kesi ya uchaguzi CHADEMA vs CCM, mwaka 1995 kule Kigoma, jamaa aliwapelekesha puta majaji kinoma, hatimaye CHADEMA wakashinda ile kesi. Jamaa ana sauti nzito halafu anaongea kama anahasira halafu ana accent ya kisukuma hivi, du! ilikuwa burudani ya aina yake.
 
wote hamjui nyie......yupo manzese pale, kwenye kale kagorofa kake alichoshindwa kimalizia kwa miaaka kumi......lkn aliporudi ccm alikimaliza in a week............
ivi ulevi ameacha kweli.......coz nakumbuka alikuwa analewa mpaka anashindwa tembea
 
Naona pamoja na kuwa chama cha mafisadi wanambana kweli, wamemgaia Eskudo wakati wao wakiendesha ma-vogue...!
 
Aliingia kwenye mtego wa thithiem baada ya kuichachafya sana akiwa ENISISIARA ya enzi ambayo ilikuwa moto wa kuotea mbali. Thithiem walimpatia ubunge akalamba posho kwa miaka mitano baada ya hapo wakamtupa. Baada ya hapo sielewi aliekea wapi.
 
Mwaka 1994 akiwa NCCR Mageuzi tulimchagua kuwa Diwani kata ya Manzese, na hapo ndipo alianza kujulikana zaidi mitaani. Mwaka 1995 akiwa aligombea ubunge jimbo la Ubungo na alikuwa ameshinda pamoja na wenzake wa NCCR katika majimbo yote ya DSM lakini uchaguzi huo ulifutwa saa nane ya usiku baada ya tume kuona kuwa dsm yote imechukuliwa na upinzani.

Kwa kuwa NCCR haikuridhika na uchaguzi tanzania nzima, iliamua kujitoa, ila kisheria haikuwezekana. Wagombea wengine wote wa NCCR walitangaza kususia uchaguzi wa marudio dsm, lakini Lamwai alikataa na kushiriki; na tulimchagua kuwa mbunge wa jimbo la ubungo. Matokeo hayo yalipingwa mahakamani na Lamwai akashindwa kesi; na huo ukawa mwanzo wa mporomoko wake.

Baada ya hapo alifutiwa ualimu wa udsm na pia serikali ilimfutia leseni yake ya uwakili wa kujitegemea. Lamwai akadhoofu na akawa hana budi kujisalimisha kwa CCM. Ndipo Mkapa alimteua kuwa mbunge.

Kitendo cha Lamwai kurudi CCM na kuteuliwa na mkapa, kilimshushia heshima katika jamii - kama mchangiaji mmoja alivyosema 'siamini kama mtu aliyekuwa anaikandia sana ccm angeweza kurudi huko'. Wengi tulimwona kama mtu aliyekosa uvumilivu na ujasiri wa kundelea kuwa upinzani - alitusaliti. Kwa kuwa JK hakumteua tena kuwa mbunge; ikawa ndio mwisho wake katika siasa. Hana tofauti na Kabourou wa Kigoma
 
Mbona Lamwai amekuwa maarufu hata kabla ajachaguliwa Diwani wa Manzese, Kwenye Corridor za Mahakama za Tanzania jina lake si Dogo, Ni Mwalimu mzuri wa Sheria, kwamba UKIMWI unamtaiti, sina uhakika sana na hilo, mara nyingi nimetokea kufanya naye kazi kwa karibu sijaona tofauti ya Afya yake. Naona yuko fit.Kila mtu anahitaji kuombewa aliye na ........., na asiye na .............., unless kama mtu ameamua kuwa Towashi , vinginevyo huwezi kujua kesho yako.
 
Kwa sasa amefulia tu, yuko nyumbani kwake Ubungo Kibangu na kazi yake sasa hivi ni kukagua daftari la bili ya maziwa, biashara ya mkewe.

Aliyeko CHADEMA ni mdogo wake Joseph Selasini, yule aliyemng'oa Mramba kule Rombo.
 
Katika wanasheria walioingia kwenye siasa mimi namkubali aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA jaji mstaafu BOB MAKANI, jamaa ni noma!!!
nakumbuka wakati wa kesi ya uchaguzi CHADEMA vs CCM, mwaka 1995 kule Kigoma, jamaa aliwapelekesha puta majaji kinoma, hatimaye CHADEMA wakashinda ile kesi. Jamaa ana sauti nzito halafu anaongea kama anahasira halafu ana accent ya kisukuma hivi, du! ilikuwa burudani ya aina yake.

Mohamed Nyanga Makani alias 'Bob Makani' hajawahi kuwa jaji.
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom