Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Uongozi wa #MabingwaWaKihostoriaTanzania, unamkaribisha tena kikosini beki @vicentandrew ‘Dante’ baada ya kumalizika kwa shauri la kesi baina ya pande mbili.
Karibu tena Nyumbani.

@Yangasc

japo nawaza kiwango chake kwa muda aliokuwa nje akishughulikia haki zake.
Hivi alikuwa hachezi sababu ya madai au kulikuwa na lingine? Nahofia kama ilikuwa ni madai pengine uongozi unaweza kushinda ilihali yeye hajaridhika hivyo anaweza asiwe na moyo pia kama alivyokuwa awali.
 
Yah!! Ni hilo la madai tu Mkuu hakuwa na jengine.

Hata na mie nimewaza hivyo sababu ni TFF ndio wametoa hayo maamuzi na huwezi jua moyoni mwake huenda alishapanga kufanya maisha sehemu pengine.

Ila tusubiri tuone sababu hata Juma Abdul alikuwa na madai kama yake akagoma mwisho wa siku alipomalizana na Uongozi aliporudi wamempa nafasi na anacheza kwa moyo tu.
 
Of course akiwa professional atapiga kazi
 
20191214_100117.jpg
Tanzia:
Klabu ya Yanga inasikitika kutangaza kifo cha Mwanachama wetu Maarufu na Mzee wetu Ibrahim Akilimali kilichotokea alfajiri ya leo Bagamoyo Mkoani Pwani. Maziko yanatarajiwa kufanyika kesho saa 10 jioni Tandale kwa Mtogole.

Innah lillah wainnah ilayh rajiuun.. Haikuwa Dunia ila ni mapito.

@Yangasc
 
20191214_101348.jpg

Jana tumecheza Mechi ya Kirafiki Kigoma
FT
Mwamgongo FC 1 - Yanga Sc 2.

Goli la Mwamgongo lilifungwa na Abdullazak Boban huku ya Yanga yalifungwa na Balama 19 na Adam Stanley 34
 
Tanzia:
Klabu ya Yanga inasikitika kutangaza kifo cha Mwanachama wetu Maarufu na Mzee wetu Ibrahim Akilimali kilichotokea alfajiri ya leo Bagamoyo Mkoani Pwani. Maziko yanatarajiwa kufanyika kesho saa 10 jioni Tandale kwa Mtogole.

Innah lillah wainnah ilayh rajiuun.. Haikuwa Dunia ila ni mapito.

@Yangasc
Mwenyezi Mungu ampe makazi anayostahili Mzee Akilimali.
 
20191215_165112.jpg
TARIQ KIAKALA AWASHUKURU MASHABIKI KWA MAPOKEZI NA DUA ZAO

Mshambuliaji mpya wa Yanga Tariq Seif Kiakala amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa mapokezi waliyompa baada ya kukamilisha usajili wake kujiunga na mabingwa hao wa kihistoria

Tariq amesema ni heshima kubwa kwake kujiunga na Yanga, anaamini kwa ushirikiano na wachezaji walipo, wataweza kutimiza malengo yliyowekwa na timu "Juzi baada ya kukamilisha zoezi la kusaini mkataba wa kujiunga Yanga, sikupata nafasi ya kuwashukuru mashabiki wa timu yangu mpya. Hivyo nachukua fursa hii kuwashukuru kwa dua zenu mpaka hili limekamilika na nawaahidi sitawaangusha" "Nitajituma na kushirikiana na wachezaji wenzangu kufikia malengo yaliyowekwa na uongozi wa klabu, najua mashabiki wote mtatuunga mkono mimi na wenzangu ili tuwape furaha," amesema

Tariq ameongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga baada ya timu hiyo kuvunja mikataba ya Sadney Urikhob na Juma Balinya

Kama TFF itamuidhinisha mapema huenda akaanza kuonekana dimbani wiki ijayo kwenye wa kombe la FA dhidi ya Iringa United.

@Yangadaima
 
Back
Top Bottom