Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Tuombe
Subiria Jumamosi Ses pia nikukaribishe uje ujionee yatakayotokea dhidi ya Zesco.
Tuombe uzima Shadeeya maana tusiandikie mate na wino ungalipo. Nitakua pembeni yako nikiwa tayar kabisa kutoa huduma ya kwanza maana nahisi pressure yako itakua juu muda wote wa mechi
 
Tuombe
Tuombe uzima Shadeeya maana tusiandikie mate na wino ungalipo. Nitakua pembeni yako nikiwa tayar kabisa kutoa huduma ya kwanza maana nahisi pressure yako itakua juu muda wote wa mechi
Hii kauli Ses naikumbuka ulishaitamka tangia Mechi na Township Roller na mwisho wa siku mi ndio nilikaribia kukupa huduma ya kwanza. 🤣🤣. Hivyo angalia yasijirudie tu.
 
20190913_110938.jpg
 
20190913_111022.jpg

Kesho ndio ile siku inayosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa klabu ya Yanga ambapo timu yao itashuka dimba la Taifa kuikabili ZESCO United ukiwa ni mchezo wa ligi ya mabingwa raundi ya kwanza

Yanga ilifanya mazoezi yake ya mwisho jana kwenye uwanja wa Taifa 

Kocha Mwinyi Zahera alisema wamefanya kila linalotakikana kupata ushindi dhidi ya ZESCO, imebaki zamu ya mashabiki kuonyesha sapoti yao kwa kujitokeza kwa wingi uwanjani

Leo ZESCO United itaruhusiwa kufanya mazoezi kwenye dimba la Taifa, kulingana na sheria za FIFA

Yanga inahitaji kushinda kesho ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa kwa mara ya pili katika historia yake

Mwaka 1998 Yanga ilikuwa klabu ya kwanza kutoka Tanzania kutinga hatua ya makundi, wakati huo timu 8 tu zilikuwa zikiingia lakini sasa ni 16

Yanga soccer
 
Mlinda lango Farouk Shikalo amepata leseni ya CAF ambayo itampa nafasi kuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoikabili ZESCO United kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa kesho

Hata hivyo Shikalo ameingia kikosini wakati ambao Metacha Mnata anafanya vizuri

Metacha alidaka mechi zote mbili za hatua ya awali dhidi ya Township Rollers

Kwenye mchezo wa marudiano uliopigwa nchini Botswana, Metacha alifanya kazi kubwa kuhakikisha Yanga inasonga mbele

Tukio muhimu alilofanya kwenye mchezo huo ni kuokoa mkwaju wa penati 

Metacha anaonyesha kujiamini, michezo hiyo imemuimarisha sana, ana kila sababu ya kuaminiwa na benchi la ufundi kuanza kwenye mchezo wa kesho

Jambo muhimu zaidi ni kuwa sasa Yanga ina amani kwenye eneo la ulinzi wa lango

Mlinda lango atakayepewa nafasi kesho, bila shaka atatimiza wajibu wake kikamilifu.

Yanga Soccer
 

Similar Discussions

97 Reactions
Reply
Back
Top Bottom