Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Lakini mbumbumbu wao wako huru kufanya watakachoView attachment 1496900
Jamal Malinzi si ametoka jela, muiteni awabebe tena, vyura zenu keleke tu
IMG-20200621-WA0000.jpg
 
Daktari wa klabu ya Yanga Dk Shecky Mngazija amesema hali ya kiungo fundi Haruna Niyonzima ambaye alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Biashara United, anaendelea vizuri.

Niyonzima alicheza mchezo huo kwa dakika saba tu baada kupata majeraha kwenye dakika ya tatu na kulazimika kutoka kwenye dakika ya saba baada ya kushindwa kuendelea na mchezo.

Dk Mngazija amesema Niyonzima anaendelea na matibabu na upo uwezekano atakuwa sawa kabla ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa Julai 09.

Aidha ameeleza kusikitishwa na mchezo wa kibabe ulioonyeshwa na vijana wa Biashara United ambao umesababisha nyota wake kupata majeraha.

"Siyo Niyonzima tu, nahodha wetu msaidizi Juma Abdul na Abdulaziz Makame nao wamepata majeraha lakini tunashukuru wote wanaendelea vizuri," alisema.

Baada ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Yanga itarejea jijini Dar es salaam ambapo Julai 12 inakabiliwa na mchezo wa nusu fainali kombe la FA dhidi ya Simba.
 
Back
Top Bottom