Young Killer matunzo yamekubali, muziki unataka kukukataa

Cja walinganisha ila hata wao kweny angle yao wana ukubwa wao vile vile na sio hicho cheo cha utoto mnacho jaribu kuwapa
True. Kuna raia wa tz wanafanya trap poa sana.
Kuna
Country boy
Salmin swagz
Loski_tzn
Conboi
Moni centrozone
Young Lunya
Fredrick mulla
G_RELL
Slimsal
Chin bees
Rosa ree & frida amani
Orbit
Brian Simba
Jimmie_ wrld
Dullahstar
Rapcha_tz
Na wengineo nlosahau kuwaweka hapo

Ila nachoweza kusema Ni lazima kuweka respect kwa jina la YOUNG KILLER
 
Kiwanda cha muziki, lazima tukubali, mara ya mwisho kimetengeneza msanii ambaye kinaweza kikajitutumua na kujisifia kwaajili yake ni kilipomtambulisha "Erick Msodoki" kwa watanzania! Wengi tunamfahamu kama Young Killer, Mimi namuitaga King of Puns - Dogo anacheza na maneno sana kiasi kwamba unaweza kujiuliza alikuwa anawaza nini hadi kuandika hicho alichokiandika.

Nilianza kuwa shabiki yake zamani kidogo kwa hivyo nina facts zake ndogo ndogo ninazozifahamu. Moja na iliyonipa Tittle ya huu uzi ni kuwa: Zamani kidogo kipindi ambacho alikuwa anaanza muziki alijipa a.k.a kibao ila kubwa iliyovuma ni ile ya "handsome boy asiyekuwa na matunzo". Tukaenda na hilo jina mpaka likazoeleka hadi kwenye medias kubwa kwa kiasi cha kulifanya likawa la kwake kabisa. Akatutambulishia "Matunzo zero unit" kuonesha ni kiasi gani alivyo hana matunzo. Basi kwenye hii phase huyu ndugu yangu alitupa ladha, mistari na muziki ambao tulikuwa tunautaka. Naongelea hits kama "13", " Umebadilika", "My Power", " Dear Gambe", na zingine nyingi nyingi sana!

Kusema kweli tulifaidi ladha ya hip hop. Na ni ukweli usiopingika Young Killer ni moja kati ya wasanii ambao wamefanya muziki wa hip hop uwe na mashabiki - Nawajua washkaji baadhi na mademu kadhaa ambao wao hip hop haikumaanisha chochote hadi walipomsikiliza Young Killer na mitazamo yao juu ya huu muziki ukabadilika!

Sasa hapa kati sijui ikawaje?? Ni ghafla tu the kid switched. Kuna intavyuu moja pale Wasafi FM, kama kumbu kumbu zangu hazinidanganyi, jamaa alisema matunzo yamekubali kwa hivyo akatangaza rasmi yeye sio "Handsome boy aliekosa matunzo" kuanzia pale na kuendelea and that was that. Ilikuwa intavyuu nzuri, lazima nikubali na hoja yangu kubwa sio yeye kubadilisha jina ila najaribu kutumia lugha ya picha kuelekeza hili suala ili lieleweke.

By the time anatangaza uamuzi ule alikuwa ameachia Jitafute. Kwa hivyo tukasubiria wimbo ambao utabeba utambulisho wa handsome boy mwenye matunzo hatimae jana ikafika, nikiwa YouTube nikaona hio inayoitwa "Leo". Binafsi mimi sio prodyuza ila ile ngoma nitaiweka kwenye kundi la trap - sio hip hop. Na sio yule Young Killer tunaemtaka. Period.

Bro, sisemi ameshuka ila namkumbusha tu hizo michezo za trap awaachie hao watoto watoto kina OMG, Country Boy na Chin Bees. He is better than that!
Choo cha kike ulichoingia umekuta demu wako anamegwa
Nnavoanza kumkubali killer kabla haja hit alikua ana ryhme tamu
 
Huyu Amefanya kuandika tu hiyo mistari ya dogo mmoja hivi YOUNG LUNYA naona anataka tension kwa kuanzisha battle na KILLER. Coz. OMG ishaanza ku drop na kila mtu anafanya project zake mwenyewe
Leo hii Tz tuna waweka kweny mzani wa ubora kati ya ali kiba na mond ni kwa sababu wote wanafanya mziki aina moja na matokeo yke tuna pata majibu sawia ila Mnacho jaribu kukifanya ni kama kumpima Nash mc na marioo na majibu yake yawe Nash mc ni mtoto sana kwa marioo hiyo sio kweli kuwapima hao wa wili na kupata majibu sawia kati ya Marioo na Nash mc Ni lazima marioo nae Atie miguu kweny hip hop then tuna wapima na kipimo kitasema ukweli Na ndy maana hata kweny hesabu baadhi tuna toa kwani mabano na kuendelea ku calculate
 

Similar Discussions

5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom