Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

Itakuwa vyema zaidi Mkuu kwani misimu miwili iliyopita tulikuwa dhohofu lihali na kama msimu huu wachezaji tu na hamasa ya kocha ndio iliyotufanya tusimame na kuwapeleka puta mikia.

Hivi huyo Lamine Moro ni mzuri kweli nina wasiwasi kama atakua sio mzito kama Wawa, na huyo Mzambia ni kweli tumesajili? Uzuri nimeziona dalili za ari ya kufanya vizuri msimu ujao
 
Yanga tumepata nafasi ya kushiriki klabu bingwa msimu ujao. Tahadhari kwa viongozi wetu wa timu na benchi la ufundi kwa ujumla; Fanyeni usajili makini kama walivyofanya watani wetu wa jadi msimu uliopita. Achaneni na wachezaji wa kawaida.

Jengeni kikosi imara na tishio dhidi ya wapinzani wetu wa ndani na nje! Mambo ya Ally Ally sijui na 10% achaneni nayo! Msimu uliopita, mmetutesa sana mashabiki wenu maana timu yetu ilikua na wachezaji wa kawaida sana kiasi kwamba hatukuwa tishio kwa timu nyingine kama ilivyokua kwa Simba; na wachezaji wengi walikua ni tia maji tia maji tu! Msimu huu tuseme tu inatosha.
 
Hawa wataweza klabu bingwa? Msajili kwa umakini. Kule sio mchezo, simba imewabeba mtapata pesa kule mkifanya vizuri.
 
Nina imani hili jukwaa linapitiwa na viongozi wetu wa Yanga. Mimi kama shabiki wa Yanga tangu utotoni mpaka nilipofikia ktk umri wangu huu wa utu uzima; Naomba nitoe rai kwa viongozi wangu wa Yanga mliochaguliwa hivi karibuni;

Kama kuna uwezekano wa kusitisha mkataba na mwalimu Mwinyi Zahera, fanyeni hivyo ili kulinda maslahi ya timu na pia hadhi yenu kama viongozi iweze kuheshimika na kutambulika.

Ni ukweli ulio wazi, ametusaidia sana kwa hali na mali msimu uliopita hadi timu yetu kushika nafasi ya pili na kupata nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa Afrika msimu ujao. Lakini tukubali tu ukweli kocha wetu ana mapungufu hasa nje ya uwanja na hivyo wakati fulani kutishia umoja na mshikamano ndani ya timu na klabu kwa ujumla.

Amekuwa ni mlalamishi kupitiliza kwa TFF, bodi ya ligi, waamuzi, wachezaji, nk. Amejipa majukumu mengi ndani ya klabu jambo ambalo binafsi naona siyo sahihi.

Amekua si mtu wa kushaurika! Akiamua ameamua kiasi kwamba anaonekana yuko juu ya timu jambo ambalo naona siyo sahihi kiasi fulani. Mfano ni wakati wa kulishughulikia suala la Benno Kakolanya( lilikua ni jambo la kusameheka lakini alimkataa mwanzo mwisho) ili tu mkongomani mwenzake Kindoki apate nafasi lakini mwisho wa siku matokeo tuliyaona!

Kwenye suala la Makambo pia tulishuhudia alipojivika joho la uwakala wa mchezaji pasipokujali maslahi ya timu kama mchezaji bado anahitajika au la! Pia nikasikia tetesi alimkataa kocha Mecky Maxime asijiunge Yanga kuongeza nguvu kwa sababu zake binafsi!

Kubwa kuliko, ni hili la kumkataa nahodha wa timu asiongezewe mkataba kwa sababu alikataa kujiunga na klabu ya swahiba wake/ mkongomani mwenzake na pia bosi wake kwenye timu yao ya taifa( timu ya Tp Mazembe)

Ushauri wangu ni kusitisha mkataba na huyu kocha kwa maslahi ya timu maana iwapo mtaendelea kumkumbatia, basi madhara yake yatendelea kuitafuna timu kama ilivyotokea pale alipokataa kufanya kazi na Kakolanya na mwisho wa siku lile dodoki lake kuishia kufungwa magoli ya kizembe na hivyo kuchangia timu yetu kukosa ubingwa msimu uliopita. Haya ni maoni yangu!
 
Hayo yote ni ukweli au kunakusadikika, tumpe nafasi maana ndani ya uwanja ameweza ya nje yanarekebishika si tumepata uongozi kwa sasa
 
Mengine uliyoandika sijui kama ni kweli au la, ila kwa ishu ya Benno nipo na Zahera, ilifika hatua yule kijana alikuwa havumiliki! Na ile ilisaidia kidogo la sivyo hata hiyo nafasi ya 2 tusingeipata!
 
20190708_064055.jpg

Uongozi wa Yanga umeamua kulifanyia maboresho benchi lake la ufundi upande wa kocha wa makipa ambapo mlinda lango wa zamani wa timu hiyo Peter Manyika anatajwa kuchukua nafasi ya Juma Pondamali

Awali Yanga ilimuhitaji Razak Ssiwa kutoka Bandari Fc ya Kenya

Hata hivyo inaelezwa kumekuwa na ugumu kumpata mlinda lango huyo ambaye alikuwa akihusishwa kutua Yanga tangu msimu uliopita

Pondamali amekuwa kocha wa makipa wa Yanga kwa zaidi ya misimu minne

Manyika atakuwa na kazi ya kuhakikisha viwango vya walinda lango wa Yanga Farouq Shikalo, Metacha Mnata na Klaus Kindoki vinakuwa kwenye ubora wakati wote
 
20190712_163646.jpg

YANGA KUCHEZA MECHI TANO ZA KIRAFIKI,
.
.
Club ya Yanga itacheza mechi tano za kirafiki kabla ya mechi kubwa ya kirafiki na yakimataifa itakayopigwa pale uwanja wa Taifa, Kaimu katibu mkuu wa @yangasc 'Dismas Ten"-
.
.
Pia tamasha la siku ya mwanachi lasogezwa mbele kupisha mchezo wa timu ya Taifa michuano ya CHAN kuwania nafasi ya kufuzu kucheza kombe la Dunia,
.
.
Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Dismas Ten amesema timu ya Taifa itacheza na Kenya kati ya Julai 26 na 28 katika mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa ndani ndiyo sababu ya mabadiliko ya tarehe ya siku ya Wananchi,
.
.
Taarifa mpya ya tarehe nyingine ya siku hiyo ya WANANCHI itakapokuwa tayali uongozi utatujulisha,
 
YANGA SC YAWALETA AS VITA SIKU YA KILELE CHA WIKI YA MWANANCHI

Kuelekea kilele cha wiki ya mwananchi Klabu ya Yanga inawaleta As Vita kutoka nchini Congo kwa ajili ya kucheza mchezo wa kirafiki katika siku hiyo.

Makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Fredrick Mwakalebela amesema kuwa ziara ya wiki ya mwananchi itaanza Julai 28 mwaka huu na kilele chake kitakuwa Agosti 4 mwaka huu.

Sherehe hizo za kilele cha wiki ya mwananchi zitafanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 12.00 jioni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom