You left for the city, you promised to come back to take care of us!

musa yasini

Member
Dec 15, 2020
28
36
Nahuzuni moyoni mimi siimbi nalia,
Ulituahidi mengi, binafsi nayalilia,
"Hapa kazi tu!" ndio kauli uliyotuachia,
kwa bidii tulijituma, na mengi tuliachilia,
Ulitufundisha uzalendo, kazi kwanza mazuri yangetujilia,

Uwajibikaji kwanza, ndo kigezo cha kuinuliwa,
Tumbuatumbua, "surgeon" kazi ulipewa,
Wengine chamoto walikiona, wengine walidai kuonewa,
Wapo wakiokimbia, na hifadhi kupewa!
Sijui ni kwa ujinga au ni kili zao, au na mabeberu walitumwa?
Kazi ulifanya kweli, baba sifa na shukrani pewa,

Ulisimama imara, kipindi cha korona,
Wengi walibeza, wengine tulipona!
Tuliwapuuza "mabeberu" , tiba mbadala imefana?
Miradi ilikuwa lukuki, matunda yalikua bado kunona!
Ujinga wa ukubwani, ulikua bado kila kona,
Ndio ikaja elimu bure, shule hata kama sare hujashona!

Haya yote yatoshe, ninalo langu jambo!
Uliahidi mazuri kazini kwangu, na hilo ndio jambo,
Sita miaka kazini, sijamiliki hata pikipiki bado!
kwani ndugu zangu, nasema uongo?
nyumba nayoishi (kazini), darini imejaa popo,
nimekwenda kwa huzuni ya wangu moyo,
Nikaamini ndio tuko vita ya uchumi hio!

Tumaini bado silioni, mimi mtoto wa mkulima,
Ingawa nimesoma, bodi bado inaniandama,
Badala ya kufaidi maziwa, bodi iko kwa nyuma!
Familia haiko nami, na sitakiwi kuhama,
Natamani ashikaye hatamu, abebe dhamana,
Na ahadi za babayetu kwetu, ziwe kwetu amana,
Ndipo taposema "kidumu chamaaa!!"
 
Back
Top Bottom