Yoweri Museveni atasimamia mazungumzo ya kuleta amani Ethiopia kuanzia leo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Rais wa Uganda Yoweri Museveni atasimamia mazungumzo ya kuleta amani nchini Ethiopia kati ya serikali na maafisa wa eneo la Tigray.

Kulingana shirika la habari la AFP, maafisa wa serikali ya Ethiopia wasiotaka kutajwa wamesema kwamba mazungumzo hayo yamepangwa kuanza Jumatatu, kaskazini mwa Uganda.

Naibu waziri mkuu wa Ethiopia Demeke Mekonnen Hassen, ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje, pamoja na wawakilishi wa Tigray, wanatarajiwa nchini Uganda Jumatatu kwa mazungumzo hayo.

Hayo yanajiri wakati kiongozi wa eneo lililojitenga nchini Ethiopia, Tigray, amethibitisha kwamba wapiganaji wake walifanya mashambulizi ya roketi kwenye uwanja wa ndege katika mji mkuu wa Eritrea.

Shambulizi hilo linaongeza wasiwasi wa kusambaa kwa vita katika eneo hilo la pembe ya Afrika.

Debretsion Gebremichael, amesema kwamba wapiganaji wake walishambuliwa kila upande na maelfu ya wanajeshi wa Eritrea na vifaru anavyodai waliingia Tigray kuwasaidia wanajeshi wa Ethiopia.

Wanadiplomasia waliwaambia waandishi wa habari Jumamosi usiku kuwa makombora mengi yalipiga Asmara, yakitua karibu na uwanja wa ndege, ingawa vizuizi vya mawasiliano huko Tigray na Eritrea vilifanya ripoti hizo vigumu kuthibitisha.

Waziri mkuu Abiy Ahmed ameandika ujumbe wa Twitter kwamba Ethiopia ina uwezo wa kutosha kufanikisha malengo yake katika eneo la Tigray bila msaada wowote lakini hakujibu moja kwa moja madai ya Debretsion.

Mwanadiplomasia mkuu wa wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kwa Afrika, Tibor Nagy, alishutumu mashambulizi ya vikosi vya Tigray dhidi ya Eritrea na kulaani kile alichokiita juhudi zao za kuufanya mzozo huo kuwa wa kimataifa.
 
Huwa wanatumia vigezo gani kuchagua mtu atakayesikiliza na kusuluhisha?
Hahah hakunaga vigezo maalumu mkuu,hata Mkapa alikua amepewa kazi ya kusuluhisha mzozo wa Burundi wkt huku bongo anawaita wapinzani ni malofa na wapumbavu.

M7 mwenyewe kwake yuko anawapiga mabomu na kuua wafuasi wa Bob wine lkn leo eti yeye ndio msuluhishi.
 
Hawa watigray sijawafuatilia sana,ngoja niwafuatilie nijue harakati zao zikoje.
Hizi tuzo za Nobel ni vyema wapewe mashirika ya kiraia.

wanaharakati wa haki za binadamu, wanasayansi, watafiti wa tiba/afya, wanamazingira, waandishi wa habari/waandishi wa kazi za fasihi, wanasiasa waliostaafu siasa angalau miaka 10 iliyopita.

Hii kuwapata viongozi waliopo madarakani kunashusha hadhi ya hii tuzo.

Huyu mshindi wa Nobel ambaye ni mwanasiasa mwenye madaraka kwa sasa ameitumbukiza nchi yake vitani na kufanya maelfu ya raia wake kuwa wakimbizi.
 
WANAOWACHAGUA WATU WA USULUHISHI WAWE WANAANGALIA AINA YA KIONGOZI SIO KILA MTU history background ya kiongozi ni muhimu sana sasa hili li dikteta unalipa kazi ya usuluhishi kwa heshima ipi iliyopo? HII NAFASI ILIKUWA YA MRISHO JAKAYA KIKWETE
Kikwete huyu huyu ambae wapinzani mulimbeza kwa kumuita babu cheka? Sintoshangaa Magufuli akimsliza muda wake na yeye mutaanza kumpamba.
 
Ila watigray nawakubali sana wameitwanga ethiopia na eritrea kwa makombora mpaka waethiopia wamekuwa wapole
Unajua kule ndio ilikuwa kitovu cha vita kati ya Eritrea na Ethiopia so Ethiopia iliwekeza mashine heavy kule Tigray.

Sasa waTigray kwanza walivamia kwa kushtukiza kambi ya Federal Force na wakajimilikisha yale makombora mazito. Ndio maana majeshi kutoka Addis Ababa yanapata taabu
 
AU ni genge la wazee wapigaji tu! Hakuna la maana pale halafu ukiwagusa wanakuambia "African problems need African solutions " ambazo miaka nenda rudi tunaendelea kudumaa tu.
 
Huyu mshindi wa Nobel ambaye ni mwanasiasa mwenye madaraka kwa sasa ameitumbukiza nchi yake vitani na kufanya maelfu ya raia wake kuwa wakimbizi.
Most likely hakuwa na choice nyingine. Kwa walichofanya Watigray kama wangeachwa kwanza ingekuwa ni fedheha kwa Nchi na ingeset precedence kwa Regions nyingine kubwa kama Amhara, Oromia au Somali nao kutamani kufanya hivyo hivyo

Hii “law enforcement operation” ni muhimu sana ili kurestore heshima ya Federal government na pia kama demo kwa Regions nyingine. Afterall Watigray ni watu wajivuni mno na kimsingi regions nyingine zote zinasupport wachapwe tu
 
Most likely hakuwa na choice nyingine. Kwa walichofanya Watigray kama wangeachwa kwanza ingekuwa ni fedheha kwa Nchi na ingeset precedence kwa Regions nyingine kubwa kama Amhara, Oromia au Somali nao kutamani kufanya hivyo hivyo

Hii “law enforcement operation” ni muhimu sana ili kurestore heshima ya Federal government na pia kama demo kwa Regions nyingine. Afterall Watigray ni watu wajivuni mno na kimsingi regions nyingine zote zinasupport wachapwe tu
Nadhani wameona vita haitakuwa suluhisho la kudumu la huu mzozo ndio maana wameamua kuzungumza.
 
Nadhani wameona vita haitakuwa suluhisho la kudumu la huu mzozo ndio maana wameamua kuzungumza.
Federal government wamegoma. Wanaendelea kudondosha mabomu na hawataki kuzungumza na hao viongozi na wanajeshi wake

7E1B4D6E-0B56-4D71-BAE9-3A65C68B5B48.jpeg
 
Back
Top Bottom