Young D vs Young Killer (Bongo bahati mbaya v Pambana na hali yako)

ubuntuX

JF-Expert Member
Aug 18, 2014
1,970
2,184
Kiukweli kwa sasa mayoung wanaotamba mjini wamebaki wawili tu kwa hii game ya hiphop, hapo awali dogo janja alijumuishwa pia lakini kwa sasa ametupwa nje na hawa madogo wanaotamba
Young dee anadude lake linakwenda kwa bongo bahati, hii imepelekea kuibuka kwa msemo hapa mjini "Bongo bahati mbaya" (BBM)
Huku kwa young killa ametoka na hitsong zake kama nne hivi zote zikiisha na msemo unashika jiji sasa "Pambana na hali yako"


Msemo upi unakimbiza saana mjini, maana msemo wako ukibamba sana ni ishara tosha ngoma yako imepenya kwa washabiki wa muziki kitu ambacho ni ngumu sana kwa sasa

Bongo bahati mbaya vs pambana na hali yako!



Kwangu naupenda sana huu, "pambana na hali yako"
 
Aisee nimesikia msemo wa pambana na hali yako kabla sijasikia ngoma yenyewe... Young killa atakua katisha
 
pambana na hali yako haukuwa wimbo rasmi, ila ilikuwa zawadi nzuuuri ya Eid kwa Ney wa mitego.
 
Young killer ana hit song moja hivi inaitwa UNAIONAJE akiwa na Harmonize.Mwishoni anamalizia pia Pamabana na hali yako.Huyu dogo hajawahi kuwaacha madogo wenzie salama
 
Mwenye song la young killer pambana na hali yako naomba anisaidie japo ahiweke humu ndani.
 
Back
Top Bottom