Young jeezy na rick ross washikana mashati 'backstage' wakati wa tuzo za bet hiphop awards. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Young jeezy na rick ross washikana mashati 'backstage' wakati wa tuzo za bet hiphop awards.

Discussion in 'Celebrities Forum' started by NEW NOEL, Oct 1, 2012.

 1. NEW NOEL

  NEW NOEL JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 837
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 60
  Rick-Ross.jpg
  Yalianza maneno,kila mtu anamrushia mwenzake,ghafla wakaanza kusukumana...watu hawajakaa sawa,milio ya risasi ikasikika.
  Ilikuwa back stage kwenye tuzo maarufu za BET HIPHOP AWARDS zilizokuwa zinafanyika Atlanta ambapo Rozay na Young Jeezy walianza kurushiana maneno na ghafla kusukumana. Tukio hilo la ajabu lilipelekea risasi kusikika na inaelezwa ni mmoja wa watu wa karibu Rick Ross ndio alirusha risasi. Ingawa inaelezwa kuwa kutoweka huko kwa amani kulifanikiwa kutulizwa na watu wa usalama na shughuli nyingine kuendelea kama kawaida.
  Ni takribani miaka kama miwili ambapo Young Jeezy na Rick Ross wamekuwa hawaelewani na chanzo kinaelezwa kuwa ni pale Rick Ross alipotoa wimbo wa BMF (Blowing Money Fast) na Young Jeezy kumponda Rick Ross kuwa anaimba asichokijua. Katika wimbo wa BMF rozay anamtaja Big Meech ambaye ni mmoja wa watu wa karibu wa Young Jeezy na kwa sasa yupo jela. Na ndio sababu ya Young Jeezy kumponda Rozay kuimba wimbo unaomuhusu mshikaji wake wa muda mrefu.
  Hivi karibuni Rick ross alieleza kuwa yupo tayari kufanya kazi na Young Jeezy na kulikuwa na tetesi ya uwezekano wa wawili hao kufanya kazi ya pamoja.
  POPOTE TZ
   
Loading...