Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

DAIMA MBELE.... NYUMA MWIKO!View attachment 1178184
Tatizo nini sasa hapo? Unjano na weusi! Kwani hii ni nini?
IMG-20190803-WA0003.jpg
 
Hongera Yanga kwa ushindi dhidi ya AFC Leopalds. Wachezaji wamecheza kwa kujituma ili kurudisha imani kwa mashabiki. Changamoto ni safu ya umaliziaji. Kiukweli washambuliaji wa kati wanatakiwa waongeze bidii na uchu wa kufunga.

Pengo la Makambo liko wazi kabisa! Inashangaza kocha kumuuza mchezaji kirahisi tu na wakati bado alihitajika kwenye timu. Achilia mbali Gadiel Michael.
 
Tuweke ushabiki pembeni Mchezo wa Yanga na Township Rollers huenda ukaamua hatima ya Kocha Mwinyi Zahera.

Baada ya kufanyika usajili makini, jambo pekee ambalo mashabiki wa Yanga wanataka kuona, ni timu yao ikifanya vizuri

Ukiachana na michezo ya kirafiki ambayo Yanga imecheza, matokeo ya mchezo wa kwanza wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers hayakuwafurahisha wengi hasa ikizingatiwa mchezo huo ulipigwa ardhi ya nyumbani

Tayari baadhi ya mashabiki wameanza kuhoji uwezo wa kocha Zahera katika kuipa mafanikio timu hiyo msimu huu

Ni jambo la kawaida hasa pale timu inapokuwa haipati matokeo ingawa bado ni mapema sana, lakini hali hiyo ilitarajiwa

Kwa misimu miwili Yanga haikuwa katika ubora wake wa miaka mingi, hivyo baada ya usajili wa nyota wengi wapya, mashabiki walitarajia kuiona Yanga mpya

Kocha Mwinyi Zahera anafahamu kama Yanga itaondoshwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa hatua hii ya awali, basi atakuwa kwenye wakati mgumu

Na pengine hiyo ndio sababu iliyomfanya achukizwe na ziara ya timu yake mikoa ya Arusha na Kilimanjaro ambapo alibainisha kuwa haikuisaidia timu kwa kuwa walicheza kwenye mazingira ya viwanja ambavyo haviendani na mazingira watakayocheza huko Botswana

Hata hivyo uongozi wa Yanga umesema ziara hiyo iliikuwa na manufaa na iliandaliwa kwa matakwa ya benchi la ufundi

Lakini jambo la msingi kwake ni kuhakikisha Yanga inashinda ugenini ili kuweza kusonga mbele raundi ya kwanza

Matokeo tofauti na ushindi, yatamuweka kwenye wakati mgumu mbele ya mashabiki wa timu hiyo ambao wengi wameendelea kumuunga mkono licha ya kutoridhishwa na matokeo ya michezo ya hivi karibuni

Katika moja ya mahojiano yake, Zahera alisema wamedhamiria kushinda ugenini, lengo likiwa kupata bao mapema ili kuwaweka kwenye presha Township Rollers watakaokuwa wakicheza nyumbani

Pengine huu ndio mchezo ambao Wanayanga wataishuhudia ile timu yao halisi wanayoitaka

Lakini kama mambo yakienda 'kombo', mchezo huo utazidi kumpunguzia imani Zahera

Kwani siku zote, makocha wanaajiriwa ili wafukuzwe pale inapotokea timu haifanyi vizuri
 
Jamani Yanga mpira ukiisha muwahi kuondoka hapo uwanjani, Wasauzi wasije wakawakamata kufidia madeni yao wanayodai kwa Serakali ya Tanganyika.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom