Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Iyo sale lazima iwa cost,maana kama mmeshindwa kufua dafu nyumbani ugenini mtaweza?
Hata nyie hamko salama kama mnavyodanganyana, mwaka huu siyo mwaka Jana , kila timu inaweza kupata matokeo bila kujali iko home au away cha msingi ni kujipanga kuliko mpinzani wako tu.
 
Hata nyie hamko salama kama mnavyodanganyana, mwaka huu siyo mwaka Jana , kila timu inaweza kupata matokeo bila kujali iko home au away cha msingi ni kujipanga kuliko mpinzani wako tu.
POLE WEEE. Yanga sio SIMBA
Ndio mana hta uwanja MLIUOGOPA. SUBIRI UONE MUZIKI WA WANAUME
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Mpira hauna ugenini wala nyumbani baka alishinda tatu akapigwa nne

Kwahyo usikalili katika soka hatuna formula ya ushind unapigwa hata kwako

Kwahyo Simba kupata droo kule na ud songo ndio unategemea atashinda kwa urahis hapa taifa unajua timu pinzani inakuja na plan gani?¿??????
Manara kawaharibu hawa. Teh teh
 
20190813_093735.jpg

TETESI ZA AFISA HABARI YANGASC

Uongozi wa Yanga huenda ukafanya mabadiliko katika kitengo chake cha habari ambapo Mwanahabari Antonio Nugaz huenda akamrithi Dismas Ten

Nugaz amekuwa akisimamia matukio makubwa yote ya klabu ya Yanga akiwa 'MC'

Aidha Ten ambaye sasa anakaimu nafasi ya Katibu Mkuu, huenda akarithi moja kwa moja nafasi hiyo iliyoachwa na Charles Boniface Mkwasa

Kumekuwa na presha kubwa kutoka kwa mashabiki ambao wanataka mabadiliko kwenye kitengo hicho kutokana na kukosekana kwa hamasa

Siku ya tukio la Kubwa Kuliko, Rais Mstaafu awamu ya nne Mh Dk Jakaya Kikwete alishangazwa na kutokuwepo kwa hamasa miongoni mwa mashabiki wa Yanga kujitokeza uwanjani tofauti na watani zao Simba

Hali hiyo imejitokeza juzi kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers ambapo mashabiki wachache walijitokeza uwanjani

Wengi wanadhani hakuna hamasa ya kutosha ya kuwafanya mashabiki watoke majumbani kwao kuelekea uwanjani - Yanga_soccer
 
20190813_094337.jpg

Beki kisiki wa Yanga Kelvin Yondani amesema amerejea rasmi kikosini na atakuwepo kwenye mchezo wa marudiano wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers ambao utapigwa jiji la Gaborone nchini Botswana

Yondani, Juma Abdul na Andrew Vicent walikosa mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa wakijiweka pembeni wakisubiri wakamilishiwe madai yao na uongozi wa Yanga

Kocha Mwinyi Zahera aliwaunga mkono wachezaji hao akiutaka uongozi umalizane nao ili warudi kikosini

Habari njema ni kuwa changamoto ya wachezaji hao imemalizwa na watakuwa sehemu ya kikosi kitakachoelekea mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Rollers "Mimi sina tatizo na uongozi, kila kitu kimerekebishwa hivyo nawaambia mashabiki wasiwe na hofu," amesema "Nitakuwepo kambini Moshi na pengine mchezo wa marudiano Botswana nitacheza"

Kurejea kwa Yondani kikosini huenda kukamlazimu Zahera kukifanyia mabadiliko kikosi chake cha kwanza

Zahera amekuwa akiwatumia Ally Mtoni na Lamine Moro katika nafasi ya ulinzi wa kati

Anaweza kumpeleka Mtoni pembeni na kati wakacheza Moro na Yondani

Katika mchezo huo wa marudiano, pia Zahera atakuwa na nyota waliokosa mchezo wa kwanza kutokana na kuchelewa kuwasili kwa vibali vyao

Nyota hao ni Farouk Shikalo, Mustapha Suleyman na David Molinga - Yanga_soccer
 
20190813_094906.jpg

Kikosi cha Yanga jana kimeelekea mkoani Arusha kuweka kambi ya maandalizi ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers

Baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Taifa, Yanga inahitaji kushinda Botswana au hata sare ya kuanzia mabao mawili itawabeba hatua inayofuata

Hali hiyo inaufanya mchezo huo uwe wa kufa na kupona kwa mabingwa hao wa kihistoria

Kutolewa raundi ya kwanza kwenye michuano hiyo ni jambo amalo halitawafurahisha mashabiki wa timu hiyo ambao wengi wamerejesha imani baada ya kikosi kusukwa upya

Yanga itaelekea mkoani Arusha ikiwa na majembe yake yote wakiwemo Kelvin Yondani, Juma Abdul na Andrew Vicent ambao hawakuwa kikosini

Maproo kupata vibali

Habari njema zaidi ni kuwa kwenye mchezo wa marudiano huko Botswana Yanga itakuwa na uhakika wa kuwatumia nyota wake Farouq Shikalo, Mustapha Suleyman na David Molinga ambao walikosa mchezo wa kwanza kutokana na kukosa vibali

Kocha Mwinyi Zahera amesema wachezaji hao watakiongezea nguvu kikosi chao kwenye mchezo wa marudiano

Ikiwa Arusha Yanga itacheza michezo miwili ya kirafiki; August 16 itacheza na Polisi Tanzania mkoani Kilimanjaro na August 18 itacheza na AFC Leopards - Yanga_soccer
 
20190813_095716.jpg


Mshambuliaji wa Yanga Patrick Sibomana amefichua kuwa mkwaju wa penati aliokosa kwenye dakika ya 30 ya mchezo dhidi ya Township Rollers, ulimuondoa mchezoni kwa muda

Sibomana mmoja wa wapambanaji wapya kwenye kikosi cha Yanga amesema walihitaji kushinda mchezo huo hivyo aliumia sana baada ya kukosa mkwaju wa penati "Ilikuwa nafasi adimu kwetu, baada ya kukosa nilisikitika sana, nilikuwa nikifikiria nitawaambia nini wachezaji wenzangu na mashabiki wetu," alisema

Hata hivyo Sibomana amesema kuwa alijipa moyo na kuendelea kuipigania timu

Kuhusu kupiga penati ya pili, Sibomana amefichua awali alimtaka nahodha Papi Tshishimbi apige lakini akamwambia apige tena "Nilimwambia Tshishimbi apige lakini naye akaniruhusu nipige tena"

Sibomana amesema wanajiandaa kikamilifu kuhakikisha wanapata ushindi kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Botswana August 25 "Bado tuna nafasi ya kusonga mbele, sasa tunajiandaa vyema kuweza kupata matokeo ugenini"
 
 
20190816_101846.jpg
Msafara wa kikosi cha Yanga unatarajiwa kuondoka nchini August 20 kuelekea Botswana kwa ajili ya mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers Mchezo huo utapigwa August 23, jijini Gaboronne Yanga imeweka kambi Moshi ikijiandaa na mchezo huo Mabingwa hao wa kihistoria wataunganisha moja kwa moja kutoka Moshi kuelekea Botswana baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya AFC Leopards ambao utapigwa Jumapili, August 18 Leo Ijumaa Yanga itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Polisi Tanzania #sisihao✈ - Yangafulldoz
 
20190816_112410.jpg

Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema kurejea kwa beki Juma Abdul ni habari njema kwa kikosi chake kinachojiandaa na mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers

Abdul alikosa mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Dar es salaam, akiweka ngumu kuingia kambini hadi alipwe madai yake

Abdul ana nafasi ya kuanza mchezo utakaopigwa Botswana August 23 baada ya Boxer kupata majeraha

Zahera amefichua kuwa anataka kumtumia Abdul kwenye mechi hiyo ya ugenini kumimina krosi zenye macho ambazo zitakuwa zikiwafikia mastraika wake watakaokuwa na kazi ya kufunga tu, baada ya kubaini kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita walizikosa krosi hizo. "Kikosi chetu kilikuwa kikimtegemea zaidi Boxer ambaye atakuwa nje kwa muda baada ya kuumia goti kwenye mchezo wa awali ulioisha kwa sare ya 1-1, lakini hata wale ambao niliwatumia kuziba nafasi yake hawakufiti ndio maana nimefurahi Abdul kurejea," Zahera amenukuliwa na Mwanaspoti

Zahera alisema kwa jinsi alivyowasoma wapinzani wake amegundua ni wabovu kwenye mipira ya krosi, hivyo ujio wa beki huyo anayefanya vizuri eneo hilo inaweza ikawa dawa dhidi ya wapinzani wao kuweza kupata matokeo katika uwanja wao wa ugenini

Kuhusu Yondani, Zahera alisema pia ana nafasi ya kucheza itategemea na mfumo atakaoutumia, huku akiwamwagia sifa mabeki Ally Mtoni ‘Sonso’, Lamine Moro jinsi walivyocheza kwa kuelewana hawakuwa na makosa mengi kwenye mchezo huo.

Alisema kwa mfumo wa kuchezesha mabeki watatu Yondani anaweza kufiti kwa kukaa kati huku Sonso na Moro wakiwa pembeni yake, lakini alisisitiza mchezo unaofuata unahitaji mawinga wenye kasi sambamba na mabeki wa kupanda kupitia pembeni.
#sisihao✈ - Yangafulldoz
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom