Young Africans Sports Club (Yanga) | Special Thread

20190510_102617.jpg
 
Mbona uzi huu umedoda? Watani wetu kumbukeni wahenga walisema kuwa "kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi"!!!! Haiwezekani siku ya mechi muhimu ya biashara Vs Yanga halafu kila mtu anakula kona wala hakuna wa kuleta updates!!!
 
Wamekata tamaa na kocha wao kasema wajipange next season.. hii imegoma
 
Zahera kuwasilisha mapendekezo ya usajili kwa uongozi Yanga

Baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, uongozi wa Yanga utakutana na kocha Mkuu wa timu hiyo Mwinyi Zahera ambapo pamoja na mambo mengine, Zahera atawasilisha mapendekezo yake ya usajili, imefahamika

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema kikao hicho ni cha pili kufanyika tangu uongozi mpya uingie madarakani

Amesema kikao cha kwanza kilikuwa cha Kamati ya Utendaji ambacho kiliweka maazimio mawili, moja; kuhakikisha Yanga inashinda michezo mitatu iliyobaki na la pili linahusu usajili "Kikao chetu kilikuwa na agenda mbili, moja ni usajili ambao tutakutana na Zahera baada ya kumaliza mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting na nyingine kumaliza ligi kwa heshima," amesema "Tulivyopewa uongozi, timu ilikuwa inaongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, hivyo tumeweka mikakati kushinda mechi zote tatu zilizobaki na kujua hatima yetu huko mbele"

Katika kikao hicho inaelezwa Zahera atawasilisha majina ya wachezaji ambao ametaka waendelee kubaki Yanga ili kuanza mchakato wa kuhuisha mikataba kwa wale ambao mikataba yao inamalizika mwishoni mwa msimu

Zahera pia atawasilisha majina ya wachezaji wapya anaotaka kuwasajili

Jumamosi ya wiki hii May 18 Yanga imeandaa tukio la futari na chakula cha jioni litakalofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ambapo kwenye tukio hilo itafanyika Harambee ya kuichangia Yanga

Wageni mbalimbali wanatarajiwa kualikwa katika Harambee hiyo wakiwemo wabunge, mashirika mbalimbali ya Serikali na binafsi, taasisi za dini na wadau wote wenye mapenzi na Yanga

Aidha siku hiyo Kamati ya Hamasa itakabidhi kwa uongozi kiasi cha fedha ambazo zimekusanywa tangu kuanzishwa kwa kampeni ya kuichangia Yanga
 
Itapendeza kama itakuwa mikakati ya kiukweli na wasifanye siasa kwenye mpira
 
Kamati ya Utendaji kwa kutumia mamlaka iliyopewa na Ibara ya 28 (1) (d) ya Katiba ya Yanga ya mwaka 2010, imefanya uteuzi wa wanachama wafuatao kuwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga.

1. Dkt Athumani Kihamia - Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)

2. CPA Shija Richard Shija - Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Uteuzi huo unaanza mara moja.

Katiba hiyo imetoa mamlaka kwa Kamati ya Utendaji ya Yanga kufanya uteuzi wa wajumbe watatu wa Kamati ya Utendaji.

Uteuzi wa mjumbe mmoja aliyesalia utafanyika baadaye.
 
Upo vizuri sana Shadeeya kwenye vipengele vya katiba, pamoja na kwamba Yanga na mimi mbalimbali ila hapo nimekukubali
 
Uwiiii! Sio siri Ses umefanya nimecheka asubuhi asubuhi. lol

Nimeikuta sehemu hii nikaamua nishare na wapenzi wenzangu wa Timu ya Wananchi na huko ndio nmekuta wameweka na hicho kifungu. 😀😀
Hahahaha sawa Mama Yanga, ila uhakikishe pia unatumia hivo vipengele vya katiba kuwabana kina Mzee Akilimali na wenzie watapoanza kuwawashia moto viongozi wapya pale mtakapokua mnapokea kichapo kutoka Msimbazi:D
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom