Yoweri Museveni: Afrika ingeingilia kati na kuisaidia Libya dhidi ya Mataifa ya Magharibi

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
730
2,957
Uganda's President Yoweri Museveni is in London this week to attend the UK-Africa Investment Summit 2020. The event was hosted by British Prime Minister Boris Johnson who told the attending 16 African heads of state that the continent is the future of trade and business and that the UK was keen to play an important role to in developing Africa's potentials.

Mr Johnson also met the Ugandan President and spoke of the UK’s commitment to invest in Uganda and his desire to see their trade relationship "go up a gear." But it wasn't all about business and trade. Speaking to BBC Newsday’s Alan Kasujja, the Ugandan leader expressed some strong opinions how western involvement had changed the political landscape of Africa over the years.

----
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema kwamba bara la Afrika lina uwezo wa kuzuia Mataifa ya Magharibi kuingilia kati ama hata kuvamia mataifa ya Afrika kiholela.

Museveni ambaye alikuwa akizungumza na BBC amesema kwamba ilikuwa makosa kwa mataifa ya Magharibi kuivamia Libya na kumng'oa kiongozi wake Muammar Gaddafi bila ya Afrika kuzuia kitendo hicho.

Amesema kwamba viongozi wa Afrika walitumia diplomasia kutatua mzozo huo lakini badala yake wangetumia jeshi lake kukabiliana na wavamizi.

Kiongozi huyo wa Uganda anasema kwamba bara la Afrika lina uwezo mkubwa wa kuweza kuwakabili waliovamia Libya ambayo hadi sada inakumbwa na mzozo wa wenye kwa wenyewe.

''Nawaza Afrika ingeingilia kati na kumpatia mtu funzo, hapo ndipo tulipofeli'', alisema rais huyo anayedaiwa kuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika waliokalia madaraka kwa kipindi kirefu kufikia sasa.

Bw. Museveni amesema: ''Lilikuwa shambulio la uvamizi kwani hata mimi mwenyewe sikudhania kwamba mtu anaweza kuwa na mawazo ya kipuzi na kuvamia taifa la Afrika kama walivyofanya''.

''Tatizo ni kwamba tulipatikana wakati mbaya ambapo tulikuwa tumetawanyika hatuakuwa tumejiandaa'', aliongezea.

Amesema kwamba bara la Afrika lina uwezo ambao haujutumika wa kukabiliana na uvamizi wowote kutoka kwa mataifa ya magharibi.

''Iwapo tunataka kuwafurusha wavamizi tunaweza, tuliwafukuza na kuwashinda Wareno na Boers wakati wa ukolini wa mwisho wa karne ya 17 licha ya wao kusaidiwa na mataifa mengi ya kigeni.

Museveni anasema licha ya kukabiliana na wanajeshi wa Muamar Gaddaffi mara mbili nchini Uganda, anasema kwamba kiongozi huyo alikuwa na matatizo yake lakini jinsi alivyotendewa na mataifa ya magharibi ilikuwa makosa makubwa.

Anasema kwamba kulikuwa na njia chungu nzima za kukabiliana na kiongozi huyo na kwamba nguvu zilizotumika dhidi yake zilikuwa mbaya kwa kiongozi wa Afrika aliyekuwa na haiba kama yake.

Kuhusu mazungumzo yanayoendelea kuhusu Libya, Museveni anasema kwamba bara la Afrika lingechukua jukumu la kuangazia maswala yake badala ya kutegemea mataifa ya nje kutafuta suluhu Afrika.

Swala hilo linajiri wakati ambapo Ethiopia na Misri pia zimeamua kuwasilisha tatizo lao la matumizi ya mto Nile Marekani badala ya Muungano wa Afrika.
 
Day dreamer, ndio tatizo la kuwa na Marais Wazee. Not sure though kama kweli aliongea haya au hapana. Huenda alipewa Wine
1579690789832.png
 
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema kwamba bara la Afrika lina uwezo wa kuzuia mataifa ya magharibi kuingilia kati ama hata kuvamia mataifa ya Afrika kiholela.

Museveni ambaye alikuwa akizungumza na BBC amesema kwamba ilikuwa makosa kwa mataifa ya magharibi kuivamia Libya na kumng'oa kiongozi wake Muammar Gaddafi bila ya Afrika kuzuia kitendo hicho.

Amesema kwamba viongozi wa Afrika walitumia diplomasia kutatua mzozo huo lakini badala yake wangetumia jeshi lake kukabiliana na wavamizi.

Kiongozi huyo wa Uganda anasema kwamba bara la Afrika lina uwezo mkubwa wa kuweza kuwakabili waliovamia Libya ambayo hadi sada inakumbwa na mzozo wa wenye kwa wenyewe.

''Nawaza Afrika ingeingilia kati na kumpatia mtu funzo, hapo ndipo tulipofeli'', alisema rais huyo anayedaiwa kuwa miongoni mwa viongozi wa Afrika waliokalia madaraka kwa kipindi kirefu kufikia sasa.

Bw. Museveni amesema: ''Lilikuwa shambulio la uvamizi kwani hata mimi mwenyewe sikudhania kwamba mtu anaweza kuwa na mawazo ya kipuzi na kuvamia taifa la Afrika kama walivyofanya''.

''Tatizo ni kwamba tulipatikana wakati mbaya ambapo tulikuwa tumetawanyika hatuakuwa tumejiandaa'', aliongezea.

Amesema kwamba bara la Afrika lina uwezo ambao haujutumika wa kukabiliana na uvamizi wowote kutoka kwa mataifa ya magharibi.

''Iwapo tunataka kuwafurusha wavamizi tunaweza, tuliwafukuza na kuwashinda Wareno na Boers wakati wa ukolini wa mwisho wa karne ya 17 licha ya wao kusaidiwa na mataifa mengi ya kigeni.

Museveni anasema licha ya kukabiliana na wanajeshi wa Muamar Gaddaffi mara mbili nchini Uganda, anasema kwamba kiongozi huyo alikuwa na matatizo yake lakini jinsi alivyotendewa na mataifa ya magharibi ilikuwa makosa makubwa.

Anasema kwamba kulikuwa na njia chungu nzima za kukabiliana na kiongozi huyo na kwamba nguvu zilizotumika dhidi yake zilikuwa mbaya kwa kiongozi wa Afrika aliyekuwa na haiba kama yake.

Kuhusu mazungumzo yanayoendelea kuhusu Libya, Museveni anasema kwamba bara la Afrika lingechukua jukumu la kuangazia maswala yake badala ya kutegemea mataifa ya nje kutafuta suluhu Afrika.

Swala hilo linajiri wakati ambapo Ethiopia na Misri pia zimeamua kuwasilisha tatizo lao la matumizi ya mto Nile Marekani badala ya Muungano wa Afrika.
 
Anaogopa na yeye kugeukwa siku moja na kutolewa kwa nguvu ama

Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Mradi wa bomba la mafuta kutoka "Hoima" nchini Uganda hadi Tanga (Tanzania) umekwamia wapi? Mzee m7 haya mambo ya siasa kutunishana misuli na nchi za magharibi (mabeberu) hayatusaidii! Tekeleza miradi ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi wetu. Inasadikika Tanzania hiko tayari ila Uganda inasuasua!
 
Aachie ngazi kaongoza miaka yote ,tunataka controlling power ya ku balance haya aliyoyasababisha huyu deflecting power
 
Kuhusu mazungumzo yanayoendelea kuhusu Libya, Museveni anasema kwamba bara la Afrika lingechukua jukumu la kuangazia maswala yake badala ya kutegemea mataifa ya nje kutafuta suluhu Afrika.
TUJITEGEMEE....waafrika walio wengi hawataki kusikia hili.
 
Africa inabidi iingilie kati,miongoni mwa nchi zake kua na rais kwa ziaid ya miaka 30

Sent using Jamii Forums mobile app
'international terrorism sympathizers', poor all of type of you. What was done to Libya under Baath party led Comrade M. Ghaddafi (R.I.P) by invaders qualifies to be international terrorisms as it has been explained by Iran foreign minister.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom