Yote yalikuwa majungu, huu ndiyo ukweli sasa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Yote yalikuwa majungu, huu ndiyo ukweli sasa...

Discussion in 'International Forum' started by Mwanjelwa, Dec 17, 2008.

 1. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2008
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hakika sasa iko wazi. Licha ya kushabikia sana kuchelewesha kwa jumuiya hii, bado nilikuwa sijaju kwenye inner cycles kuna nini hasa. Kumbe.........

  Tanzania yaonya kusambaratika EAC

  Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) iko hatarini kusambaratika kama ilivyotokea mwaka 1977, ikiwa baadhi ya nchi wanachama zitaendekeza unafiki na ubinafsi katika Jumuiya hiyo, Tanzania imeonya.

  “Hatuwezi kuendesha Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ubinafsi, unafiki tukiendekeza mambo hayo na lile la ukabila, Jumuiya itavunjika kwani mambo hayo hayajengi, tutaibomoa EAC,” ameonya Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Dk. Diodorus Kamala.

  Alikuwa akifungua mkutano wa siku moja hapa jana ulioandaliwa na wananchi wa Wilaya ya Mjini Unguja kuhusu mchakato wa kuwa na soko la pamoja. Alisema tatizo la ujanja ujanja na ubinafsi linaloonekana kuweka mizizi katika jumuiya hiyo, litaipeleka pabaya ikiwa hatua madhubuti hazitachukuliwa kulikomesha.

  Alisema Tanzania imejitolea kutoa elimu ya bure kwa nchi nyingine za EAC namna ya kupiga vita ukabila. Alisema tangu kuundwa kwa jumuiya hiyo, kero nyingi zimeongezeka ikiwamo vikwazo vya kibiashara vikiwasumbua wananchi kwani bado kuna vikwazo visivyo kuwa vya kodi vinawekwa na baadhi ya mataifa wanachama.

  “Ukiniuliza tumefaidika nini nitakujibu kuwa badala ya mategemeo ya kupungua na kuondoka kabisa, ndio kwanza vikwazo vimeongezeka,” alisema na kuzitaka nchi hizo kuacha unafiki na ujanja ujanja kwani hakusaidii kuimarisha EAC.

  Alisema mtindo wa baadhi ya nchi za EAC kukataa bidhaa fulani kuingia katika nchi nyingine ni mambo yatakayosababisha kuyumba na kulegalega kwa jumuiya hiyo ambayo imeundwa tena baada ya ile ya zamani kuvunjika mwaka 1977.

  Alitoa mfano wa nyama ya Tanzania inayopelekwa na wafanyabiashara kutoka Simbawanga kuwekewa vikwazo Kenya; maziwa yanayozalishwa mkoani Mara pamoja na magari ya mizigo kukataliwa kufanya kazi katika nchi mojawapo (hakuitaja), ni mambo ambayo hayaonyeshi nia njema katika ushirikiano huo ambao awali ulivunjika kwa mambo ya kutokuaminiana mwaka 1977.

  Alisema kutokana na kutokuwapo kwa dhamira njema na ubinafsi wa nchi wanachama wamediriki hata kudai nafasi za ajira kama za uhudumu, udereva na ulinzi kwa zile taasisi za jumuiya zinazokuwapo katika nchi mojawapo, jambo alilosema ni kinyume cha mkataba wa kuanzishwa kwa EAC.

  Alikanusha na kuwakemea wanaodai Tanzania inachelewesha Soko la Pamoja, na kusisitiza kuwa msimamo wa nchi utaendelea kubaki ule ule katika mambo matatu; ardhi kubakia mikononi mwa Watanzania; matumizi ya pasi za kusafiria yabakie kama yalivyo pamoja na kupinga kuwapo kwa ukazi wa kudumu.
   
 2. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2008
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180


  Mwanjelwa, thanks for the quote ambayo hata mimi nimeiona gazetini leo asubuhi.
  Nafikiri tunafikia bottom line ya uhusiano wetu na wenzeto hasa Kenya na Uganda.
  Hawa jamaa ndo walivyo ukiwapakia ukweli wao wanalia kuwa tuna watumia hate mail!!
  Wataka kutufanya shamba la bibi.
   
Loading...