Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,756
- 40,930
01.05.2008 1712 EAT
PORIS wapendekeza rushwa ifundishwe shule za msingi nchini (RAI)
SHIRIKA lisilo la kiserikali la African International Group of Political Risk Analysis (PORIS), limependekeza mitaala ya shule za msingi nchini kuhusisha somo la rushwa.
Ushauri huo ulitolewa na washiriki katika semina ya siku mbili iliyofanyika katika Hoteli ya Paradise mjini Bagamoyo wiki hii. Walisema kwa hali ilipofikia ni wazi maadili yamepotea kwa kiwango kikubwa nchini, hivyo wakaomba ikiwezekana elimu ya rushwa ianze kufundishwa kuanzia ngazi ya shule za msingi.
Mbali na shule za msingi, wameomba serikali iangalie uwezekano wa kushirikisha viongozi wa dini zote katika vita dhidi ya rushwa. "Hii iwe ajenda ya kitaifa. Masheikh misikitini wahubiri vita dhidi ya rushwa. Mapadre nao wafanye hivyo altare, wale wa CDA nao wasisite kuhubiri vita dhiti ya rushwa kila Jumamosi. Kwa njia hii pengine masikio yatazibuka," alisema Mkurugenzi Mtendaji wa FiorDIA, Bubelwa Kaiza.
Kaiza alisisitiza kuwa tatizo kubwa linalolikabili taifa hili ni uwezo (capacity) wa watendaji serikalini, wananchi na katika taasisi mbalimbali kwani wengi hawafahamu haki na wajibu wao. Alisema kazi ya kwanza inayopaswa kufanywa ni kujenga mfumo na uwezo kwa wananchi wote, ili kila mmoja ajue haki na wajibu wake na hilo litaondosha mazingira ya rushwa kwa kiwango kikubwa.
Mkurugenzi Mkuu wa PORIS, Prince Bagenda, ilisema ikibidi taifa litafute mahala pa kuazima maadili na mienendo bora kwani katika mfumo wa sasa baadhi ya watu wana nguvu kuliko sheria zilizopo. "Tupo katika mazingira ya hatari. Maafisa wanaingia mikataba na hakuna mtu mwenye uwezo wa kuiona. Hata wabunge hawaruhusiwi kuiona. Hii ni hatari. Wananchi wanapaswa kupata haki ya kuona mikataba hii," alisema Bagenda.
Mwambata wa Ubalozi wa Ubeligji nchini, Herman Boonen, alisema Serikali ya Awamu ya Nne imeanza vizuri hivyo ipewe muda katika vita dhidi ya rushwa. Alisisitiza kuwa kwa nchi yoyote kuendelea katika mapambano dhidi ya rushwa inapaswa kuhakikisha inaimarisha mifumo ya utawala bora na uwajibikaji.
Pia alisema wananchi wanapaswa kushirikishwa katika maamuzi, kupata taarifa zote ndani ya serikali na kuhusika katika maamuzi. Kwake anaona kuwa uwazi una nafasi kubwa ya kusaidia kuondoa vitendo vya rushwa. Ubeligji ndiyo iliyofadhili warsha hiyo.
Mada kuu katika warsha hiyo ilikuwa ni kupitia maazimio ya Brussels ya mwaka 2007 juu ya mapambano dhidi ya rushwa, jukumu la vyombo visivyo vya kiserikali katika mapambano dhidi ya rushwa Tanzania na mada ya mwisho ilikuwa juu ya Jinsia na Rushwa. Pia warsha hiyo ilitumika kuzindua kitabu kilichoandikwa na Bagenda kiitwacho Improving Governance