Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Daah! Ulivyoandika hadi nimeona aibu lol.

Hapana wala sitaki kumuona hiyo saa anavua.
Karibu kwa Mkapa uone soka maridadi, soka la ufundi na udambwidambwi mwingii, magoli ya move, magoli yakiufundi haswaa wa soka bila kusahau vibe la mashabiki wa mnyama wa Lunyasi
 
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema bado anafanyia kazi safu yake ya ushambuliaji ili iongeze makali ya kuzifumania nyavu

Akizungumza baada ya kuwasili kutoka Botswana leo, Zahera amesema bado washambuliaji wake hawana muunganiko mzuri

"Tuna tatizo moja la washambuliaji kujipanga tunaposhambulia ndio maana mabao mengi tunafunga kupitia mipira ya adhabu na kona," amesema

"Hili ni tatizo ambalo tunalifanyia kazi, hata baada ya mchezo dhidi ya AFC Leopards, niliwaambia wachezaji wangu kuhusu hili"

"Tulipokuwa Botswana tulitumia muda mwingi kufanya mazoezi ya kujipanga tunapokuwa na mpira mita 30 kuelekea lango la mpinzani"

Tangu mchezo dhidi ya Kariobangi Sharks, Yanga imefunga mabao yake kupitia mikwaju ya penati, adhabu na kona

Hata hivyo Zahera atakuwa na wiki tatu kurekebisha mapungufu hayo kabla ya kuikabili ZESCO United

Habari njema ni kuongezeka kikosini kwa mshambuliaji David Molinga ambaye ataruhusiwa kuichezea Yanga kuanzia mchezo huo

Pia mlinda lango Farouq Shikalo na beki Mustafa Suleyman nao hawatakuwa na pingamizi la kushiriki mchezo huo
 
Juma Balinya alifunga bao pekee la Yanga kwenye mchezo dhidi ya Township Rollers uliomalizika kwa mabingwa hao wa kihistoria kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kutinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa

Yanga imerejea usiku wa kuamkia, mapokezi aliyopewa na mashabiki yamempagawisha Mganda huyo

Mashabiki wenye furaha waliisubiri Yanga mpaka usiku wa manane, walipotua Balinya alivamiwa na umati wa mashabiki ambao walimtuza fedha kumshukuru kwa kazi aliyofanya Botswana

Yeye hakuwa akifahamu, hii ndio heshima ambayo utaipata unapofanya vizuri Yanga

Mashabiki wa Yanga wana upendo kwa timu yao, wako tayari kutoa kile walichonacho ili kuhakikisha wanapata furaha
 
Wachezaji watano wa Yanga wanatarajiwa kujiunga na timu za Taifa baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ruvu Shooting utakaopigwa keshokutwa Jumatano kwenye uwanja wa Taifa/Uhuru

Metacha Mnata, Kelvin Yondani, Mohammed Issa na Abdulaziz Makame watajiunga na kambi ya kikosi cha Stars ambacho Septemba 02 kitakuwa ugenini nchini Burundi katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga makundi ya kusaka nafasi ya kucheza kombe la dunia 2022 kwa upande wa Afrika

Mlinda lango Farouq Shikalo yeye ataelekea kwao Kenya kujiunga na Harambee Stars itakayochuana na Uganda kwenye mchezo wa kirafiki

Wachezaji hao watakosa sehemu ya maandalizi ya kikosi cha Yanga kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya ZESCO ambao utapigwa kati ya Septemba 12-15 uwanja wa Taifa

Tanzania itamaliza hapa nchini mchezo dhidi ya Burundi Septemba 08 2019
 
Kipa wa Yanga, Metacha Mnata amesema kupangua penalti kwake haikuwa ya kubahatisha kwani alimsoma vyema mpigaji.

Mnata amesema baada ya wapinzani wao Township Rollers kupata penalti hakuwa na wasiwasi aliwatuliza wachezaji wenzake na kumsubiri mpigaji.

Wakati kiungo Segolame Boy akijiandaa kupiga penalti hiyo Mnata amesema alijua mpigaji huyo alitaka kumdanganya wapi anapopeleka mpira kwa kutumia macho yake na baadaye kuidaka kiurahisi.

Alisema alitambua umuhimu wa kuwa mtulivu na kucheza penalti hiyo kwa kuwa kama wapinzani wao wangefunga ingewaongezea nguvu huku wao wakiingia katika presha ya kupoteza.

Kipa huyo alisema licha ya ushindi wao huo mchezo huo haukuwa rahisi kwani walihitaji kupambana zaidi kuhakikisha wanaitetea klabu yao na mwisho wa mchezo walifanikiwa.

Aidha Mnata alisema kuelekea mchezo dhidi ya Zesco ya Zambia wanatambua kwamba haitakuwa mechi rahisi na kwamba watajipanga kuhakikisha wanashinda vizuri.

Mwanaspoti

Screenshot_2019-08-26-20-14-37.jpeg
 
20190827_061347.jpg
Imeelezwa kuwa ushindi wa Yanga nchini Botswana ulichangiwa na mambo mengi, ikiwamo kitendo cha Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Frederick Mwakalebela kuwazidi ujanja wenyeji wao.

Mmoja wa Watanzania wanaoishi Botswana, Dickson John, aliliambia gazeti la Bingwa kuwa viongozi wa Township Rollers walitishwa na kocha wao, Tomas Trucha, raia wa Jamhuri ya Czech alipowaambia Yanga si timu ya mchezo mchezo hivyo kusuka mikakati kabambe ya nje ya uwanja ili kuwamaliza Wanajangwani hao. "Walipanga kuwaanza kuwadhibiti Yanga toka uwanja wa ndege hadi hotelini, waliposikia kuna viongozi wa Yanga walishatangulia hapa, walipagawa, wakahofu mambo yao yasijejulikana na kujitia aibu CAF (Shirikisho la Soka Afrika), matokeo yake wakaamua kusubiri matokeo ya uwanjani," alisema.

Watanzania waishio Botswana walikuwa na mchango mkubwa kwani walihaha kushirikiana na Mwakalebela na viongozi wengine wa Yanga kuhakikisha hakuna hujuma yoyote inayofanyiwa timu yao na mwisho wa siku, mshindi apatikane uwanjani kama ilivyokuwa. "Jana (juzi) baada ya mchezo, viongozi wa Rollers na mashabiki wao, walichanganyikiwa, hawakuamini kilichotokea," alisema John.

Yanga haikumpeleka Mwakalebela Botswana kwa bahati mbaya, uzoefu wake kwenye masuala ya Kimataifa kufahamiana na watu nchini Botswana ilikuwa ni faidi kubwa kwa Yanga
 

Similar Discussions

97 Reactions
Reply
Back
Top Bottom